Thursday, 30 June 2016
Uturuki kuziba nafasi ya Uingereza EU
Ukurasa mpya umefunguliwa katika juhudi za Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya huku mashauriano kuhusu kuchangia bajeti yakianza mjini Brussels.
Sura ya 33 inayohusiana na maswala ya kifedha na bajeti imefunguliwa mapema leo.
Uturuki lazima itimize kurasa 35 za uanachama wa Ulaya lakini kurasa tano bado zimezuiliwa kutokana na Ankara kutotambua Cyprus kama taifa.
Hatua ya Ankara ya kujiunga na Umoja wa Ulaya imekuja wiki moja tu baada ya Uingereza kuamua kujitoa kwenye muungano huo jambo ambalo Waziri wa Umoja huo kutoka Uturuki, Omer Celik, amesema litaimarisha nafasi ya nchi yake hata zaidi kwenye muungano huo.
Watu wengi kutoka Ulaya wanapinga uanachama wa Uturuki kutokana na sababu nyingi wengi wakihofia wingi wa waislamu walioko pamoja na hofu kwamba hatua hiyo itafungua milango kwa wahamiaji kuingia mataifa mengine ya Ulaya.
Labels:
Kimataifa
Location:
Brussels, Ubelgiji
Kundi la Tembo lavamia na kuharibu mazao mashambani Uganda
Kundi la tembo (Ndovu) kutoka mbuga ya Nimule nchini Sudan Kusini wamekuwa wakivuka na kuingia Kaskazini mwa Uganda na kuharibu mashamba ya mahindi, mihogo, viazi na pamba.
Maurice Vuzi ambaye ni mwenyekiti wa wa kaunti ndogo ya Dufile, alisema kuwa ndovu hao waliharibu zaidi ya ekari 35 ya mimie siku ya Jumatatu.
Wakulima wanasema kuwa hawajui hatma yao kwa sababu kila ifikapo msimu wa kuvuna, ndovu uharibu mazao yao na wakati huu ndovu wanafika wakiwa wengi.
Mkulima moja aliliambia gazeti la Daily Monitor kuwa hili limesababisha kushuhudiwa uhaba wa chakula katika vvjiji vilivyo eneo hilo.
Makanisa na Misikiti yafungwa Lagos, kisa ni nini?
Mamlaka katika mji wa Lagos nchini Nigeria umefunga makanisa 60 na misikiti 20 katika jitihada za kupunguza kelele.
Karibu hoteli kumi na klabu kadha nazo zilifungwa. Mji wa Lagos una karibu watu milioni 10 huku honi za magari, maombi kutoka misikitini na nyimbo makanisani vikitawala mji huo.
Mwezi Agosti utawala ulifunga maeneo 22 baada ya wenyeji kulalamika kutokana na kele zilzokuwa zikitoka maeneo hayo.
Labels:
Habari kutoka Afrika
Location:
Lagos, Nigeria
Tishio la Dola la Kiislam kuikumba Kenya
Imebainika kwamba ushawishi wa kundi la Dola la Kiislamu Afrika Mashariki umeongezeka kwa kuwaandikisha vijana wa Kenya kuendesha mapambano ya jihadi nchi za nje na baadhi yao kurudi Kenya kuitishia nchi hiyo.
Mashirika ya ujasusi nchini Kenya yanakadiria kwamba takriban wanaume na wanawake 100 yumkini wakawa wamekwenda kujiunga na kundi la Dola la Kiislamu nchini Libya na Syria na kuzusha wasi wasi kwamba baadhi yao huenda wakarudi nchini humo kufanya mashambulizi kwa Kenya na katika vituo vya kigeni, katika nchi ambayo tayari ni muhanga wa mashambulizi ya kigaidi yanayofanyika kila mara nchini humo.
Rashid Abdi mchambuzi mwandamizi katika Shirika la Kimataifa la Kushughulikia Mizozo ambalo ni jopo la ushauri lilioko katika mji mkuu wa Kenya Nairobi amesema, "Kwamba hivi sasa kuna tishio la kweli linaloikabili Kenya kutoka kundi la Dola la Kiislamu na hatari hiyo itazidi kuongezeka."
Tatizo la wafuasi wa itikadi kali ambao mara nyingi ni watu wenye shauku lakini wasiokuwa na mafunzo, kupatiwa mafunzo stadi ya kigaidi na kundi la Dola la Kiislamu na kurudi nyumbani kufanya mashambulizi ni tatizo ambalo tayari mataifa ya Ulaya yanakabiliana nalo na yumkini hivi karibuni likawa pia ni tatizo kwa Kenya.
Mshauri elekezi wa masuala ya usalama na afisa polisi wa zamani George Musamali ameliita hilo kuwa ni "bomu linasubiri kuripuka."Amesema watu kwenda Libya au Syria sio tatizo kwa Kenya tatizo ni kile watakachokifanya wakati watakaporudi.
Wanajeshi wa Kenya kufuatia shambulio katika chuo kikuu cha Garissa 2015.
Shambulio la kwanza la kigaidi la Al-Qaeda nchini Kenya ilikuwa ni kuripuliwa kwa ubalozi wa Marekani hapo mwaka 1998 na hivi karibuni kabisa yalikuwa ni mauaji katika chuo kikuu cha Garissa mwaka jana lakini tishio la Dola la Kiislamu ni jipya na bado kueleweka vyema.
Hapo mwezi wa Machi wanaume wanne walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutaka kwenda Libya kuijunga na kundi la Dola la Kiislamu.
Baadae hapo mwezi wa Mei polisi ya Kenya ilitangaza kukamatwa kwa mwanafunzi wa udaktari,mke wake na shoga yake wanaotuhumiwa kuwaandikisha watu kujiunga na kundi la Dola la Kiislamu na kupanga shambulio la kibiolojia kwa kutumia anthrax.
Inasemekana wanafunzi wengine wawili wa udaktari wamekimbia.
Wanafunzi wa Kenya katika kumbukumbu ya shambulio la chuo kikuu cha Garissa.
Wiki tatu baadae polisi ya Kenya ilitangaza kukamatwa kwa wanachama wengine wawili wa mtandao wa kundi la Dola la Kiislamu ambao ulikuwa ukitaka kujipenyeza Kenya ili kuweza kufanya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Wakenya wasiokuwa na hatia.
Polisi ilisema imegunduwa vitu ambayo hutumiwa na magaidi kutengeneza mabomu ya kienyeji pamoja na mikuki na mishale iliotiwa sumu.
Wakati baadhi ya wataalamu wanatupilia mbali ishara ya shambulio kubwa lainyemelea Kenya wanakiri kwamba kuna tishio la dhati la kundi la Dola la Kiislamu kupandikiza itikadi kali,kuandikisha watu kujiunga nalo na baadae kuwarudisha nyumbani.
Labels:
Ugaidi
Location:
Nairobi, Kenya
Jambazi sugu Dar mikononi mwa Polisi
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa sugu wa ujambazi aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu Abdallah Bushiri Said ambaye anadaiwa kushiriki matukio mbali mbali ya Uporaji na mauaji ambaye pia anadaiwa kuwa mshirika Mkuu wa Abuu Seif aliyeuawa juzi wakati wa mapambano na Polisi eneo la Buguruni jijini Dar es salaam.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum CP Simon Siro amesema mtuhumiwa huyo ambaye anashikiliwa amekiri kuhusika na matukio makubwa ya unyang’anyi wa kutumia silaha ikiwemo ya mabenki, matukio ya uporaji wa silaha katika vituo vya polisi likiwemo la sitaki shari.
Aidha, jeshi hilo limetangaza kumsaka mtuhumiwa mwingine hatari wa ujambazi Heri Suleiman Mpopezi mwenye asili ya Pemba ambaye alikuwa mwajiri wa kikosi cha JKU Zanzibar na kuacha kazi na kujitumbukiza katika ujambazi wa kutumia silaha.
Lissu akana mashtaka na kuachiwa kwa dhamana
MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) amesomewa shitaka lake la kutoa maneno ya uchochezi kinyume cha kifungu namba 32 cha sheria ya magazeti.
Lissu anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mnamo June 28, 2016 kwa kumuita ‘Mkuu wa Nchi ni dikteta uchwara’.
Baada ya kusomewa shtaka hilo Lissu amekana shtaka na kuachiwa huru kwa dhamana na hatotakiwa kusafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Agosti 02, 2016.
Mbunge Sugu ahukumiwa, vikao 10 vya Bunge kuvisikilizia nje ya Bunge
Bunge limeridhia pendekezo la adhabu ya kumsimamisha vikao 10 kuanzia leo Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi baada ya kutiwa hatiani na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kudharau mamlaka ya Spika.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kepten Mstaafu George Mkuchika alisema alinyoosha kidole cha kati kwenda juu cha mkono wa kulia huku vingine akivikunja jambo ambalo ni matusi na dharau kwa mamlaka ya Bunge.
Naibu Spika Dk Tulia Ackson amewasimamisha Wabunge wengine wawili wa Ukawa,ambao ni Mbunge wa Ubungo (Chadema) Saed Kubenea kwa kutohudhuria vikao vitano kuanzia leo baada ya kutiwa hatiani na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwa alisema uongo Bungeni.
Mbunge mwingine aliyesimamishwa ni Mbunge wa Simanjiro (Chadema) James Ole Millya kutohudhuria vikao vitano kuanzia leo baada ya kutiwa hatiani na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwa alisema uongo Bungeni.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameanza kutoa hotuba ya kuahirisha Bunge na kueleza bajeti ni ya kihistoria tangu nchi ipate uhuru kwa kutenga asilimia 40 ya Sh. 29.5 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kepten Mstaafu George Mkuchika alisema alinyoosha kidole cha kati kwenda juu cha mkono wa kulia huku vingine akivikunja jambo ambalo ni matusi na dharau kwa mamlaka ya Bunge.
Naibu Spika Dk Tulia Ackson amewasimamisha Wabunge wengine wawili wa Ukawa,ambao ni Mbunge wa Ubungo (Chadema) Saed Kubenea kwa kutohudhuria vikao vitano kuanzia leo baada ya kutiwa hatiani na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwa alisema uongo Bungeni.
Mbunge mwingine aliyesimamishwa ni Mbunge wa Simanjiro (Chadema) James Ole Millya kutohudhuria vikao vitano kuanzia leo baada ya kutiwa hatiani na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwa alisema uongo Bungeni.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameanza kutoa hotuba ya kuahirisha Bunge na kueleza bajeti ni ya kihistoria tangu nchi ipate uhuru kwa kutenga asilimia 40 ya Sh. 29.5 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Labels:
Bungeni
Location:
Dodoma, Tanzania
Baada ya mbinu ziba mdomo, UKAWA waja na mbinu nyingine; wavaa Suti nyeusi na kubeba mabango yakimtaja JPM na Tulia
Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani leo asubuhi wameingia bungeni wakiwa wamevalia nguo nyeusi wote walipohudhuria kikao cha 54 cha Bunge la Bajeti mjini Dodoma.
Baada ya Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson kuingia bungeni na kuongoza dua ya kuliombea Bunge, walianza kunyanyua mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakitoka nje ya ukumbi wa bunge hilo.
Akizungumza nje ya ukumbi wa bunge mjini dodoma mara baada ya kutoka nje, Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia, amesema hawajatoka wala kulikimbia bunge, na kwamba wapo bungeni na wanaendelea kufanya kazi za bunge.
“Hatujakimbia bungeni, tunashiriki kwenye kamati, hatujasusia bunge, tumechukizwa, tuna hasira na vitendo vya kibabe, vya kionevo vinavyofanywa na kiti.” Alisema Mbatia
Baada ya Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson kuingia bungeni na kuongoza dua ya kuliombea Bunge, walianza kunyanyua mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakitoka nje ya ukumbi wa bunge hilo.
Akizungumza nje ya ukumbi wa bunge mjini dodoma mara baada ya kutoka nje, Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia, amesema hawajatoka wala kulikimbia bunge, na kwamba wapo bungeni na wanaendelea kufanya kazi za bunge.
“Hatujakimbia bungeni, tunashiriki kwenye kamati, hatujasusia bunge, tumechukizwa, tuna hasira na vitendo vya kibabe, vya kionevo vinavyofanywa na kiti.” Alisema Mbatia
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Dodoma, Tanzania
Bomu laripuka na kuua watu 18 Somalia
Habari kutoka Somalia zinasema kuwa watu 18 wameuawa baada ya bomu kulipuka na kuharibu kabisa basi walimokuwa wakisafiria katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara lililipua gari lililokuwa limewabeba abiria. Wote waliouawa walikuwa raia.
Mashambulizi hayo yalitokea katika mji wa karibu wa Lafole.
Inadhaniwa kuwa washambuliaji hao walikuwa wakilenga gari la wanajeshi lililokuwa karibu.
Mara kwa mara wapiganaji wa Al-Shaabab hulenga wanajeshi wa Serikali.
Mwandishi maarufu wa "The Concubine" afariki dunia
Mwandishi maarufu wa Nigeria Elechi Amadi amefariki akiwa na umri wa miaka 82.
Amadi ambaye aliandika vitabu maarufu kama vile The Concubine, Isiburu, Sunset in Biafra, Peppersoup na The Road to Ibadan alifariki siku ya Jumatano mwendo wa saa tisa,wiki moja moja baada ya kuripotiwa kuugua.
Duru zimearifu kuwa marehemu alitarajiwa kuhudhuria hafla ya kusoma vitabu katika bandari ya Hacourt lakini hakuweza kutokana na kuugua kwake.
Akiwa mzaliwa wa eneo la Aluu katika jimbo la Riverstate mwaka 1934, Elecchi Amadi alisoma katika taasis ya Umuahia, Oyo na chuo kikuu cha Ibadan ambapo alipata shahada yake katika somo la fizikia na hisabati.
Pia aliwahi kufanya kazi kama mpimaji wa mashamba.
Labels:
Habari kutoka Afrika
Location:
Nigeria
Joseph Kabila asema hakuna kizuizi cha Uchaguzi DRC
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, Joseph Kabila, amesema Serikal yake iko tayari kwa mazungumzo ya kitaifa yatakayoshirikisha pande zote, na kutoa wito kwa wanasiasa wa nchi hiyo kuheshimu katiba wanapodai haki yao.
Rais Kabila amesema haya kwenye hotuba yake aliyoitoa usiku wa kuamkia leo wakati huu nchi hiyo ikiadhimisha kumbukumbu ya miaka 56 ya uhuru wa taifa hilo kutoka kwa Wabelgiji.
Rais Kabila, amesema hakuna njia ya mkato ambayo nchi yake inaweza kupitia kufikia suluhu ya kisiasa, na kwamba mapendekezo yaliyotolewa na mpatanishi aliyeteuliwa na umoja wa Afrika, Edem Kodjo, hakuna anayeweza kuyageuza ambapo amemtaka mpatanishi huyo kuharakisha kuanza kwa mchakato wa mazungumzo.
Kabila pia aligusia kuhusu matayarisho ya kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika mwaka huu, ambapo akawakumbusha wanasiasa nia yake aliyoonesha mwaka jana ya kuitisha mazungumzo ya kitaifa yaliyolenga kutathmini na kukubaliana namna bora ya kuandaa uchaguzi mkuu uliokuwa wa huru, haki na wenye kuaminika, nia ambayo amesema bado anayo.
Hotuba ya rais Kabila mbali na kugusia utangamano wa kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu, amewapongeza wananchi wa taifa hilo kwa kuendelea kudumisha amani, huku akiapa kuendelea na juhudi za kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana kwenye eneo la mashariki mwa nchi ambalo linakabiliwa na uasi wa makundi ya wapiganaji wenye silaha.
Rais Kabila ameendelea kusisitiza kuwa uchaguzi wa taifa hilo utafanyika kwa misingi ya kidemokrasia na kwamba hakuna suala ambalo litatatiza uchaguzi huo usifanyike kwa muda uliopangwa, kauli inayotoa matumaini ya kufanyika kwa uchaguzi mwaka huu.
Amerika Kaskazini watetea Utandawazi
Viongozi wa Marekani, Canada na Mexico wamekataa kwa kiasi kikubwa mpango wa kulinda biashara na kutokuunga mkono utandawazi katika mkutano wa viongozi wa Amerika kaskazini uliofanyika siku ya Jumatano mapema wiki hi.
Rais wa Marekani Barack Obama, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau na rais wa Mexico Enrique Penya Nieto walisifu faida za mkataba wa biashara huru wa Amerika kaskazini (NAFTA) uliodumu kwa miaka 22 katika wakati ambapo biashara za kimataifa zinashambuliwa Marekani na Ulaya . Kwa pamoja nchi hizo tatu zinajumuisha asilimia zipatazo 27 ya uchumi duniani.
Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau alisema mkutano huo ulikuwa wa huzuni kidogo kwasababu ya kile alichokiita matarajio ya kustaafu rais Obama. Watatu hao walieleza urafiki wao wa karibu na jinsi wanavyoheshimiana na kusisitiza neno la “3 amigos” –ikimaanisaha marafiki watatu jina la utani ambalo vyombo vya habari vimewapa.
Obama, Trudeau na Pena Nieto walikubaliana kuunga mkono uzalishaji wa nishati safi kwa Amerika kaskazini katika miaka 10 ijayo wakilenga kuzalisha nusu ya umeme wa Amerika Kaskazini kutoka kwenye vyanzo visivyokuwa Carbon ifikapo 2025.
Labels:
Kimataifa
Location:
North America
Bilioni 33 zatengwa kukarabati Shule kongwe 88 Tanzania Bara
Serikali ya Awamu ya Tano imetenga Sh bilioni 33 kwa ajili ya mpango maalum wa ukarabati mkubwa na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali, yakiwemo majengo ya madarasa, mabweni na nyumba za walimu katika shule kongwe za sekondari za serikali nchini.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, alisema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango huo katika Shule ya Sekondari ya Mzumbe iliyopo Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Profesa Ndalichako alisema mpango huo wa miaka miwili utahusisha shule kongwe 88 za serikali kwa kufanyiwa ukarabati mkubwa wa miundombinu, majengo ya madarasa, nyumba za walimu, mabweni, majengo ya chakula na uboreshaji wa maabara na vitendea kazi vyake.
Waziri huyo alikuwa pia mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Elimu Tanzania iliyofanyika juzi kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mzumbe na kuhudhuriwa na wadau wa sekta ya elimu wakiwemo wakuu wa shule za sekondari za serikali na maofisa elimu wa mikoa kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
Alisema utekelezaji wa mpango huo unatarajia kuanza wakati wotote baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Serikali na kuanza kutumika na utaanza kwa awamu ya kwanza ambako shule kongwe 33 zitahusika.
“Tumekadiriwa kuwa kila shule itagharimu shilingi bilioni moja na kwa maana hiyo shule 33 zimeingizwa awamu ya kwanza. Fedha hiyo inaweza ikapungua kulingana na mazingira ya kitadhimini ya uchakavu wa majengo,” alisema Profesa Ndalichako.
Alisema uboreshaji wa elimu ni pamoja na ubora wa majengo na miundombinu mingine katika shule hizo, na lengo la kuzirejesha katika uhalisia wake wa zamani wa kuwa na mandhari nzuri za kuvutia wanafunzi, walimu na wazazi.
“Shule hizi tumeziweka katika mpango maalumu wa miaka miwili kukarabatiwa majengo yake, miundombinu ya kufundishia, vifaa vya kila somo, vitabu vya kufundishia na kujifunzia, vifaa vya kutosha vya maabara na kuboresha makazi ya walimu,” alifafanua Profesa Ndalichako.
Naye Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais Tamisemi, Juma Kaponda, alimpongeza Waziri Ndalichako kwa kusimamia uboreshaji wa shule kongwe za sekondari na kuomba wadau mbalimbali waliosoma shule kongwe hizo na wanazo nyadhifa kubwa serikalini na sekta binafsi kuona wanao wajibu wa kuchangia maboresho hayo.
Labels:
Elimu
Location:
Morogoro, Tanzania
Zanzibar kupata Nishati ya uhakika
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imeweka malengo ifikapo mwaka 2020 itahakikisha vijiji vyote vya Unguja na Pemba vinapata huduma ya nishati ya uhakika ya umeme.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Maji, Nishati, Ardhi na Mazingira, Juma Makungu Juma, wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Ole, Said Omar Mjaka aliyetaka kufahamu lini huduma ya nishati ya umeme zitapatikana Zanzibar.
Juma alisema kwa sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanikiwa kusambaza huduma ya nishati ya umeme kwa asilimia 86 kwa wananchi wake wa Unguja na Pemba.
Alisema mafanikio hayo yamekuja zaidi baada ya kisiwa cha Pemba kuunganishwa na Gridi ya Taifa kutoka Tanga kwa msaada mkubwa wa Serikali ya Norway.
“Mheshimiwa Spika napenda kulijulisha Baraza la Wawakilishi kwamba katika kipindi cha miaka minne ijayo visiwa vya Unguja na Pemba vitakuwa vimefaidika na huduma za usambazaji wa nishati ya umeme,” alisema Naibu Waziri.
Alisema kwamba matumizi ya nishati ya umeme faida zake ni kubwa ambapo katika baadhi ya vijiji vimefanikiwa kupiga hatua kubwa ya maendeleo.
Alisema serikali ipo katika hatua za mwisho za kusambaza huduma ya umeme katika baadhi ya visiwa wanavyoishi wananchi huko Pemba.
Wapinzani Kisiwani Zanzibar watishia kumshtaki JPM ICC
Polisi katika kisiwa cha Pemba visiwani Zanzabar nchini Tanzania imepinga vikali kuwa inavunja haki za binadamu kwa kuwatesa na kuwashikilia wapinzani.
Hata hivyo limekiri kuwashikilia baadhi ya wapinzani kwa madai kwamba ni wahalifu.
Hapo jana Muungano wa Upinzani nchini Tanzania ulitoa kauli ya kulaani Polisi huko Pemba kwamba imekuwa ikiwapiga, kuwatesa na kuwafungulia kesi za bandia wafuasi wa upinzani .
Muungano huo tayari umetishia kumpeleka Rais wa Tanzania John Magufuli kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC iwapo hataingilia kati mgogoro huo unaoendelea visiwani humo.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Pemba, Zanzibar
Uwanja wa Ndege watwaliwa na Waasi nchini Syria
Wapiganaji wa waasi wa Syria wanaosaidiwa na Marekani walichukua udhibiti wa uwanja mdogo wa ndege uliotumika kama kambi na kundi la Islamic State karibu na mpaka wa Irak mapema hapo jana.
Kambi ya jeshi la anga huko Hamdan ilitumika kama kituo muhimu cha kijeshi cha Islamic State karibu na mji wa Al-Bukamal, kilomita chache kutoka Irak.
Kambi hiyo ya jeshi la anga ilitekwa saa kadhaa baada ya kuanzishwa mashambulizi siku ya Jumanne yaliyokuwa na lengo la kufunga njia inayotumiwa na kundi la ugaidi kuingia Syria na Irak.
Kundi la Islamic State lilichukua udhibiti wa Al-Bukamal mwaka 2014 kwa ajili ya operesheni zao za kijeshi na mara moja kuondoa mpaka kati ya Irak na Syria.
Labels:
Ulinzi na Usalama
Location:
Syria
Dr. Besigye kutinga Mahakamani bila Mawakili wake
Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama kikuu cha upinzani nchini Uganda, Dr. Kizza Besigye, anayekabiliwa na mashtaka ya uhaini, Jana alipandishwa tena kizimbani kwenye mahakama ya Uganda, ambapo alijiwakilisha mwenyewe bila ya mawakili wake.
Besigye ambaye toka kushikiliwa kwake ameshapandishwa kizimbani kwenye mahakama kadhaa za Uganda, kwenye maeneo tofauti tofauti ya nchi, hali ambayo mawakili wake wanasema wanashindwa kumuwakilisha vema.
Besigye alitarajiwa kupanda kizimbani bila kuwa na mawakili wake, katika kile alichosema ni hujuma zinazofanywa dhidi yake kuhakikisha anakosa wawakilishi muhimu kwenye kesi ambayo ameendelea kusisitiza kuwa imepikwa kisiasa kummaliza.
Mmoja wa mawakili wake, Yusuf Nsibambi, amesema wao kama wataalam wa sheria wanashindwa kumuwakilisha Besigye inavyopaswa kutokana na kutokuwepo kwa mahakama moja inayosikiliza kesi yake, na kwamba wanaona ni kama tayari ameshahukumiwa kuliko madai ya Serikali kuwa anashtakiwa.
Wafuasi wa Besigye, wanaharakti pamoja na wanasiasa wengine nchini Uganda, wamekosoa namna kesi hiyo inavyoendeshwa wakisema siasa imeingia hadi kwenye mfumo wa kimahakama, kwa kuwa kiongozi huyo hapati haki yake kisheria kama inavyotamkwa kwenye katiba ya nchi.
Besigye mwenyewe ameendelea kushikilia msimamo wa kujiwakilisha mwenyewe kwa kile anachosema ni kudai haki yake popote pale atakaposomewa mashtaka hata kama sio kwenye mahakama moja inayofahamika.
Labels:
Haki na Sheria
Location:
Kampala, Uganda
EU: Uingereza marufuku kuhudhuria mkutano wa EU
Nchi ya Uingereza imepigwa marufuku kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ulaya. Kwa sasa mkutano huo utakua ukihudhuriwa na viongozi kutoka nchi 27 badala ya 28, baada ya Uingereza kuamua hivi karibuni kujitoa katika Umoja huo.
Uamuzi huu umemshangaza Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, ambaye ametakiwa kutokuwepo wakati viongozi 27 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya watakuwa wakikutana katika kikao kisicho rasmi juu ya mustakabali wa muungano huo baada ya kuondoka kwa Uingereza.
Baraza la Ulaya lilikutana Jumanne hii, baada ya Uingereza kuamua kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, katika muktadha wa kutafakari jinsi ya kuimarisha uchumi, maendeleo na ushirikiano katika umoja huo.
Jumatatu wiki hii Juni 27, Angela Merkel, François Hollande na Matteo Renzi walikutana mjini Berlin kwa maandalizi ya mkutano wa Baraza la ulaya ambao ulifanyika Jumanne hii mjini Brussels. Viongozi hao watatu walitoa kauli mmoja ya kupinga mazungumzo na London kabla ya kurasimisha uamuzi wake wa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.
Angela Merkel, François Hollande na Matteo Renzi wameonyesha msimamo pamoja dhidi ya kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. Viongozi hao walithibitisha hayo walipokutana Jumatatu hii mjini Berlin. Walisema hakutakuwa na mazungumzo na London kama Uingereza itakua bado haijarasimisha ombi lake la kujiondoa katika Umoja wa Ulaya kwa Baraza la Ulaya.
Rais wa Umoja wa Ulaya, Jean-Claude Junker, amesema kuwa shughuli za kutegua kujiondoa kwa Uingereza kutoka muungano huo zinapaswa kutekelezwa baada tu ya Uingereza kumpata Waziri Mkuu mpya.
Mapigano makali yaripotiwa kusini mwa Burundi
Mapigano makali yanaripotiwa tangu Alhamisi hii Asubuhi katika kijiji cha Mubuga mtaa wa Gasanda, mkoani Bururi, kusini mwa Burundi. Mapigano hayo ni kati ya vikosi vya usalama vikishirikiana na jeshi na kundi la waasi.
Mpaka sasa hasara kufuatia mapigano hayo haijajulikana, lakini chanzo cha polisi kinabaini kwamba mpiganaji mmoja ameuawa na watu wawili wamejeruhiwa, huku wapiganaji watano wakikamatwa na silaha zao.
Kiongozi wa vijana wakereketwa wa chama madarakani (Imbonerakure) na askari polisi wamejeruhiwa kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Bururi, Christian Nkurunziza.
“Mapema asubuhi tulipata taarifa kwamba kuna kundi la majambazi 11 wenye silaha ambao walikua katika kijiji cha Mubuga, vikosi vya usalama viliwaona na kuanza kupambana nao”, amesema mkuu wa mkoa wa Bururi, akihojiwa kwa njia ya simu na RFI.
“Jambazi mmoja ameuawa na wengine watano wamekamatwa”, Christian Nkurunziza ameongeza.
Jambazi au majambazi ni neno linalotumiwa mara kwa mara na serikali, ikimaanisha wapiganaji wa makundi ya waasi yaliyoanzishwa baada ya maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza.
Kwa mujibu wa shahidi ambaye hakutaka jina lake litajwe, “askari polisi mmoja na kijana kutoka kundi la vijana wa chama madarakani (ambao Umoja wa Mataifa unawaita wanamgambo) wamejeruhiwa”.
Mkuu wa mkoa wa Bururi amebaini kuhusu kijana huyo kutoka kundi la vijana wa chama tawala (Imbonerakure) kwamba “mtu aliyejeruhiwa ni raia wa kawaida ambaye alikua aliitikia wito wa serikali wa kushirikiana na vikosi vya usalama kwa kuwakamata majambazi hao.”
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mubuga wameyatoroka makazi yao na wengine wamesema kuwa na hofu ya kuwa huenda mapigano hayo yakachukua muda mrefu.
Mapigano hayo yanatokea wakati ambapo serikali ya Bujumbura imekua ikibaini kwamba tayari imerejesha hali ya utulivu nchini kote.
Hata hivyo hali ya usalama imeendelea kudorora katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, ambapo magruteni na mauaji ya kuvizia au visa vya ulipizaji kisasi vimekua vikiripotiwa.
Machafuko nchini Burundi yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 500, kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu na zaidi ya watu 270,000 kukimbilia nje ya nchi kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi, UNHCR.
Labels:
Ulinzi na Usalama
Location:
Burundi
Wednesday, 29 June 2016
Watatu wauawa na Polisi Tanga
Jeshi la Polisi mkoani Tanga limewahakikishia wananchi kwamba eneo la amboni lipo salama baada ya kuwakamata watuhumiwa watatu, Bunduki 2 aina ya SMG, bastola moja, risasi 30, mapanga na silaha nyingine katika msako maalum ulioshirikisha na vyombo vya ulinzi na usalama.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Leonard Paulo amesema silaha hizo zimepatikana zikiwa zimefukiwa ardhini ambapo watu waliokamatwa wanaaminika ndiyo waliohusika na mauaji ya watu 8 katika Mtaa wa kibatini.
Kamanda Paulo amesema watuhumiwa hao watatu wamefariki kutokana na majeraha waliyopata katika mapambano na vyombo vya usalama akiwemo kiongozi mkubwa wa kundi hilo ambaye ametambuliwa kwa jina la Abu Seif.
Aidha kamanda Paulo ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa taarifa mbalimbali zitakazowezesha kubaini wahalifu na kuwahakikishia wananchi kuwa eneo la amboni liko salama na limedhibitiwa.
Labels:
Ulinzi na Usalama
Location:
Tanga, Tanzania
Tundu Lissu kulala Mahabusu kwa kukosa dhamana, UKAWA hampo?
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana, mara baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kufuatia kauli yake aliyoitoa jana inayoelezwa kuwa si ya kiungwana.
Kukosa dhamana hiyo kunafuatia kwa Mbunge Lissu kuripoti katika kituo cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa na Jeshi hilo kuhusu kauli yake aliyoitoa jana baada ya kutoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mbunge huyo amehojiwa kwa saa tatu kuhusiana na maneno mengine ambayo anayodaiwa kuyaandika kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni ya uchochezi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekiri kuwa Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana na hataachiwa leo, hivyo atalala huko mpaka kesho.
Mbunge CHADEMA anyang'anywa tonge aliloweka mdomoni
Kesi iliyokuwa inaunguruma kuanzia tarehe 29.02.2016 katika Mahakama Kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii.
Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea Ubunge wa CCM, Jimbo la Longido, Dk. KIRUSWA alifikisha mahakamani shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya Mbunge wa Longido, Mhe. Onesmo Nangole.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mwagesi alisema kwamba mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili Dk. Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.
Katika shauri hilo, dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikuwa ni;
1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa Mhe. Onesmo Nangole.
2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mhe. Nangole.
3.Kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura.
4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.
5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo
Kutokana na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni, sheria na ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili, Jaji kutoka Mahakama Kuu Bukoba Mh. Jaji Mwagesi alisema;
“Kutokana na kuzingatia viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa sheria, Natamka kwamba;
Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa kujiridhisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki.”
Watu wasiopungua 40 wauawa Sudan Kusini
Serikali ya Sudan Kusini imetangaza kuwa watu wasiopungua 40 wameuawa katika mapigano yaliyotokea hivi karibuni katika mji wa Wau na kubaini kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka.
Tume ya umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, imeweka nyenzo maalum za usalama kuzunguka kambi yake iliyoko kwenye mji wa Wau, kufuatia kuzuka kwa mapigano kati ya wapiganaji wenye silaha na wanajeshi wa Serikali, SPLA.
Kwenye taarifa iliyotolewa na UNMISS, imesema kuwa inaendelea kutoa ulinzi kwa zaidi ya raia elfu 1, ambao wamenaswa kwenye mapigano yaliyoanza mwishoni mwa juma lilillopita.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa baada ya kufikiria kwa kina, iliamua kufungua milango yake siku ya Jumapili na kuruhusu mamia ya raia kuingia kwenye kambi yake, wakikimbia mapigano hayo.
Waziri wa Habari Michael Makuei, amesema kuwa maiti za raia 39 zimepatikana ikiwa ni pamoja na maiti nne za askari polisi.
Katika taarifa iliyotolewa na wakuu wa jimbo la Wau, baada ya kikao cha baraza la usalama la mji huo toka kulipozuka mapigano hayo Jumamosi ya wiki iliyopita, mkuu wa polisi kwenye mji huo, Chol Thuc amesema hali imeanza kurejea kama kawaida.
Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini alisema kuwa vikosi vyake vilipigana na makundi yaliyokuwa yamejihami pamoja na wale waliowataja kuwa wapiganaji wa makabila.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa mapigano kwenye mji huo, ambapo maelfu ya raia wameendelea kuyakimbia makazi yao kwa hofu ya kiusalama.
Mashirika hayo yanautaka umoja wa Mataifa kuingilia kati hali hiyo, kwa kuvisaidia vikosi vya Serikali kukabiliana na makundi ya wapiganaji wenye silaha ambao wameendelea kutekeleza mashambulizi ya kushtukiza kwenye maeneo mengi ya nchi.
UKAWA wamtaka JPM kutoa tamko uvunjifu wa Haki Zanzibar
Wabunge wa Ukawa wamemtaka Rais John Magufuli kutoa tamko juu ya uvunjifu wa haki za binadamu Zanzibar na kwamba, wana mpango wa kumpeleka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wakidai yanayotokea visiwani humo yana baraka zake.
Katika mkutano wao na wanahabari jana, wabunge hao wamemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kwenda Zanzibar kujionea hali halisi badala ya kupata taarifa kutoka kwa wasaidizi wake.
Hata hivyo, CCM imesema inalaani tamko hilo na kuwa kama Ukawa wanaona kuna masuala yanayohitaji kurekebishwa na kuhitaji hatua za haraka za Serikali watumie vyombo vinavyotambulika kisheria kama Bunge badala ya kuishia kulalamika vichochoroni.
Akitoa tamko la wabunge hao jana, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) alieleza kuwa hali ya kiusalama inazidi kuwa mbaya Pemba na Unguja baada ya uchaguzi wa marudio wa Machi 20 kutokana na baadhi ya wananchi kupigwa na vikosi alivyodai ni vya usalama.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Dodoma, Tanzania
JPM Mgeni Rasmi mechi ya wabunge wapenzi wa Simba na Yanga
Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mechi ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga inayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari bungeni mjini hapa jana Mwenyekiti wa Bunge Sports Klabu, William Ngeleja, alisema kuwa mechi hiyo inafanyika mahususi kwa ajili ya kuchangia madawati kwa ajili ya shule za msingi na sekondari nchini.
“Mechi hiyo ambayo huandaliwa na kuchezwa kila mwaka baada ya kumalizika kwa mkutano wa Bunge la Bajeti, awamu hii italenga kuisaidia serikali kuchangia madawati ili kusaidia tatizo la upungufu wa madawati lililopo nchini.”
Alisema, mechi hiyo itatanguliwa na michezo ya utangulizi ambayo ni mpira wa pete na kuvuta kamba, kipindi hiki imeandaliwa na Ofisi ya Bunge tofauti na miaka mingine, ambapo huwa inaandaliwa na wabunge wenyewe.
Ngeleja alifafanua kuwa, katika maandalizi hayo Bunge litashirikiana na wadau mbalimbali ambao wataombwa kuunga mkono kwa kuchangia madawati. Alisema, kutakuwa na kituo cha kukusanyia madawati hayo, ambacho kitakuwa ni hapa bungeni na yatakabidhiwa kwa Katibu wa Bunge, Thomas Kashililah.
“Sisi tunahitaji madawati, lakini mtu akiamua kutuchangia pesa pia tutashukuru hatutakataa tutazitumia kununulia madawati,” alisema.
Kufuatia maandalizi hayo, wameunda kamati ya maandalizi ambayo itazunguka kwa wadau kwa ajili ya kukusanya mchango huo wa madawati.
Alikitaja kikosi kinachoundwa na kamati hiyo ambayo itaongozwa na Mwenyekiti wa kamati ambaye ni Mbunge wa Ulyankulu, John Kadutu, wengine ni Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabibu.
Wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Busega, Rafael Chegeni, Mbunge wa Igunga, Dalay Kafumu, Mbunge wa Segerea, Bonna Kalua na Mbunge wa Morogoro Mjini, Mohamed Abood.
Ngeleja aliwataja wengine kuwa ni Mbunge Salim Hassan Turki, Mbunge wa Iringa na kocha wa timu ya soka ya Bunge Vanance Mwamoto, Mbunge wa Viti Maalumu Zainabu Vullu na makatibu wawili ambao ni watumishi wa Bunge.
Akijibu swali la kama kususa kwa wabunge wa upinzani kutaathiri mchezo huo, Njeleja alisema hakutaleta athari yoyote katika mechi hiyo, kwani wabunge waliopo ukijumlisha na wafanyakazi wanafikia mia sita, hivyo hawawezi kupwaya.
“Juzi tumecheza pale uwanjani, tulikuwa na mechi na Mtwara na Tabora na tuliwafunga, wachezaji tunao wa kutosha,” alisisitiza.
Aidha, Ngeleja alibainisha kuwa shindano hilo litahudhuriwa na wasanii mbalimbali kutoka ndani ya nchi ambao nao watatumbuiza lakini pia watakuwa na mechi ya utangulizi. Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo maalumu, Zungu, alisema madawati yatakayopatikana yatagawiwa nchi nzima.
“Tunawaomba, vyombo vya habari kuwasaidia kwani lengo letu ni zuri, jambo hilo lichukuliwe kwa uzito ili wadau wajitokeze kwa wingi,” alisema. Naye Mjumbe wa kamati hiyo aliwasihi waandishi wa habari, kupitia Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (Taswa), kushiriki katika kuchangia mchango huo wa madawati.
JPM azidi kumiminiwa pongezi
Siku chache baada ya uteuzi wa wakuu wa wilaya, Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania limeeleza kufurahishwa na namna Rais John Magufuli anavyozidi kujipambanua kwa Watanzania kuwa Rais wa Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa.
Katibu wa Jukwaa hilo, Mtela Mwampamba akizungumza Dar es Salaam jana alisema uteuzi wa wakuu wa wilaya umezingatia uadilifu, uwajibikaji, uzalendo na uwezo wa kiongozi husika katika kuwaunganisha wananchi.
“Jukwaa linatumia fursa hii kumpongeza Rais kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya alioufanya hivi karibuni. Rais amezidi kudhihirisha kuwa yeye ni kiongozi anayeishi na kusimamia kile anachoahidi kwa vitendo.
“Rais alisema na namnukuu; ‘Nimeona vijana ndio wachapakazi, wasiopenda rushwa na wazalendo, hivyo nitaendelea kuwaamini ndani ya serikali yangu kwa kuwateua kunisaidia kazi mbalimbali’, mwisho wa kunukuu.
“Hili amelitimiza na kulithibitisha katika uteuzi huu wa wakuu wa wilaya ambapo kwa zaidi ya asilimia 70 ya wateuliwa wote ni vijana. Sote tunajua vijana wana ari, utayari na shauku ya kuongoza kwa sifa ya kiuongozi ambazo ni uadilifu, ubunifu, uwajibikaji na uzalendo."
Alisema jukwaa hilo linatoa rai kwa Watanzania, viongozi wa dini na kisiasa kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli katika harakati za kuleta maendeleo.
Tuesday, 28 June 2016
KMKM yawazuia watetezi wa Haki za binadamu
Kikosi maalum cha kupambana na magendo, KMKM, kisiwani Pemba kimewazuia ndugu, jamaa na watetezi wa haki kukaribia mahakama ya Wete, Mkoa wa Kaskazini kwa kile walichodai ni maelekezo kutoka ngazi za juu.
Tukio hilo lilitokea wakati wananchi kadhaa wakishikiliwa kwa tuhuma za kujihusisha na uharibifu wa mashamba na mali mbalimbali za makada wa Chama cha Mapinduzi kisiwani Pemba.
Kutaka kufahamu zaidi kuhusu kinachoendelea Josephat Charo amezungumza na Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu wa chama cha Wananchi, CUF, Pemba, Mwinyi Juma.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Pemba, Zanzibar
Rais JPM hula chakula alichopika Mama Janette Magufuli
Baada ya kutambuliwa kama mtu mwenye msimamo mkali na asiyependa dhihaka, mabaye huwafuta watu hadharani, huenda sasa Rais wa Tanzania John Magufuli ana maadui wengi.
Sasa akiwa Ikulu na kama njia ya kuchukua tahadhari, inaripotiwa kuwa Magufuli hula chakula kilichopikwa na mke wake tu.
Kulingana na gazeti la Financial Times ni kwamba hili limedhihirika kutoka na upinzani anaokumbana nao.
Lakini hilo halijathibitishwa bado wala gazeti la Financial Times halijasema ni jinsi gani walipata uvumi huo.
Tume ya Uchaguzi yawasilisha Taarifa za Uchaguzi wa Zanzibar
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi –NEC Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema amefarijika kuona Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 umemalizika katika hali ya usalama na amani.
Jaji Lubuva amesema hayo kisiwani Zanzibar alipokuwa akikabidhi taarifa ya mwenendo wa uchaguzi kwa Spika wa Baraza la wawakilishi .
Akizungumzia suala la Katiba mpya iliyopendekezwa Jaji Lubuva amesema atahakikisha anasimamia sheria ambazo zimepitwa na wakati kwa lengo la kutetea haki za wananchi.
Naye Spika wa Baraza la wawakilishi Kisiwani Zanzibar Zubeir Ali Maulid amemshukuru Jaji Lubuva kwa kutembelea baraza hilo na kusema wakazi wa Zanzibar wanaendelea kuishi katika hali ya amani na usalama.
Mtihani umeongoza, halafu unafungwa jela. Kwa nini?
Mwanafunzi mmoja wa India amehukumiwa kifungo jela kwa kudanganya katika mtihani baada ya kujaribiwa kwa mara ya pili.
Ruby Rai mwenye umri wa miaka 17 ambaye alikuwa wa kwanza katika mtihani huo katika jimbo la Bihar, alisema katika mahojiano kwamba somo alipendalo la sayansi ya siasa linahusu mapishi.
Baada ya kanda hiyo kusambaa, bi Rai alilazimika kukalia tena mtihani na alikamatwa aliposhindwa huku matokeo yake ya mtihani wa awali yakifutiliwa mbali.
Alifikishwa mahakamani siku ya Jumapili ambapo hakimu alimuhukumu kifungo jela hadi tarehe 8 mwezi Julai.
Uamuzi wa kumpeleka jela umekosolewa kwa kuwa ni mtoto na kwamba badala yake angepelekwa katika jela ya watoto.
Gazeti la Hindu lilimnukuu afisa mkuu wa polisi Manu Maharaj akisema kuwa bi Rai atalazimika kubaini kwamba yeye ni mtoto.
Wakati huo huo agizo la kukamtwa limetolewa kwa wanafunzi wengine ambao walifanya vyema katika mtihani akiwemo Sauragh Shrestha ambaye alikuwa wa kwanza katika somo la sayansi lakini ambaye baadaye alishindwa kusema kwamba H20 ni maji.
Labels:
Taaluma
Location:
Bihar, India
Vituo vya mafuta Nchini Kenya vyanyang'wa leseni
Tume ya kudhibiti nishati nchini Kenya (ERC), imevipokonya leseni vituo vya mafuta kwa kuuza mafuta machafu.
Uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa mafuta ya diesel na petroli, yalikuwa yamechanyanywa na mafuta taa pamoja na bidhaa zingine.
Hata hivyo ni vituo vichache viliathiriwa kwa sababu asilimia 96.1 ya vituo vyote vilivyofanyiwa uchunguzi viligunduliwa kuwa na mafuta safi.
Tume hiyo ilianzisha mpango wa kuchunguza mafuta mwaka 2015 ili kuwawezesha wauza mafuta, kuhakikisha kuwa mafuta yao ni safi kabla ya kuyauza.
Labels:
Madini na Nishati
Location:
Nairobi, Kenya
Merkel aionya Uingereza kufuatia kujitenga kwake EU
Kiongozi Mkuu wa Ujerumani bi Angela Merkel ameionya Uingereza isitarajie kuendelea kupata faida ilizokuwa ikizipata katika Umoja wa Ulaya, hata baada ya kuamua kujitenga na Umoja huo.
Akizungumza katika mkutano maalum mjini Berlin kabla ya kwenda Brussels kushiriki katika mkutano wa wakuu wa Umoja wa Ulaya, Bi Merkel amesema ukijiondoa katika familia, huwezi kuendelea kunufaika bila kuwajibika.
Merkel amesisitiza kuwa hayatakuwepo mazungumzo yoyote na Uingereza, yawe rasmi au vinginevyo, kabla ya nchi hiyo kuwasilisha ombi la kujiondoa katika Umoja huo.
Bi Merkel amesema kujiondoa kwa Uingereza, maarufu kama Brexit, hakuwezi kuipotosha Ulaya katika kushughulikia changamoto kubwa zilizopo. Mkutano wa Brussels unajadili hatua ya Uingereza kuondoa uanachama wake katika Umoja wa Ulaya.
Helium yagunduliwa Tanzania
Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
Baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalum wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.
Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.
Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia.
Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.
Mnamo mwaka wa 2010 Mwanafizikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.
Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalam kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen.
''Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI'' alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford.
Labels:
Madini na Nishati
Location:
Tanzania
John Kerry asema bado wanaichunguza Uingereza
Kufuatia kura ya maoni ya Uingereza kujitoa ndani ya Jumuiya ya Ulaya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekari John Kerry amesema Marekani inaangalia mfumo wa ushirikiano na Uingereza kiuchumi.
Msimamo huo wa Marekani dhidi ya Uingereza,ni kufuatia kura ya maoni ijumaa wiki iliyopita, kujitoa katika jumuiya ya Ulaya. John Kerry ameyasema hayo katika mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond.
Hata hivyo waziri Hammond alitaka kujua kama Rais Obama ana mtazamo tofauti na kauli yake ya awali,kuhusiana na Uingereza ambapo awali alisema Uingereza itarudi mstari wa nyuma kibiashara iwapo itapiga kura kujitoa.Lakini Waziri Kerry akalitolea ufafanuzi hilo.
John Kerry anasema kilicho salia kwa Marekani ni kusubiri na kuona matokeo ya mazungumzo hayo na kuamua ni kwa mfumo gani uendeshaji wa mahusiano ya kibiashara utakuwa iwapo kutakuwa na mabadiliko ya kimfumo.
Akizungumzia kauli ya Rais Obama alisema Uingereza imekuwa na ushirikiano imara na Marekani kwa miaka mingi,na kuwa rais atafanya kila linalowezekana kusaidia kwa namna yoyote kuimarika kwa umoja uliopo na Uingereza na pia kusaidia jumuiya ya Ulaya kwa maslahi ya usalama wa dunia na ustawi wa dunia kwa ujumla.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Washington
Scotland yang'ang'ania kubaki EU
Waziri kiongozi wa Scotland amesema utawala wake utafanya kila linalowezekana kubakia katika Umoja wa Ulaya.
Nicola Sturgeon amesema jana kwamba hatua hizo ni pamoja na uwezekano wa kuzuwia hatua za kisheria zinazohusiana na kujitoa kwa Uingereza kutoka kundi hilo la mataifa.
Wapiga kura wa Scotland wameunga mkono kwa wingi mkubwa kubakia katika Umoja wa Ulaya. Sturgeon pia amesema kura ya pili ya maoni kuhusiana na uhuru wa Scotland kutoka Uingereza pia itajadiliwa.
Amedokeza kwamba kinachomuongoza katika suala hilo ni kulinda maslahi ya Scotland na hasisitizi kuhusu uhuru, lakini iwapo uhuru unakuwa ndio njia pekee ya kulinda maslahi ya Scotland basi itakuwa chaguo litakalojadiliwa.
Monday, 27 June 2016
Waziri Mkuu Majaliwa amwakilisha Rais John Magufuli mkutano wa SADC
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumatatu, Juni 27, 2016) kwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria mkutano maalum wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika kwa niaba ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika mkutano huo, Waziri Mkuu Majaliwa atahudhuria kikao maalum cha Wakuu wa Nchi na Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika) kitakachofanyika kesho (Jumanne, Juni 28, 2016).
Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Botswana, Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama ambaye pia ni Mwenyekiti wa SADC na utajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini Lesotho. Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu ambao unafanyika leo (Jumatatu, 27 Juni, 2016).
Januari 20, mwaka huu, mkutano wa SADC uliiagiza Serikali ya Lesotho iwe imetangaza matokeo ya Tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya kisiasa nchini humo ifikapo Februari Mosi, mwaka huu. Pia, SADC Double Troika iliitaka nchi hiyo iandae mchakato wa kueleza njia za utekelezaji wa mageuzi kama yalivyopendekezwa kwenye ripoti ya tume hiyo ifikapo Agosti, mwaka huu.
Mkutano huo ulikuwa umepokea taarifa ya Tume ya Usuluhishi ya SADC kwenye mgogoro wa Lesotho iliyoongozwa na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Dk. Cyril Ramaphosa ambayo iliainisha mambo kadhaa yakiwemo ya kikatiba na kiusalama ndani ya nchi hiyo.
SADC Double Troika ni kikao maalum cha Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Summit) na wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ on Politics, Defense and Security Cooperation).
SADC Double Troika ni mkutano unaohusisha viongozi wakuu watatu wanaoongoza chombo cha ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama na wengine watatu kutoka kwenye Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa SADC. Hawa wanawakilisha mwenyekiti aliyepo madarakani, mwenyekiti aliyemaliza muda wake na mwenyekiti ajaye ambaye huwa ni makamu mwenyekiti.
Chini ya muundo wa SADC, kuna mambo makuu mawili; la kwanza likiwa ni utangamano wa kikanda ambao unasimamiwa na mkutano wa wakuu wa nchi (SADC Summit) na la pili ni la siasa, ulinzi na usalama ambalo linasimamiwa na chombo maalum (SADC Organ)
Wajumbe wa mkutano wa SADC Organ ni Msumbiji (Mwenyekiti); Afrika Kusini (Mwenyekiti aliyemaliza muda wake) na Tanzania inayotarajia kuchukua uenyekiti wa chombo hiki ifikapo Agosti, 2016. Botswana, Zimbabwe na Swaziland ndizo zinaunda SADC Summit.
Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Dk. Aziz Mlima na maofisa wengine waandamizi.
Labels:
Kimataifa
Location:
Dar es Salaam, Tanzania
CHADEMA wawazuia viongozi wake kushiriki mikutano ya Serikali
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani kimesema kinatafakari hatua gani ya kuchukua baada ya Rais John Magufuli kutaka siasa za nguvu zifanywe wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao, kauli inayotafsiriwa kuwa ni kupiga marufuku shughuli za kisiasa.
Rais alitoa kauli hiyo mapema wiki iliyopita wakati akipokea taarifa ya Uchaguzi Mkuu kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kuisisitizia juzi wakati wa hafla ya kuzindua mpango wa polisi wa kuboresha huduma za usalama wa jamii.
Akizungumza jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam, katibu wa Chadema wa kanda hiyo, Casmir Mabina alisema wamefikia azimio la kupinga unyanyasaji na ukandamizaji kwa vyama vya siasa unaofanywa na Serikali ya Dk Magufuli.
Mabina alisema Rais Magufuli anavunja Katiba na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ambayo inaviruhusu vyama vya siasa kuendesha shughuli mbalimbali za kisiasa.
Alisema vyama haviwezi kukaa kimya mpaka mwaka 2020 wakati kazi yao ni kukutana na wananchi.
“Tunamshauri Rais Magufuli aache kutawala nchi kwa woga na ubabe … afuate misingi ya Katiba na sheria, na kuwaongoza Watanzania badala ya kuwatawala,” alisema Mabina.
Mabina aliongeza kuwa Jeshi la Polisi liache kutumiwa na Serikali kufinyanga sheria za nchi na kukandamiza upinzani kwa kutumia vibaya Sheria ya Jeshi la Polisi, kifungu cha 43 (3) kwa kusingizia habari za ‘kiintelijensia’ na ‘hali ya uvunjifu wa amani’.
Mwenyekiti wa Chadema wa Kanda ya Dar es Salaam Kuu, Mwita Waitara alilalamikia kitendo cha mameya wa Dar es Salaam kunyimwa vibali vya kwenda nje ya nchi kutafuta fedha ili kusaidia maendeleo ya halmashauri zao.
Alisema fedha za safari hizo zinatolewa na washirika wa maendeleo, lakini Serikali imekuwa ikizuia safari hizo kwa kisingizio cha kubana matumizi.
Alisema safari nyingine za nje ni muhimu kwa sababu zinawawezesha mameya kukutana na wadau wa maendeleo ili kupata misaada.
“Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alikuwa na safari ya kwenda Afrika Kusini kukutana na mameya wengine duniani, lakini alizuiliwa kwa maelekezo.
“Hatuwezi kuendelea kama tutashindwa kukaa na wenzetu ili kujifunza mambo ya maendeleo,” alisema.
Mwita alidai kuwa huo ni mpango wa Serikali kudhoofidha halmashauri zinazoongozwa na upinzani ili wasiweze kufanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kufanywa na CCM.
Alisema yeye pia alizuiliwa kwenda Marekani akiwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii.
Ushauri mwingine ulitolewa na mwenyekiti wa Kanda ya Ilala, Dk Makongoro Mahanga ambaye alimtaka Rais kufuata Katiba kwa sababu aliapa kuilinda na kuitetea kwa masilahi ya Taifa.
Dk Mahanga alimtaka Rais akumbuke ahadi mbili alizozitoa wakati wa kampeni na wakati anaapishwa, ambazo ni kuilinda Katiba na kuwaletea wananchi maendeleo.
“Kinachowaogopesha CCM ni upinzani kupata kura zaidi ya milioni sita wakati wa uchaguzi. Wanajua kwamba wanaweza kuchukua nchi, ndiyo maana wameanza kudhibiti vyama vya siasa ili visiwe na nguvu,” alisema Dk Makongoro ambaye aliwahi kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.
Rais alitoa kauli hiyo mapema wiki iliyopita wakati akipokea taarifa ya Uchaguzi Mkuu kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kuisisitizia juzi wakati wa hafla ya kuzindua mpango wa polisi wa kuboresha huduma za usalama wa jamii.
Akizungumza jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam, katibu wa Chadema wa kanda hiyo, Casmir Mabina alisema wamefikia azimio la kupinga unyanyasaji na ukandamizaji kwa vyama vya siasa unaofanywa na Serikali ya Dk Magufuli.
Mabina alisema Rais Magufuli anavunja Katiba na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ambayo inaviruhusu vyama vya siasa kuendesha shughuli mbalimbali za kisiasa.
Alisema vyama haviwezi kukaa kimya mpaka mwaka 2020 wakati kazi yao ni kukutana na wananchi.
“Tunamshauri Rais Magufuli aache kutawala nchi kwa woga na ubabe … afuate misingi ya Katiba na sheria, na kuwaongoza Watanzania badala ya kuwatawala,” alisema Mabina.
Mabina aliongeza kuwa Jeshi la Polisi liache kutumiwa na Serikali kufinyanga sheria za nchi na kukandamiza upinzani kwa kutumia vibaya Sheria ya Jeshi la Polisi, kifungu cha 43 (3) kwa kusingizia habari za ‘kiintelijensia’ na ‘hali ya uvunjifu wa amani’.
Mwenyekiti wa Chadema wa Kanda ya Dar es Salaam Kuu, Mwita Waitara alilalamikia kitendo cha mameya wa Dar es Salaam kunyimwa vibali vya kwenda nje ya nchi kutafuta fedha ili kusaidia maendeleo ya halmashauri zao.
Alisema fedha za safari hizo zinatolewa na washirika wa maendeleo, lakini Serikali imekuwa ikizuia safari hizo kwa kisingizio cha kubana matumizi.
Alisema safari nyingine za nje ni muhimu kwa sababu zinawawezesha mameya kukutana na wadau wa maendeleo ili kupata misaada.
“Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alikuwa na safari ya kwenda Afrika Kusini kukutana na mameya wengine duniani, lakini alizuiliwa kwa maelekezo.
“Hatuwezi kuendelea kama tutashindwa kukaa na wenzetu ili kujifunza mambo ya maendeleo,” alisema.
Mwita alidai kuwa huo ni mpango wa Serikali kudhoofidha halmashauri zinazoongozwa na upinzani ili wasiweze kufanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kufanywa na CCM.
Alisema yeye pia alizuiliwa kwenda Marekani akiwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii.
Ushauri mwingine ulitolewa na mwenyekiti wa Kanda ya Ilala, Dk Makongoro Mahanga ambaye alimtaka Rais kufuata Katiba kwa sababu aliapa kuilinda na kuitetea kwa masilahi ya Taifa.
Dk Mahanga alimtaka Rais akumbuke ahadi mbili alizozitoa wakati wa kampeni na wakati anaapishwa, ambazo ni kuilinda Katiba na kuwaletea wananchi maendeleo.
“Kinachowaogopesha CCM ni upinzani kupata kura zaidi ya milioni sita wakati wa uchaguzi. Wanajua kwamba wanaweza kuchukua nchi, ndiyo maana wameanza kudhibiti vyama vya siasa ili visiwe na nguvu,” alisema Dk Makongoro ambaye aliwahi kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Pwani, Tanzania
Mtoto ashambuliwa na fisi Afrika Kusini
Maafisa wa mbuga ya wanyamapori nchini Afrika Kusini wamewashauri wageni kuwa makini, baada ya fisi kumshambulia mtoto wa umri wa miaka 15 alipokuwa amelala ndani ya hema katika mbuga ya Kruger.
Msemaji wa mbuga za wanyamapori William Mabasa, aliwashauri wageni kuchukua tahadhari kila wakati, kwa kuwa kuna wanyamapori wanaowazunguka, na kuwataka wahakikishe kuwa hema zao zimefungwa vizuri.
Mtoto huo alifanyiwa upasuaji ili kupata matibu kwenye mdomo, kutokana na majeraha aliyoyapata kufuatia shambulizi hilo.
Labels:
Matukio
Location:
South Africa
Messi astaafu akina na rekodi mbaya mwishoni
Katika hatua iliyoonekana kuwashanga wapenzi wa soka nchini Argentina na dunia kwa ujumla, mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa.
Uamuzi wa Messi kustaafu kucheza soka la kimataifa, umewachukua watu kwa mshtuko, hasa ikiwa ni baada ya timu yake ya taifa kushindwa kutwaa taji la michuano ya Copa Amerika.
Mchezaji huyo na timu yake ya taifa kwa mara nyingine walishindwa kufua dafu katika ngazi ya kimataifa, ikiwa ni mara ya nne mfululizo kwa mchezaji huyu akiwa na timu yake ya taifa kushindwa kutwaa taji lolote kubwa baada ya hapo jana timu ya taifa ya Chile kuchomoza na ushindi kwa njia ya penati.
"Kwangu mimi, timu ya taifa nimemaliza," alisema Lionel Messi wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi na Chile.
"Nimefanya kila nilichoweza, nimeshiriki fainali nne, inauma kushindwa kuwa bingwa, ni wakati mgumu kwangu na timu nzima pia, na ni ngumu kusema, lakini nimemalizana na timu ya taifa ya Argentina." alisema Messi.
Uamuzi huu wa kushanga wa Lionel Messi umekuja baada ya kushindwa kwenye fainali ya tatu mfululizo akiwa na timu ya taifa, toka kwenye fainali za kombe la dunia nchini Brazil.
Argentina ilifungwa bao 1-0 na Ujerumani kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka 2014 na kushindwa kwenye hatua ya penati na Chile kwenye fainali ya kombe la Copa Amerika.
Messi pia alishuhudia timu yake ikipoteza kwenye mchezo wa fainali mwaka 2007 ya kombe la Copa Amerika.
Licha ya kutokuwa na mafanikio na timu yake ya taifa, Messi hajapungukiwa kupata mafanikio akiwa na klabu yake ya Barcelona, ambapo ameshinda taji la mchezaji bora wa dunia kwa mara 5.
Licha ya mafanikio haya Messi amekuwa akikosolewa pakubwa na mashabiki wa soka nchini mwake kutokana na kushindwa kuisadia timu yake ya taifa kutwaa mataji muhimu.
Kushindwa kwa Leonel Messi kufikia japo nusu ya rekodi ya mchezaji mkongwe na maarufu nchini humo, Diego Maradona, ambaye bao lake la mkono liliipa taji ya dunia timu yake mwaka 1986, amekuwa akimkosoa mara kadhaa.
Maradona mwenyewe amekuwa akimkosoa Messi kwa kushindwa kuonesha umahiri akiwa na timu ya taifa ukilinganisha na akiwa na timu yake ya Barcelona.
Uamuzi wa Messi kustaafu kucheza soka la kimataifa, umewachukua watu kwa mshtuko, hasa ikiwa ni baada ya timu yake ya taifa kushindwa kutwaa taji la michuano ya Copa Amerika.
Mchezaji huyo na timu yake ya taifa kwa mara nyingine walishindwa kufua dafu katika ngazi ya kimataifa, ikiwa ni mara ya nne mfululizo kwa mchezaji huyu akiwa na timu yake ya taifa kushindwa kutwaa taji lolote kubwa baada ya hapo jana timu ya taifa ya Chile kuchomoza na ushindi kwa njia ya penati.
"Kwangu mimi, timu ya taifa nimemaliza," alisema Lionel Messi wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi na Chile.
"Nimefanya kila nilichoweza, nimeshiriki fainali nne, inauma kushindwa kuwa bingwa, ni wakati mgumu kwangu na timu nzima pia, na ni ngumu kusema, lakini nimemalizana na timu ya taifa ya Argentina." alisema Messi.
Uamuzi huu wa kushanga wa Lionel Messi umekuja baada ya kushindwa kwenye fainali ya tatu mfululizo akiwa na timu ya taifa, toka kwenye fainali za kombe la dunia nchini Brazil.
Argentina ilifungwa bao 1-0 na Ujerumani kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka 2014 na kushindwa kwenye hatua ya penati na Chile kwenye fainali ya kombe la Copa Amerika.
Messi pia alishuhudia timu yake ikipoteza kwenye mchezo wa fainali mwaka 2007 ya kombe la Copa Amerika.
Licha ya kutokuwa na mafanikio na timu yake ya taifa, Messi hajapungukiwa kupata mafanikio akiwa na klabu yake ya Barcelona, ambapo ameshinda taji la mchezaji bora wa dunia kwa mara 5.
Licha ya mafanikio haya Messi amekuwa akikosolewa pakubwa na mashabiki wa soka nchini mwake kutokana na kushindwa kuisadia timu yake ya taifa kutwaa mataji muhimu.
Kushindwa kwa Leonel Messi kufikia japo nusu ya rekodi ya mchezaji mkongwe na maarufu nchini humo, Diego Maradona, ambaye bao lake la mkono liliipa taji ya dunia timu yake mwaka 1986, amekuwa akimkosoa mara kadhaa.
Maradona mwenyewe amekuwa akimkosoa Messi kwa kushindwa kuonesha umahiri akiwa na timu ya taifa ukilinganisha na akiwa na timu yake ya Barcelona.
Jacob Zuma aamriwa kurudisha pesa alizochota
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameambiwa kuwa ni lazima alipe zaid ya dola nusu milioni pesa za umma, ambazo alitumia kukarabati nyumba yake.
Mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini imetaka wizara ya fedha, kutambua ikiwa ni kiasi gasi Rais Zuma anastahili kurejesha kufutia uamuzi wa mapema mwaka huu kuwa alikuwa amekiuka katiba ya Nchi.
Uturuki yakasirika kufuatia matamshi ya Papa Francis
Vatican imetoa majibu ya madai ya Uturuki kwamba kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameonyesha "mawazo ya vita vya msalaba" baada ya kutamka mauaji ya waarmenia yaliyofanywa Ottoman kama "mauaji ya kimbari."
Papa Francis amezidisha hasira za waturuki katika ziara yake ya siku tatu katika jimbo la zamani la muungano wa kisovieti la Armenia na kutumia neno hilo kwa mauaji ya siku nyingi ambayo Uturuki inayakanusha kuwa yalikuwa ya kimbari.
Naibu waziri mkuu wa Uturuki Nurettin Canlikli ameyaita matamshi ya Papa kama "bahati mbaya" na kwamba yanaonyesha ishara ya "mawazo ya vita vya msalaba ."
Vatican imekataa madai hayo ikisema kiongozi huyo alikuwa akijaribu kuweka "daraja na sio ukuta" na kwamba hana nia mbaya na Uturuki.
Uturuki ambayo ni nchi ya Kiislamu inakubali kwamba Wakristo wengi wa Armenia waliuwawa katika mapigano yaliyoanza mwaka 1915 lakini inakanusha kwamba mamia kwa maelfu ya watu waliuwawa katika mapigano hayo kustahiki kuitwa mauaji ya kimbari.
Papa Francis amezidisha hasira za waturuki katika ziara yake ya siku tatu katika jimbo la zamani la muungano wa kisovieti la Armenia na kutumia neno hilo kwa mauaji ya siku nyingi ambayo Uturuki inayakanusha kuwa yalikuwa ya kimbari.
Naibu waziri mkuu wa Uturuki Nurettin Canlikli ameyaita matamshi ya Papa kama "bahati mbaya" na kwamba yanaonyesha ishara ya "mawazo ya vita vya msalaba ."
Vatican imekataa madai hayo ikisema kiongozi huyo alikuwa akijaribu kuweka "daraja na sio ukuta" na kwamba hana nia mbaya na Uturuki.
Uturuki ambayo ni nchi ya Kiislamu inakubali kwamba Wakristo wengi wa Armenia waliuwawa katika mapigano yaliyoanza mwaka 1915 lakini inakanusha kwamba mamia kwa maelfu ya watu waliuwawa katika mapigano hayo kustahiki kuitwa mauaji ya kimbari.
Madiwani Jijini Mwanza wabuni mpango lukuki wa maendeleo
Madiwani Jijini Mwanza na Manispaa ya Ilemela wamepitisha Mpango Kabambe wa Jiji la Mwanza.
Mpango huo utahakikisha jiji na manispaa, zimepangwa kisasa kuondoa migogoro na kuongeza kasi ya ukuaji wa kiuchumi.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa wadau wa mpango huo hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema kuwa rasimu ya mpango huo, inahusisha mikakati na mapendekezo kutoka sekta tatu za maendeleo ya mji ambazo ni matumizi ya ardhi, usafirishaji na miundombinu.
“Huu ni mkutano wa sita wa mapendekezo ya rasimu ya mpango kabambe wa jiji la Mwanza na wa mwisho ili kuwa na mpango kamili utakaotumika katika jiji la Mwanza kama sheria,” alisema Mongela.
Mongela alisema mpango huo wa kina wa matumizi ya ardhi, utatumiwa kama kichocheo cha kujumuisha ardhi inayohitajika kwa mapendekezo ya maendeleo mbalimbali katika sekta za usafirishaji na miundombinu.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Mwanza, Tanzania
Benki ya NMB yatoa Mil. 143 Polisi kuimarisha Ulinzi
Benki ya NMB Tanzania imetoa TSh. Mil. 143 katika kuhakikisha usalama wa raia na Mali zaoi unaimarika. Benki hiyo imeunga mkono jitihada za serikali za kuboresha huduma za ulinzi na usalama zinazofanywa na Polisi.
Hivi karibuni, Rais John Magufuli alizindua mpango wa kuboresha Usalama wa Jamii katika viwanja vya Biafra, Dar es Salaam, ambapo pia alizindua moja ya vituo vipya vya Polisi vinavyohamishika vilivyotolewa na Benki ya NMB.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Waziri Barnabas alisema Polisi ipo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa raia na mali zao, hivyo kama benki wameona ipo haja kuunga mkono jitihada hizo za kuboresha ulinzi.
“Ushirikiano tunaojivunia leo unatokana na NMB kuunga mkono ujenzi wa vituo viwili vya polisi vinavyohamishika na kugharamia shughuli hii ya uzinduzi kwa kiasi cha Sh milioni 143 ikiwa ni sehemu ya maboresho makubwa na mabadiliko katika Jeshi la Polisi,” alisema Barnabas.
Aidha, katika hatua nyingine Barnabas alisema Sh bil 28 zimetolewa na kwamba, zaidi ya maofisa wa Polisi 10,000 wanaendelea kunufaika na mikopo ya benki hiyo kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao ya kifedha.
Labels:
Ulinzi na Usalama
Location:
Tanzania
Magufuli afanyiwa maombi maalum Mkoani Shinyanga
Jana Jumapili Juni 26,2016 kulifanyika Maombi Maalum katika Kanisa la The International Evangelical Assemblies of God-Tanzania (IEAGT) lililopo kata ya Kambarage Mkoani Shinyanga kwa ajili ya taifa la Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa rais, bunge, mahakama, polisi na viongozi mbalimbali wa serikali.
Maombi hayo yaliongozwa na Askofu wa kanisla la (IEAGT) David Elias Mabushi na kuhudhuriwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga.
Maombi hayo pia yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, mashirika, waandishi wa habari, wageni mbalimbali na waumini wa kanisa hilo.
Pamoja na maombi hayo maalumu, Kanisa hilo limeadhimisha siku ya watoto katika kanisa hilo ambapo pia Juni 26 ni siku ya kuzaliwa kwa askofu wa kanisa la IEAGT David Mabushi ambaye leo ametimiza umri wa miaka 53.
Sambamba na matukio hayo mawili makubwa, kanisa hilo pia lilikabidhi madawati 20 kwa uongozi wa wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kumuunga mkono rais Magufuli katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa changamoto ya madawati inamalizika katika shule.
Awali akisoma risala,Katibu wa kanisa la IEAGT, Mchungaji Obed Jilala alisema baada ya uchaguzi mkuu 2015,kanisa la IEAGT limekuwa likisikia kwa nyakati tofauti rais Magufuli akiomba maombi kwa ajili ya kazi yake ya kuliongoza taifa, hivyo kanisa lao limeguswa sana na kauli hiyo na katika kuonesha wanamuunga mkono walikubaliana siku ya Jumapili Juni 26,2016 iwe ya maombi maalum kwa ajili ya kiongozi wa taifa sambamba na kuliombea nchi ya Tanzania.
"Maombi haya yamebebwa kwa kiasi kikubwa na upendo tulio nao kwa nchi yetu ,kanisa la IEAGT kama sehemu ya jamii ya watanzania tumeona siku ya leo iwe kilele cha maombi ya kitaifa katika mkoa wetu na mahali popote lilipo kanisa letu",aliongeza Mchungaji Jilala.
Naye Askofu wa kanisa hilo David Mabushi akitoa mahubiri yake, mbali na kumpongeza rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa rais, alimuomba kuendelea kuonesha msimamo wake katika kuwaletea maendeleo watanzania huku akimfananisha na Nabii Musa akisema Magufuli amekuja kuiokomboa nchi na kuifanya kuwa nchi ya asali na maziwa.
"Tumeandaa siku hii muhimu kwa ajili ya kuiombea nchi yetu ili iendelee kuwa na amani, tunamuombea rais wetu kwa sababu wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi. Sisi kama kanisa tutahakikisha tunamuunga mkono rais Magufuli kwa maneno na vitendo ndiyo maana leo tunatoa sadaka ya madawati 20, tunaomba watanzania waendelee kumuombea rais wetu aliyeonesha kuwajali watanzania tangu alipoingia madarakani amekuwa mstari wa mbele kupigana dhidi ya rushwa na vitendo vyote viovu", aliongeza Askofu Mabushi.
Kwa upande wake mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Josephine Matiro ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, alilipongeza kanisa hilo kuona umuhimu wa kuombea viongozi wa nchi na kuongeza kuwa kanisa la IEAGT ni kanisa la kwanza mkoani Shinyanga kufanya maombi kwa ajili ya viongozi wa nchi.
"Ndugu zangu watanzania naomba tuendelee kuiombea nchi ili iendelee kuwa ya amani na viongozi kuwa na hofu ya Mungu, lakini pia naomba watanzania wafanye kazi, sasa ni muda wa kuchapa kazi tuache siasa za majukwaani, tumuunge mkono Mheshimiwa Rais katika kutekeleza kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu", aliongeza Matiro.
Miongoni mwa mambo yaliyoombewa katika ibada hiyo ni kuombea taifa, kumuombea rais Magufuli, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na viongozi wengine wa serikali, kuombea bunge na madiwani, mahakama na katika maeneo yote viongozi wa dini waliwataka viongozi hao kuwa hofu ya Mungu na kuchukia rushwa pamoja na kutumia nguvu zao kupambana na vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji ya watu kwenye nyumba za ibada, vikongwe, albino na watu mbalimbali wasio na hatia.
Labels:
Habari njema
Location:
Shinyanga, Tanzania
UKAWA mtasusia vikao vya Bunge hadi lini?
Wabunge wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wameendelea kususia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson.
Jana, wabunge hao walitoka kwa muda katika Ukumbi wa Pius Msekwa wakati Naibu Spika huyo alipokuwa akifungua semina kuhusu ubia kati ya sekta binafsi na umma (PPP) na walirejea muda mfupi baada ya kumaliza kusoma hotuba yake na kumwachia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Josephat Kandege kuongoza.
Hata hivyo, waliporejea walikaa upande mmoja wa ukumbi huo wakijitenga na wabunge wa CCM na baada ya kumaliza semina hiyo, wabunge hao walionekana wakikwepa kusalimiana na wenzao wa CCM.
Akizungumzia kitendo hicho, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia alisema, “Wabunge wote wa Ukawa huwa tunaenda katika kamati, hilo hatujalikataa, tuliyokataa ni mambo ya michezo, ya kushiriki katika kantini, kusalimiana na vikao vyote vinavyoendeshwa na Dk Tulia."
Lakini hii toka bungeni rudi bungeni imeanza kuashiria nini kwa Wawakilishi wetuu hawa? Jibui huenda likawa ni kwamba huenda wameanza maandalizi ya kutengeneza mbinu ya kurejea mjengoni sasa.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Dodoma, Tanzania
Sunday, 26 June 2016
Thelathini wafa kwa ajali China
Watu 30 wamefariki dunia katikati mwa China katika ajali ya basi moja lililoungua moto kufuatia kuanguka pembeni mwa barabara.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari abiria 56 walikuwamo ndani ya basi hilo ambapo majeruhi 21 walikimbizwa hospital kwa matibabu zaidi.
Katika video iliyoonyeshwa na shirika la utangazaji la CCTV, kulionekana moshi mweusi na mzito kutoka katika basi ambapo mamlaka za mji zinasema ajali hyo huenda imesababishwa na kuvuja kwa mafuta baada ya basi hilo kuanguka pembeni mwa barabara.
China inakabiliwa na kiwango kikubwa cha ajali za barabarani ambapo inakadiriwa kuwa watu 250,000 hufariki kila mwaka kutokana na ajali.
Mawaziri wa Chama cha Labour kujiuzulu
Hali ya wasiwasi iliyoanzishwa na upigaji kura wa Uingereza kuondoka Jumuiya ya Ulaya (EU) imekumba chama kikubwa cha upinzani cha Labour.
Nusu ya Baraza la Mawaziri la upinzani linatarajiwa kujiuzulu hii leo likilalamikia jinsi kiongozi wao Jeremy Corbyn alivyoongoza kampeni ya kura za maoni.
Wa kwanza kuondoka alikuwa Waziri wa Afya, Heidi Alexander, aliyesema kuwa Bwana Corbyn hana kipaji cha kushughulikia matatizo yanayokumba Uingereza kwa wakati huu.
Awali, Waziri wa upinzani wa Mashauri ya Kigeni, Hilary Benn, aliachishwa kazi kwa kile Bwana Corbyn alidai kuwachochea wenzake waondoke katika baraza hilo iwapo Bwana Corbyn, atakataa kuheshimu mswada wa kutokuwa na imani kwake.
Wafuasi wengi wa Leba walipiga kura kwa Uingereza kujiondoa katika Jumuiya ya Ulaya.
Michael Gove kuunga mkono Boris Johnson
Waziri wa sheria nchini Uingereza Michael Gove ameweka wazi kuwa atamuunga mkono mwanaharakati kinara wa kambi ya kujiondoa kwenye umoja wa Ulaya Boris Johnson katika jitihada za kuwa waziri mkuu wa Uingereza kuchukua nafasi ya David Cameron aliyetangaza kujiuzulu nafasi hiyo ifikapo mwezi Oktoba kufuatia nchi hiyo kuamua kujiondoa kwenye muungano wa Ulaya.
Hapo jana Gove alimpigia simu Boris ambaye ni meya wa zamani wa jijini la London na kumwambia kuwa atasimama naye na kuunda nguvu ya pamoja kwa ajili ya manufaa ya nchi.
Kwa upande mwingine washirika wa karibu wa waziri wa mambo ya ndani Theresa May, jana usiku walikuwa wakiwaomba wabunge kumuunga mkono May ambaye anaonekana kuwa mpinzani mkuu wa Boris na anatarajia kuingia katika kinyang’anyiro hicho mwishoni mwa juma.
Haya yanajiri wakati mataifa yaliyoasisi muungano wa Ulaya EU, yanaitaka Uingereza kuanza kuondoka katika muungano huo haraka iwezekanavyo ili kuiondoa jumuiya hiyo katika mkwamo, waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani amesema jana Jumamosi.
Frank- Walter Steinmeier akiongoza mkutano wa mataifa sita yaliyo asisi Muungano wa Ulaya jijini Berlin, amesema wako katika makubaliano kwamba Uingereza haitakiwi kusubiri utaratibu mgumu wa kujiondoa katika muungano huo.
Tanzia: Antony Gervase Mbassa (Mb.) afariki
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi Mkoani Kagera kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amefariki Usiku wa kuamkia Leo.
Dk. Anthony Gervase Mbassa (Chadema) amefariki Usiku wa Kuamkia leo Jumapili Juni 26, 2016. Chanzo hakijajulikana kwani amepatwa na umauti ghafla.
Labels:
Tanzia
Location:
Biharamulo, Tanzania
Rais John Magufuli afurahia Sheria ya Ufisadi kupitishwa
RAIS John Magufuli Jana aliapa kuwanyoosha mkono wale wanaotafuna fedha za wananchi badala ya kuzielekeza katika maendeleo.
Pia alieleza furaha yake baada ya Bunge la Jamhuri kupitisha sheria ya kuwabana mafisadi akidai kuwa, sasa atawanyoosha.
Rais Magufuli alitoa kauli hiyo Jana wakati akihutubia katika uzinduzi wa Mpango wa Usalama wa Jamii uliofanyika katika viwanja vya Biafra, jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa, ni lazima serikali iende mbele kwa yale iliyoyaahidi sambamba na kushukuru kupitisha muswada wa kushughulikia mafisadi.
“Ninapenda kulishukuru sana Bunge kwa kupitisha muswada huo wa kushughulikia mafisadi, ili mafisadi wanyooke kweli kweli.
“Tanzania tunahela nyingi lakini watu wanakula kweli kweli lakini hawashibi, ila tufikie mahali tuwalazimeshe washibe kwa nguvu kwa hizi hatua tutakazochukua,” alisema.
Pia aliiagiza Taasisi ya ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi wa mkataba wa ujenzi wa barabara zilizopo katika Manispaa ya Kinondoni zinazoonekana kujenjwa chini ya kiwango.
“…pamoja na injinia aliyesimamia huo mradi, ninafahamu aliyekuwa injinia wa jiji hili nafikiri ni Kinondoni tulisimamisha kazi, na vyombo vya PCCB vianze kuchunguza.
“Hivi ni vitu vya kuweza kushughulikiwa, wananchi wamechoka fedha zao kuwa zinatumiwa na watu wachache, ifike mahali watu waliokuwa na mazoea ya kula mali za umma waanze kuogopa wakale mali za bibi zao kule,”alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli alitoa agizo hilo baada ya Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kushitaki kwamba, wananchi wa mkoa huo wamechoka kujengewa barabara zisizo za viwango.
“Wananchi wamechoka kujengewa barabara zilizochini ya kiwango, imekuwa kilio cha muda mrefu, pesa nyingi zinatumika kujengea barabara na matokeo yake barabara zinakuwa mbovu na kila mwaka zinajengwa barabara zile zile wakati wananchi wanatamani barabara zenye viwango vya rami,” alisema na kuongeza,
“Nikiwaambia tu hapa mbele yako ipo barabara iliyojengwa na haijamaliza hata mwaka mmoja ambayo inatokea Ubalozi wa Ufaransa inakuja hapa tulipo Biafra inaenda mpaka Mwanaymala, hii ingesaidia kupunguza foleni imeshaanza kuharibika na ni mbovu.”
Makonda alisema, mkataba uliokuwepo kwenye Manispaa ya Kinondoni unaeleza kuwa, ilitakiwa mkandarasi alipwe Sh. 500 milioni na kwamba, aliongezewa Sh. 400 milioni kinyume na taratibu pia alijenga barabara chini ya kiwango.
“Na ajabu kwa mkataba huu uliopo wa Manispaa ya Kinondoni ambapo walimlipa milioni 500 na kuongezewa milioni 400.
“Nimemuagiza mkurugenzi na mkuu wa wilaya kuhakikisha anajenga barabara kwa gharama zake na zile pesa zilizotolewa kinyume na taratibu zirudishwe.
“Jana mimi na wakuu wa wilaya tuliamua kusitisha kampuni nne zisipewe leseni katika mkoa wetu mpaka watakapothibitisha wana uwezo wa kujenga barabara zenye ubora,” alisema.
Alisema, mkandarasi yeyote atakayejenga barabara isiyo na kiwango kwenye Mkoa wa Dar es Salaam, hatapata tenda tena.
Rais Magufuli aja na mbinu mpya kisiasa
Rais John Magufuli, jana alitoa staili mpya ya kuwaalika wanasiasa kuanza kuzungumza kabla yake.
Hiyo ilitokea jana wilayani Kinondoni alikokwenda kwa ajili ya uzinduzi wa Mpango wa Jeshi la Polisi wa kuboresha usalama wa jamii.
Mh. Magufuli ambaye alifika uwanjani hapo saa 4:43 asubuhi, kabla ya kuanza kuzungumza aliwaalika wanasiasa mbalimbali kusema chochote kwa maelezo kuwa suala la ulinzi na usalama si la vyama.
Walioitwa ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni (Chadema), Boniface Jacob ambaye hakuwapo katika eneo hilo na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa.
Wengine ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na Diwani wa Kata ya Kinondoni (Chadema), Mustafa Muro.
“Mstahiki Meya wa Kinondoni yuko wapi? Hayupo, sasa Jacob yeye ujambazi anautaka tu,” alihoji Rais Magufuli.
Hata hivyo, Meya Jacob baadaye alilieleza gazeti la Mwananchi kuwa hakualikwa na badala yake alitakiwa kuteua madiwani watano kutoka Kamati ya Fedha kuhudhuria hafla hiyo na kusisitiza kwamba haungi mkono ujambazi na uhalifu.
Akisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha anatekeleza ahadi zake, Rais Magufuli amesema lengo lake ni kutowaangusha wananchi na amedhamiria kuijenga nchi kwa nguvu zote huku akirejea kauli yake ya kuwataka wananchi wamuombee.
“Nawaomba wananchi mniache nitekeleze ahadi zangu kwa Watanzania wote. Yapo aliyoahidi diwani wa Chadema aachwe ayatekeleze. Watu wa CCM wasimsumbue,” alisema.
Washukiwa wawili wa Ugaidi nchini Ubelgiji washtakiwa na Polisi
Waendesha mashtaka nchini Ubelgiji waliwashtaki wanaume wawili kwa makosa ya ugaidi hapo jana, baada ya operesheni kadhaa za msako wa usiku.
Maafisa wamesema hakuna silaha, miripuko au vifaa vyovyote vilivyogunduliwa, lakini wanaume hao wanatuhumiwa kwa kushirikiana na kundi la kigaidi.
Wiki iliyopita maafisa wa Ubelgiji waliwashtaki wanaume watatu kwa makosa ya jaribio la mauaji ya kigaidi. Operesheni kubwa za kupambana na ugaidi zilihusishwa na kuripotiwa kwa kitisho dhidi ya mashabiki wakati wa mechi za michuano ya Euro 2016.
Ubelgiji inaendelea kuwa katika tahadhari ya hali ya juu baada ya mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Kiislamu mwezi Machi.
Waripuaji wa kujitoa mhanga waliwauwa watu 32 katika mashambulizi yaliyoratibiwa dhidi ya uwanja mkuu wa ndege wa Brussels na njia za treni za chini ya ardhi.
Maafisa wamesema hakuna silaha, miripuko au vifaa vyovyote vilivyogunduliwa, lakini wanaume hao wanatuhumiwa kwa kushirikiana na kundi la kigaidi.
Wiki iliyopita maafisa wa Ubelgiji waliwashtaki wanaume watatu kwa makosa ya jaribio la mauaji ya kigaidi. Operesheni kubwa za kupambana na ugaidi zilihusishwa na kuripotiwa kwa kitisho dhidi ya mashabiki wakati wa mechi za michuano ya Euro 2016.
Ubelgiji inaendelea kuwa katika tahadhari ya hali ya juu baada ya mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Kiislamu mwezi Machi.
Waripuaji wa kujitoa mhanga waliwauwa watu 32 katika mashambulizi yaliyoratibiwa dhidi ya uwanja mkuu wa ndege wa Brussels na njia za treni za chini ya ardhi.
Labels:
Ulinzi na Usalama
Location:
Ubelgiji
Mhandisi Kakoko ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Bandari Tanzania
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, leo amemteua Mhandisi Deusdedit Kakoko kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania.
Mhandisi Kakoko anachukua nafasi iliyoachwa na Ephraim Mgawe ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Kabla ya uteuzi, Mhandisi Kakoko alikuwa Meneja wa Miradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads).
Labels:
Kiuchumi
Location:
Dar es Salaam, Tanzania
Mripuko wa Bomu waua wanne mjini Benghazi, Libya
Maafisa wa usalama na Afya nchini Libya wamesema bomu lililokuwa limetegwa katika gari limeripuka nje ya hospitali katika mji wa Benghazi nchini humo na kuwaua watu wanne na kuwajeruhi wengine 14.
Afisa mwandamizi wa jeshi nchini Libya Brigedia Jenerali Abdul-Salam al-Hassi amewashutumu wanamgambo wa kundi la itikadi kali kwa kuhusika na shambulizi hilo lililotokea hapo jana.
Shambulizi hilo lililitokea nje ya hospitali ya Jalal nchini humo. Polisi wa kijeshi walilazimika kuweka kizuizi katika eneo hilo la hospitali baada ya kutokea kwa mripuko ambao ulisababisha moshi mweusi kutanda hadi katika eneo la kuegesha magari.
Afisa mwandamizi wa jeshi nchini Libya Brigedia Jenerali Abdul-Salam al-Hassi amewashutumu wanamgambo wa kundi la itikadi kali kwa kuhusika na shambulizi hilo lililotokea hapo jana.
Shambulizi hilo lililitokea nje ya hospitali ya Jalal nchini humo. Polisi wa kijeshi walilazimika kuweka kizuizi katika eneo hilo la hospitali baada ya kutokea kwa mripuko ambao ulisababisha moshi mweusi kutanda hadi katika eneo la kuegesha magari.
Labels:
Ulinzi na Usalama
Location:
Benghazi, Libya
Zaidi ya milioni moja wataka kura za maoni Uingereza zirudiwe
Zaidi ya watu milioni moja wamesaini waraka wakitaka kuitishwa mara ya pili kwa kura ya maoni baada ya upande wa kundi linalounga mkono kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya kushinda kufuatia kura za maoni zilizopigwa Alhamisi wiki hii.
Duru kutoka nchini Uingereza zinaonesha kuwa Tovuti ya bunge la nchi hiyo kwa wakati fulani ilionekana kuelemewa kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa wakitia saini waraka huo wakitaka kuitishwa upya kwa kura ya maoni.
Waliosaini waraka huo wanaitaka serikali ya nchi hiyo kuitisha upya kura hiyo ya maoni kwa kuzingatia kanuni ya kuwa iwapo idadi ya wanaounga mkono kubakia au kuondoka itakuwa chini ya asilimia 60 kutokana na idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura kuwa chini ya asilimia 75 basi lazima kuitishwe kura nyingine ya maoni.
Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura hiyo ya maoni Alhamisi iliyopita ilikuwa asilimia 72.2. Hadi hapo jana watu milioni moja na elfu arobaini walikuwa tayari wamesaini waraka huo katika tovuti maalumu ya serikali na bunge ikiwa ni mara kumi zaidi ya saini laki moja zinazohitajika kwa ajili ya pendekezo linalowasalishwa kupata nafasi ya kujadiliwa na bunge la nchi hiyo.
Duru kutoka nchini Uingereza zinaonesha kuwa Tovuti ya bunge la nchi hiyo kwa wakati fulani ilionekana kuelemewa kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa wakitia saini waraka huo wakitaka kuitishwa upya kwa kura ya maoni.
Waliosaini waraka huo wanaitaka serikali ya nchi hiyo kuitisha upya kura hiyo ya maoni kwa kuzingatia kanuni ya kuwa iwapo idadi ya wanaounga mkono kubakia au kuondoka itakuwa chini ya asilimia 60 kutokana na idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura kuwa chini ya asilimia 75 basi lazima kuitishwe kura nyingine ya maoni.
Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura hiyo ya maoni Alhamisi iliyopita ilikuwa asilimia 72.2. Hadi hapo jana watu milioni moja na elfu arobaini walikuwa tayari wamesaini waraka huo katika tovuti maalumu ya serikali na bunge ikiwa ni mara kumi zaidi ya saini laki moja zinazohitajika kwa ajili ya pendekezo linalowasalishwa kupata nafasi ya kujadiliwa na bunge la nchi hiyo.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
London, UK
Saturday, 25 June 2016
Mlipuko watokea Hotelini mjini Mogadishu
Mlipuko mkubwa umekumba hoteli moja katikati ya mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kuna sauti za ufyatulianaji wa risasi katika kile kinachoaminika huenda ni shambulio la wapiganaji wa Al-Shabab.
Kulingana na mwandishi wa BBC Ibrahim Aden mjini Mogadishu, mlipuko huo ulikumba hoteli ya Naso Hablod ikiwa ni hatua chache kutoka kwa uwanja wa ndegewa mji huo.
Hakuna ripoti zozote za majeruhi.Ripoti zinasema kuwa huenda kulikuwa na mlipuko wa pili.
Wapiganaji wa al-Shabab hutekeleza mashambulio ya mara kwa mara katika mji huo kwa lengo la kuiangusha serikali inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi.
''Walianza na mlipuaji wa kujitolea muhanga na baadaye kuvamia.Kwa sasa wako ndani na ufyatuliaji mkubwa wa risasi unaendelea'' ,alisema msemaji wa polisi meja Nur Farah.
Sudan Kusini kutoadhimisha siku ya Uhuru wake
Serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa haitasherehekea uhuru wake mwaka huu kutokana na uhaba wa fedha.
Waziri wa habari Michael Makuel Lueth amesema kuwa maadhimisho ya tano ya uhuru wa taifa hilo yatafanyika kwa ukimya.
Serikali pia inasema haitanunua magari ya kifahari kwa mawaziri wapya.
Tangu taifa hilo lijinyakulie uhuru wake kutoka kwa Sudan,limekubwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na mgogoro wa kiuchumi.
Sarafu yake imashuka na wafanyikazi wa serikali hawawezi kutosheka na mishahara yao ambayo hulipwa kuchelewa.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Sudan
Ndege za Urusi zafanya mashambulizi Nchini Syria
Ndege za kivita za Urusi na zile za Syria zilifanya mashambulizi ya anga katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika mji wa Allepo nchini Syria hapo jana. Kundi la waangalizi limethibitisha.
Mwakilishi wa shirika la habari la AFP katika eneo la mashariki mwa mji huo linalodhibitiwa na waasi alisema mashambulizi hayo yalidumu usiku kucha hadi asubuhi.
Mji wa Allepo ambao ulikuwa ni kitovu cha biashara na uzalishaji kabla ya kuibuka kwa mgogoro nchini humo mnamo mwaka 2011 uligeuka kuwa uwanja wa mapambano tangu pale waasi nchini humo walipofanikiwa kudhibiti eneo la upande wa mashariki mwa mji huo mwaka mmoja baada ya kuibuka kwa mgogoro huo.
Makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa siku mbili yaliyokuwa yamefikiwa na Urusi pamoja na Marekani mapema mwezi huu yamemalizika pasipo kuongezewa muda huku Urusi ikisema itaendeleza mashambulizi yake nchini humo kufuatia upande wa waasi kutotekeleza ahadi yake ya kutojihusisha na wafuasi wa kundi la itikadi kali la Al-Qaeda.
Mwakilishi wa shirika la habari la AFP katika eneo la mashariki mwa mji huo linalodhibitiwa na waasi alisema mashambulizi hayo yalidumu usiku kucha hadi asubuhi.
Mji wa Allepo ambao ulikuwa ni kitovu cha biashara na uzalishaji kabla ya kuibuka kwa mgogoro nchini humo mnamo mwaka 2011 uligeuka kuwa uwanja wa mapambano tangu pale waasi nchini humo walipofanikiwa kudhibiti eneo la upande wa mashariki mwa mji huo mwaka mmoja baada ya kuibuka kwa mgogoro huo.
Makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa siku mbili yaliyokuwa yamefikiwa na Urusi pamoja na Marekani mapema mwezi huu yamemalizika pasipo kuongezewa muda huku Urusi ikisema itaendeleza mashambulizi yake nchini humo kufuatia upande wa waasi kutotekeleza ahadi yake ya kutojihusisha na wafuasi wa kundi la itikadi kali la Al-Qaeda.
Labels:
Ulinzi na Usalama
Location:
Aleppo, Syria
Msajili: Rais hajazuia mikutano ya Siasa
MSAJILI wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi ametetea kauli ya Rais John Magufuli kuhusu kufanya siasa wakati huu na kwamba alichotaka kiongozi huyo wa nchi ni ushirikiano kutoka kwa wanasiasa wenzake ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Alisema Rais Magufuli, katika kauli yake ile hakumaanisha kuzuia shughuli za siasa nchini isipokuwa alieleza kuwa hatakuwa tayari kuona siasa zinakwamisha mikakati ya kuwapelekea wananchi maendeleo yao.
Jaji Mutungi alisema hayo Dar es Salaam jana, alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu kauli ya Rais Magufuli ya kuwataka watu kuacha siasa za hovyo hadi mwaka 2020 utakapofanyika uchaguzi mkuu mwingine, ili muda uliopo wautumie kuijenga nchi.
“Watu wametafsiri tofauti kauli ya Rais, lakini ni kwamba alikuwa akiomba ushirikiano wa wanasiasa wenzake na wadau wote wa siasa kuleta maendeleo… kwa hiyo kabla ya kukosoa kauli ni vyema ukafanya utafiti siyo kuibeba na kuitafsiri kwa mrengo tofauti,” alisema .
Alisema siyo kwamba Rais anapinga siasa isipokuwa anapingana na wanasiasa ambao ni pingamizi katika kuleta maendeleo na muda wote wamejikita katika siasa bila kuangalia namna ya kutekeleza ahadi zao kwa wananchi.
Alisema wapo watu walioitafsiri tofauti hotuba aliyoitoa juzi Rais Magufuli, hivyo wananchi wanapaswa kuwa watafiti na kuweka maslahi ya nchi huku akiwataka wanasiasa kuwa wavumilivu na kutumia muda wao kutafakari jambo kabla ya kuzungumza.
“Rais alikuwa akijaribu kuwasihi wanasiasa kuangalia namna ya kujikita kwenye siasa ya maendeleo ya jamii kwa ujumla na kuachana na siasa za kupinga maendeleo,” alisema.
Alisema dhamira ya Rais ni kuwaletea maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla na vyama vinapaswa kufuata utaratibu wa kuwasilisha taarifa kwa msajili na si kusubiri hadi vyombo vya habari kutoa taarifa.
Mutungi alisema vyama vya siasa vimekuwa vikitaka demokrasia nchini, hivyo kabla ya vyama kufikiria demokrasia kitaifa, hivyo viongozi wake waanze kuangalia suala hilo kwenye vyama vyao na si kuimba, kwani wapo wanaofanya ndivyo sivyo.
Alisema mtu anapotetea jambo, kwanza anapaswa kulitekeleza kwa vitendo huku akibainisha demokrasia kutotokea nchini endapo demokrasia ndani ya vyama vya siasa kuwa ni shida.
Jaji huyo alisema bado kuna kazi kubwa huku akibainisha yapo mambo mengi yanayotokea nchini huku akitegemea ushirikiano wao na kuwataka wanasiasa kuwekeza katika kufanya upembuzi wa mambo kabla ya kutamka au kuyatenda.
Naye Msajili Msaidizi, Kitengo cha gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma, Piencia Kiure alisema ni vyama vitatu tu kati ya 22 ndivyo vimewasilisha taarifa ya gharama za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.
Mwisho wa kuwasilisha gharama hizo ni leo. Alivitaja vyama vilivyowasilisha gharama za uchaguzi kuwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), ACT-Wazalendo na Chama cha Wananchi (CUF).
Alifafanua kuwa, mgombea atakayeshindwa kuwasilisha gharama za uchaguzi utahukumiwa kifungo kisichozidi mwaka mmoja au faini isiyozidi Sh milioni mbili au vyote kwa pamoja.
Aidha, chama kitakachoshindwa kuwasilisha gharama za uchaguzi katika kipindi kilichowekwa adhabu yake ni faini isiyozidi Sh milioni tatu na kutoruhusiwa kushiriki uchaguzi hadi watakapofanya marejesho.
Rais John Magufuli aagiza CCTV camera zifungwe mitaani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa rai ya kufunga CCTV kwenye mitaa, amesema Kinondoni ndio inasifika kuwa na uhalifu mwingi katika nchi hii. Amesema wilaya ya Kinondoni ilikuwa na vitendo vya uhalifu 8,094 na mwaka 2015 vikafika 8,804 huku akitoa agizo kwa TCRA ambao ndio wana wajibu wa ku-monitor simu zote washirikiane na jeshi la polisi. Asietaka kushirikiana na jeshi la polisi aondoke.
Rais Magufuli ameyasemahayo leo wakati akihutubia kwenye hafla ya Uzinduzi wa Kuboresha Usalama wa Raia, iliyofanyika kwenye Viwanja vya BIAFRA, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo Rais Magufuli alikuwa Mgeni Rasmi.
Mbali na hayo, rais Magufuli ameviagiza vyombo vya usalama nchini kuwachukulia hatua za kisheria mara moja makandarasi wote na injia ambao jana waliosimamishwa kazi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kujenga barabara chini ya kiwango jijini Dar es Salaam.
Jana, June 24, 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alizisimamisha kazi na kusitisha mikataba ya Kampuni ya Inshinomya Co. LTD na kuyasimamisha Makampuni mengine ya kujenga barabara ya Germinex construction LTD, Del Monte (T) Ltd na Skol Building Contraction.
Kutokana na kujenga barabara chini ya kiwango na kuagiza makampuni hayo kutopewa tenda yeyote kwenye Mkoa wa Dar es Salaam mpaka Mkuu wa Mkoa atakapojiridhisha na utendaji wa kazi kwa makampuni hayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, akisalimiana na wageni na viongozi walifika kwenye hafla hiyo.
Miongoni mwa waliofika kwenye hafla ya Uzinduzi wa Kuboresha Usalama wa Raia Viwanja vya BIAFRA ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Magufuli, Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mridho Kikwete, Katibu Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi John W.H. Kijazi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Lameck Nchemba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu, mwenyekiti wa mkoa Dar es Salaam, Madabida na wengine wengi.
Mzungumzaji aliyepita ni mkurugenzi wa CRDB, Dr. Charles Kimei na miongoni mwa mambo aliyogusia ni utumbuaji majipu.
IGP Mangu: Mangu amemshukuru Rais Kikwete kwani mpango wa kuliboresha jeshi la polisi ulibuniwa wakati wake.
Tutakaa na wataalam ili kubuni vyanzo fedha ili kutimiza tuliyoyapanga na ni mkakati ili kuboresha huduma tunazozitoa kwa wananchi na kero zote kwa jamii. Mangu anasema wakati Magufuli anafungua bunge alisema ‘Serikali nitakayoiunda nataka ihudumie jamii kwa haraka’ hivyo mpango wao unajibu hilo tatizo.
Amesema mkuu wa mkoa asaidie pia wananchi watakuwa wamejisaidia wenyewe kwa kuweka taa kwenye nyumba zao mbele na nyuma kwani jiji la Dar es Salaam liko kwenye giza. Mangu anasema Bilioni 27 zinahitajika ili jiji la Dar es Salaam liwe kwenye kiwango cha juu cha usalama pengine kuliko majiji yote Afrika.
Mwigulu Nchemba: Mwigulu amewataka wananchi wawe wanatoa taarifa ili kuzuia uhalifu, amemuomba Rais Magufuli kupata fedha za kuweza kutekeleza mpango wa jeshi la polisi ili kuundoa uhalifu kwenye jiji la Dar es Salaam ambayo pia itavutia wawekezaji. Amesema hadhara sio ya kwake na alikuwa anachomeka, anamkaribisha Rais Magufuli.
“Hamna demokrasia ambayo haina mipaka, mpango wa jeshi la polisi unatarajia kuanza utekelezaji wake Julai 1, 2016.” Alisema Mwigulu.
Rais Magufuli: Kwa niaba ya watanzania, niwashukuru wananchi wa Dar kwa kuweza kuacha shughuli zenu na kuja kuhudhuria, wateni wenzangu wakwere wanasema shughuli ni watu. Nawashukuru CRDB, NMB pamoja na Super doll ambao wakurugenzi wao wako hapa, pia nashukuru nchi ya Malaysia ambao ndio wamesaidia uanzishwaji wa big results now (BRN) na mimi nakushukuru kwa kuona matokeo ya big results now.
Nashukuru watu wa Biafra kwa kunipa kura nyingi.
Dar waupongeza Uongozi Muhimbili kwa kutoa chakula
Baada ya Juni 21 Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuanza utaratibu mpya wa kutoa chakula kwa wagonjwa kuanzai Julai 1, wananchi wa wa jiji la Dar es Salaam wamedai kuwa kitu hiko kitawezekana kama kitasimamiwa ipasavyo.
Wakati akitangaza agizo hilo kwa niaba ya uongozi wa hospitali ya Muhimbili, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha alisema kuwa utaratibu huo mpya, watatoza Sh 50,000 pindi watakapompokea mgonjwa, ambazo Sh 10,000 zitakuwa ni kwa ajili ya kitanda, Sh 10,000 ya kumuona daktari na Sh 30,000 itakuwa ni chakula kwa siku zote atakazokuwepo mgonjwa hospitali.
Alisema wamejipanga kutoa huduma bora ya chakula ambapo kwa wiki wagonjwa watakula ugali mara tano, wali mara tatu, pilau mara mbili na viazi mara tatu.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, mmoja kati ya wananchi wa jiji la Dar es Salaam waliotoa maoni yao kuhusu tukio hilo alisema kuwa tukio hilo siyo mara ya kwanza kutokea hapa nchi kwani miaka ya nyuma serikali iliwahi kufanya kama hivyo lakini baada wakasitisha zoezi hilo.
Jaji Mkuu asishauriane na Rais
Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imepinga pendekezo la Rais kushauriana na Jaji Mkuu katika kuanzisha Mahakama ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi, ikieleza kuwa hatua hiyo ni kuingilia mhimili wa Mahakama.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa licha ya kupongeza hatua ya Serikali kuanzisha divisheni hiyo alisema kamati yake haioni mantiki ya Rais kuingilia mamlaka ya Jaji Mkuu katika kuanzisha mahakama hiyo.
Katika marekebisho ya Sheria ya Usimamiaji Haki na Matumizi ya Sheria, Sura 358 yaliyowasilishwa bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, kifungu kipya 4A kinamwezesha Jaji Mkuu kuanzisha mahakama hiyo lakini kwa kushauriana na Rais.
“Kamati imebaki na msimamo wake na kuendelea kuitaka Serikali kuwa uhuru wa Mahakama usiingiliwe na mihimili mingine. Ni vyema Jaji Mkuu akabaki na mamlaka yake ya kuunda divisheni za Mahakama pasipo kuingiliwa na Rais,” alisema Mchengerwa.
Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe, alisema kuna umuhimu wa kutenganisha mihimili ya Dola na kumpa Jaji Mkuu haki ya kujiamulia mwenyewe mambo yanayohusu Mahakama.
Bashe pia alieleza kuwa uamuzi wa Serikali kuwa kesi zitakazosikilizwa na Mahakama hiyo kuanzia Sh1 bilioni ni kikubwa.
Alisema ukitazama ufisadi pamoja na uwepo wa rushwa kubwa kuna rushwa za kati zinazoiathiri Serikali Kuu na wananchi wengi.
Naishauri Serikali kupunguza kiasi hiki cha fedha hadi kufikia Sh100 milioni,” alisema.
Alisema dhana kubwa ya kupambana na rushwa ambayo ndiyo iliyofanya kuanzishwa kwa divisheni hiyo itapotea na pia itaruhusu baadhi ya watu kucheza na kiasi kwa kuhakikisha wanakuwa na mashtaka yasiyofikia kiwango hicho cha Sh1 bilioni.
Hata hivyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba, alipongeza hatua ya Serikali kuweka kiwango hicho cha fedha kwa sababu kingekuwa kiwango cha chini kingepunguza maana ya kuanzishwa kwa divisheni hiyo.
“Kwa kuweka Sh1 bilioni maana yake sasa tumeamua kupambana na rushwa kubwa,” alisema.
Pia, alisema suala la kuipa nguvu ya kisiasa divisheni hiyo kwa kuhakikisha inaanzia kwa Rais hadi ngazi ya chini si jambo baya.
“Hii ni kuonyesha kuwa hii vita tupo katika gari moja tunataka kupambana na rushwa kwa hiyo Rais kushirikishwa si jambo baya,” alisema.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe alisema haoni mantiki katika madai ya baadhi ya wabunge kuwa Jaji Mkuu kushauriana na Rais ni kuingilia muhimili mwingine.
“Kuwasiliana na kiongozi mwenzake wa muhimili mwingine ambaye ndiye anayetafuta pesa kuna tatizo gani? Hakuwezi kuwa ni kuingilia muhimili mwingine,” alisema.
Alisema kwa mujibu wa Katiba, Rais ndiye mkuu wa nchi, kiongozi wa Serikali na Amri Jeshi Mkuu hivyo anapaswa kufahamu.
Akijibu hoja hizo wakati wa kuchangia Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2016, Masaju alisema kuna kesi nyingi za ufisadi zinazozidi thamani ya Sh1 Bilioni na kutosha kusikilizwa na Divisheni ya Mahakama ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi.
Masaju alisema mapendekezo ya muswada huo yameletwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
“Na hawa ndio wapo kwenye tasnia hii, wanajua hiki kitu ambacho miaka mingi tumekuwa tukisema. Haya makesi yanayofikia Sh1 bilioni na kuendelea yapo ya kutosha,” alisema.
Masaju alisema Mahakama hiyo pia inatoa fursa kusikiliza makosa mengine ambayo katika uhalisia wake hayawezi kukadiriwa kwa kiasi hicho cha fedha.
Alisema kuna kifungu kwenye muswada huo ambacho kinampa mamlaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) katika masuala yenye masilahi kwa umma hata yale ambayo hayajafikia kiwango hicho na yale yasiyo ya uhujumu uchumi kupelekwa kwenye mahakama hiyo.
Alisema mambo mengine yanaibuka na mawaziri ndiyo wenye nafasi ya kujua mahitaji ya wananchi kutokana na kukutana na wananchi kwenye maeneo mbalimbali ikiwamo kwenye mikutano ya hadhara.
Masaju alisema kushauriana na waziri mwenye dhamana ya Katiba na Sheria hakuwezi kumaanishwa kuwa ni kuingilia muhimili mwingine. Mjadala huo uliahirishwa hadi Jumatatu.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Dodoma, Tanzania
Umoja wa Ulaya kujadili Mustakabali wa wanachama wake
Mataifa 6 waanzilishi wa Muungano wa Ulaya EU wanakutana hii leo kujadili mustakabali wao wa baadaye baada ya Uingereza kuamua kujiondoa kutoka kwa muungano huo.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, ufaransa,Italy, Ubelgiji, Luxembourg na Uholanzi wanatarajiwa kuanzisha mchakato huo pasi na kuwa na ngoja ngoja.
Tayari rais wa tume ya muungano wa Ulaya , Jean-Claude Juncker, amesema anataka kuanzisha majadiliano mara moja ya jinsi Uingereza itakavyotoka rasmi kutoka EU.
Viongozi wa Muungano wa Ulaya
Bw.Juncker amesema haieleweki kwamba swala hilo likumbwe na hadi waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, ang'atuke kutoka madarakani baada ya kushindwa katika kura hiyo ya maoni iliyoamua nchi hiyo ijibandue kutoka Umoja wa Ulaya.
Mawaziri hao pia wanatarajiwa kuweka masharti mapya yatakayowazuia wanachama wengine kuiga mfano wa Uingereza,baada ya vyama vya mrengo wa kulia katika mataifa mengi duniani kupongeza uamuzi huo wa Uingereza kujitoa kutoka muungano wa Ulaya.
Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, amewatahadharisha wenzake kutokuwa na hamaki na kutaka kuchua hatua za kama kuilipizia kisasi Uingereza.
Ameomba kuwepo kwa subira na umakini katika kulishughulikia suala hilo ambalo anasema linapaswa kuongozwa tu na vipi kushughulikia mahitaji ya raia wa jumuiya ya muungano wa Ulaya.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Ulaya
Hezbollah kutuma wapiganaji wake Syria
Kiongozi wa kundi la Hezbollah la Lebanon amesema jana kuwa kundi hilo litatuma wapiganaji zaidi katika jimbo la Aleppo nchini Syria, ambapo vikosi vinavyounga mkono upande wa serikali vinapambana na makundi ya waasi wa Syria katika maeneo mbalimbali.
Hassan Nasrallah ametoa ahadi hiyo licha ya kwamba kundi hilo la madhehebu ya Kishia linalomuunga mkono Rais wa Syria Bashar Al-Asaad limeshindwa vibaya mwezi huu katika mapigano yanayoendelea katika jimbo hilo la Aleppo.
Nasrallah amekiri kupoteza wapiganaji 26 katika mapigano hayo mwezi huu pekee lakini pia amedai kuwa zaidi ya wapiganaji 600 wameuawa upande wa adui wao.
Katika hotuba yake ya kumkumbuka Mustafa Badreddine aliyekuwa kamanda wa kundi hilo la Hezbollah ikiwa zimetimia siku 40 tokea alipouawa nchini Syria Nasrallah ameyataja mapigano yanayoendelea mjini Aleppo na jimbo zima kwa jumla kuwa ni mapambano makubwa ya vita nchini Syria.
Labels:
Ulinzi na Usalama
Location:
Lebanon
Obama kuendeleza Uhusiano wake kwa Uingereza na EU
Rais wa Marekani Barack Obama amewahakikishia Waingereza kwamba matokea ya kura ya maoni hayatoharibu uhusiano mzuri uliopo baina nchi hizo mbili.
Obama ambaye aliwahi kuisihi Uingereza isijiondoa katika Umoja wa Ulaya wakati wa ziara yake nchini humo mwezi Aprili, hapo jana alizungumza kwa njia ya simu katika wakati tofauti na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na kuwaahidi kwamba uhusiano wao wa karibu utaendelea kuwepo.
Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya inatishia hatua za kuufufua uchumi wa Marekani pamoja na kuwatia wasiwasi washirika wa Marekani katika masuala ya usalama wa kimataifa.
Obama ambaye aliwahi kuisihi Uingereza isijiondoa katika Umoja wa Ulaya wakati wa ziara yake nchini humo mwezi Aprili, hapo jana alizungumza kwa njia ya simu katika wakati tofauti na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na kuwaahidi kwamba uhusiano wao wa karibu utaendelea kuwepo.
Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya inatishia hatua za kuufufua uchumi wa Marekani pamoja na kuwatia wasiwasi washirika wa Marekani katika masuala ya usalama wa kimataifa.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Washington
Boris Johnson kushika hatamu za Waziri Mkuu Uingereza
Meya wa zamani wa London mji mkuu wa Uingereza Boris Johnson ambaye aliongoza kampeni ya kujiondoa katika Umoja wa Ulaya anatarajiwa kuwa miongoni mwa watakaowania wadhifa wa Waziri Mkuu, pale David Cameron atakapoondoka baada ya kutangaza kujiuzulu ifikapo mwezi Oktoba.
Hatua ya Cameron kutangaza kujiuzulu inatokana na raia wa nchi hiyo kuamua kujitenga na umoja huo katika kura ya maoni iliyofanyika juzi. Johnson amewahakikishia wapiga kura kwamba Uingereza imefanya vyema kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.
Wakati huo huo kiongozi mkuu wa Scotland Nicola Sturgeon amesema kwa vile idadi kubwa ya raia wa Scotland walipiga kura ya kutaka kubakia katika Umoja wa Ulaya hilo linamaanisha sasa kuna uwezekano mkubwa wa nchi hiyo kupiga kura upya ya kutaka kujitenga na Uingereza.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
London, UK
Mbunge CCM amtetea Rais John Magufuli
Kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa siku kadhaa zilizopita kuwa ‘siasa sasa basi isubiri mpaka 2020’ imeendelea kuzua gumzo miongoni mwa wabunge wa upinzani.
Hata hivyo, wakati wabunge hao wakiilalamikia, Mbunge wa Karagwe (CCM), Innocent Bashungwa amesema haoni kwa nini watu wameitafsiri vibaya kauli hiyo, wakati ilikuwa na nia njema.
“Rais Magufuli alikuwa anamaanisha kuwa uchaguzi umeisha, tushirikiane kwa pamoja bila itikadi ili tuijenge nchi yetu jambo ambalo ni zuri kabisa,” alisema Bashungwa.
Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe jana alipozungumza na vyombo vya habari, alisema hawatakubaliana na kauli ya Rais Magufuli ya kukataza mikutano ya shughuli za siasa hadi mwaka 2020 na kama hivyo ndivyo, Serikali iandae magereza ya kutosha.
Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alisema kutokana na kauli hiyo kuwa nzito, vyama vinavyounda umoja huo vitakutana na kujadiliana kabla ya kutoa msimamo wa pamoja.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Tanzania
UKAWA wamjibu Rais Magufuli, wasema Katiba inawaruhusu kufanya siasa
Mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni amepinga vikali kitendo cha Magufuli kuzuia watu kusema. Ali, "Unapozuia watu kusema unasababisha watu kusema kwa vitendo na wakisema kwa vitendo vitendo hivyo vinakuwa vya uvunjifu wa amani."
Alisema nchi ziizojaa vurugu ni nchi ambazo marais wake walikuwa wanajifanya wababe na watawala kujifanya wana mamlaka zote
Alishangaa pia kiongozi huyo wa Nchi aliposema kuwa atawalinda marais wastaafu kwani marais wastaafu wanalindwa na katiba wala sio kauli zake, aliwataka wasaidizi wake wamsaide aache "kuropoka" kwani kauli zake zinalifarakanisha taifa.
Naye mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia alisema Magufuli amewekwa na katiba ya Tanzania hivyo anashangaa yeye mwenyewe anapoipinga katiba na marais wengine wasingefuata katiba kama yeye anavyofanya leo hii asingekuwa rais wa Tanzania na kwamba hawezi kukataza siasa kwa kuwa ipo kikatiba na vyama vipo kisheria.
Aliongezea bila mgongano wa mawazo na demokrasia hakuna maendeleo hivyo.
Naye Peter Msigwa alisema Magufuli anaonekana anapata ushauri wa kijeshi kuliko wa kisiasa, alimtaka kutumia ushauri wa kisiasa kwani vyama vya upinzani vina wafuasi wengi na haitakiwi kutumia nguvu kama anajua maana ya siasa.
Alisema ni kweli nchi ilikuwa na ufisadi na ukosefu wa nidhamu nchini kutokana na utawala wa Kikwete kuwa dhaifu lakini pamoja na kuwa na nia nzuri ya kuondoa vitu hivyo vyote havimpi uhalali wa kufanya mambo bila kutumia sheria na taratibu zilizowekwa na wanamtaka avifanye kwa kutumia sheria.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Tanzania
Watumishi hewa mkoani Mwanza wazidi kubainika
Serikali imeingia hasara ya Sh2.1 bilioni baada ya kubainika kwa watumishi hewa 1,057 mkoani Mwanza.
Miongoni mwa watumishi hao wamo watoro, wastaafu, waliofukuzwa, waliofariki dunia, wasiojulikana kwa mwajiri na walioacha kazi na kujiingiza kwenye siasa lakini wanaendelea kulipwa mishahara.
Idadi hiyo ya watumishi hewa imebainika katika uhakiki uliofanyika kati ya Aprili 18 hadi Juni 3, baada ya ule wa awali kuwanasa 334.
Akitoa taarifa ya uchunguzi ulioshirikisha vyombo vya dola na mamlaka nyingine za Serikali, Mkuu Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema, “Niliagiza uhakiki ufanyike upya na watumishi wote waliokuwa masomoni, likizo au safari kurejea kwenye vituo vyao vya kazi kuhakikiwa kwa picha na nakala za miezi mitatu iliyopita ya malipo ya mishahara.”
Labels:
Habari mix
Location:
Mwanza, Tanzania
Neema ya Ajira kushuka Jijini Mwanza
Mkoa wa Mwanza unatarajia kutengeneza fursa za ajira milioni 1.5 ndani ya kipindi cha miaka 20 ijayo baada ya kukamilisha utekelezaji wa mpango wa jiji la Mwanza.
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Mwanza inakadiriwa kuwa na watu zaidi ya 800,000.
Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia watu 2.4 milioni ifikapo mwaka 2035.
Akiwasilisha rasimu ya mwisho ya mpango huo katika kikao cha wadau wa maendeleo jijini Mwanza, mtaalamu na mratibu wa mradi huo, Ketan Kulkarni amesema mpango huo utatoa dira na mwongozo wa matumizi endelevu ya ardhi na maendeleo ya jiji hilo.
Labels:
Kiuchumi
Location:
Mwanza, Tanzania
Kenya na Ethiopia zakubaliana ujenzi wa bomba la mafuta
Kenya na Ethiopia zimekubaliana kujenga bomba la mafuta litakaloanzia katika pwani ya Kenya na kuelekea hadi mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.
Kuna mpango wa kujenga bandari kubwa mjini Lamu lakini ujenzi huo umekuwa ukifanywa polepole.
Ethiopia ambayo haina bahari iko tayari kupunguza utegemeaji wake wa bandari ya Djibout ambayo ni mojawapo ya bandari ghali duniani.
Uganda hivi majuzi ilijiondoa katika makubaliano na Kenya mafuta yake yapitie nchini humo.
Kampuni iliyopewa kanadarasi ya ujenzi wa bomba hilo la Uganda iliamua lipitie nchini Tanzania kutokana na ukosefu wa usalama nchini Kenya ambako kuna mashambulizi ya mara kwa mara yanayotekelezwa na wapiganaji wa al-Shabab.
U.K huenda ikavunjika endapo Scotland watajiondoa baada ya Uingereza kujitoa EU
Waziri Kiongozi wa Scotland, Nicola Sturgeon, amesema kuna uwezakano mkubwa wa kuitishwa kwa kura nyengine ya maoni ya kujiondoa kwenye muungano na Uingereza, siku moja baada ya Waingereza kuamua kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.
Sturgeon amewaambia waandishi wa habari mjini Edinburgh, kwamba kuna hatari ya Scotland kuondolewa kwenye Umoja wa Ulaya, ambako inataka kubakia, jambo ambalo halikubaliki.
Asilimia 62 ya wapigakura wa Scotland, ambayo ni nchi ndani ya Muungano wa Uingereza, waliamua kusalia kwenye Umoja wa Ulaya kwenye kura ya maoni ya hapo jana.
Lakini kura ya jumla, imetoa ushindi kwa kundi la wanaotaka kujitoa kwa asilimia 52 dhidi ya 48.
Kwenye kura ya mwaka 2014, Scotland ilishindwa kujitangazia uhuru kutoka Uingereza baada ya asilimia 55 kuamua kusalia kwenye muungano huo wa miaka 300.
Kampeni kubwa ya waliotaka Scotland isalie kwenye Muungano wakati huo ilikuwa ni manufaa ya kiuchumi inayoyapata Scotland kwenye Umoja wa Ulaya kupitia Muungano wake na Uingereza.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Uingereza
Friday, 24 June 2016
Umoja wa Ulaya wataka Uingereza iondoke haraka
Viongozi wa muungano wa Ulaya wamesisitiza kuwa Uingereza inafaa kujiondoa kwa haraka katika muungano huo wakidai kuwa kuchelewa kwake huenda kukazua wasiwasi miongoni mwa mataifa yaliosalia.
Kamishna wa tume ya Ulaya Jean Claude Juncker amesema kuwa muungano wa mataifa 27 yaliosalia utaendelea.
Uingereza ilipiga kura ya aslimia 52 dhidi ya 48 kuondoka katika muungano wa Ulaya huku waziri mkuu David Cameron akisema kuwa atajiuzulu ifikapo mwezi Oktoba.
Bw Juncker alifanya mkutano wa dharura na rais wa bunge la Ulaya Martin Schulz ,rais wa baraza la Ulaya Donald Tusk na waziri mkuu wa Ujerumani Mark Rutte na kutoa taarifa hiyo siku ya Ijumaa.
Baadaye walitoa taarifa wakisema wanajuta lakini wanaheshimu uamuzi huo wa Uingereza.
Wameitaka Uingereza kuondoka haraka licha ya mpango huo kuwaathiri na kwamba kuchelewa kwake kutazua mgogoro ndani ya muungano huo.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Ulaya
Rais Jacob Zuma kushtakiwa
Mahakama nchini Afrika Kusini imetupilia mbali jaribio la Rais Jackob Zuma, kukata rufaa kupinga hukumu iliyoagiza afunguliwe mashtaka ya rushwa zaidi ya 800, uamuzi unaoongeza shinikizo kwa kiongozi huyu.
Rais Zuma alijaribu kupindua uamuzi wa awali wa mahakama wa mwezi April, ya kwamba ofisi ya mwendesha mashtaka ifungue upya mashtaka ya rushwa dhidi yake, yaliyofutwa mwaka 2009, siku chache kabla ya kuwa Rais.
Mashtaka dhidiya Rais Zuma yanahusu rushwa, udanganyifu, utakatishaji fedha na matumizi mabaya ya fedha za umma, kuhusu ununuzi wa silaha za kijeshi uliogharimu mabilioni ya dola za Marekani.
Rais Zuma amekuwa akipamabana kusafisha jina lake kutokana na tuhuma kadhaa za rushwa zinazomkabili, sambamba na ukosolewaji mkubwa kuhusu sera ya ajira nchini humo.
"Tuliangalia kwa umakini ikiwa rufaa hii ingekuwa na sababu za msingi za kufanikiwa na tumefikia hitimisho ya kuwa hakuna sababu za msingi kwenye hoja zilizowasilishwa." alisema jaji Aubrey Ledwaba wa mahakama kuu ya Pretoria.
Mwaka 2009, ofisi ya mwendesha mashtaka ilitoa maelezo ya kwa nini ilimuondolea Rais Zuma mashtaka zaidi ya 700 ya rushwa, ikisema mawasiliano yaliyonaswa wakati wa utawala wa rais Thabo Mbeki hayakuwa na uhusiano wowote kwenye kesi ikiwa wangefungua mashtaka.
Uamuzi huu wa ofisi ya mwendesha mashtaka, ulisafisha njia kwa Rais Zuma, kiongozi wa chama tawala nchini humo cha ANC, kuwania urais wiki chache baadae. Uamuzi wa mahakama unatoa njia kwa Rais Zuma, kiongozi wa chama tawala cha ANC kujiandaa kupandishwa mahakamani.
Mawasiliano yaliyorekodiwa ambayo yalifahamika kama "Spy tapes" yalifanywa kuwa siri, hadi pale yalipowekwa wazi mwaka 2014 baada ya muda mrefu wa ushindani wa kisheria mahakamani kesi iliyofunguliwa na chama cha upinzani cha Democratic Alliance.
Kwa uamuzik huu, inamaanisha kuwa ofisi ya mwendesha mashtaka itapaswa kumfungulia Rais Zuma mashtaka rasmi ya rushwa, na kumtaarifu tarehe rasmi ya kutakiwa kufika mahakamani.
Madiwani 56 wateuliwa Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheir, amewateua madiwani 56 ambao wataungana na wenzao wa kuchaguliwa kushiriki mabaraza ya miji Zanzibar.
Kwa mujibu wa uteuzi huo, madiwani 36 ni wanawake ambao ni sawa na asilimia 64 na madiwani 20 ni wanaume.
Aliyaagiza mabaraza yote kuwaapisha madiwani hao kuyatumika mabaraza yao na kuandaa taratibu za uchaguzi na kufanya uchaguzi wa viongozi kwa mabaraza ya miji na halmsahauri kabla ya Julai 20, mwaka huu.
Uingereza yajing'oa EU, Kenya wataathirika vipi?
Gavana wa benki kuu ya Kenya amejiunga na gavana wa benki kuu ya Uingereza na mataifa mengine kujiandaa kwa mdororo wa sarafu za mataifa yao kufuatia kauli ya Uingereza kujiondoa kwenye muungano wa Ulaya.
Gavana Patrick Njoroge kupitia kwa taarifa kwa vyombo vya habari amesema kuwa wakotayari kusaidia soko la ubadilishani wa fedha iwapo kauli hiyo ya waingereza itaathiri pakubwa sarafu ya Kenya. Kenya ambayo ilitawaliwa na Uingereza wakati wa ukoloni inauhusiano wa karibu sana na taifa hilo.
Asili mia 52% ya waingereza walipiga kura wakitaka nchi hiyo ijiondoe kwenye muungano wa Ulaya.
Aidha biashara nyingi na haswa zile za uuzaji wa bidhaa nje ya nchi hiyo huelekea Uingereza.
Kauli hiyo inafuatia tangazo la gavana wa benki kuu ya Uingereza Mark Carney,muda mchache uliopita kuwa hawatasita kamwe kuingilia kati endapo thamani ya sarafu ya Uingereza itaporomoka zaidi kufuatia kauli ya waingereza kujiondoa.
Bwana Carney anasema kuwa benki hiyo imejiandaa na mpango mbadala wa kuepuka mdororo wa kiuchumi unaotarajiwa katika siku za hivi punde.
Uamuzi huo wa Uingereza umesababisha kudorora pakubwa kwa sarafu ya Uingereza.
Huko Afrika Kusini, soko la hisa la Johannesburg limeporomoka kwa asilimia 4%, huku kukiwa na shauku kutoka kwa wadadisi kuwa huo ndio mwanzo tu wa msukosuko katika uchumi wa ulimwengu kuhusiana na kura hiyo ya kujiondoa ya Uingereza.
Uamuzi huo wa Uingereza umesababisha kudorora pakubwa kwa sarafu ya Uingereza ya Sterling Pound mbali na kuyumbisha soko la biashara duniani.
Katika soko la hisa jijini London, mdororo wa asilimia 8 ulishuhudiwa na kuweka historia chini kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa kipindi cha miaka 30.
Labels:
Afrika Mashariki
Location:
Nairobi, Kenya
Subscribe to:
Posts (Atom)