Tuesday, 28 June 2016

Scotland yang'ang'ania kubaki EU


Waziri kiongozi  wa  Scotland  amesema  utawala  wake utafanya  kila  linalowezekana  kubakia  katika  Umoja  wa Ulaya.

Nicola Sturgeon  amesema  jana  kwamba  hatua hizo  ni  pamoja  na  uwezekano  wa  kuzuwia  hatua  za kisheria zinazohusiana  na  kujitoa  kwa  Uingereza  kutoka kundi  hilo  la  mataifa.


Wapiga  kura  wa  Scotland wameunga  mkono  kwa  wingi mkubwa  kubakia  katika  Umoja  wa  Ulaya. Sturgeon  pia amesema  kura  ya  pili  ya  maoni  kuhusiana  na  uhuru wa  Scotland  kutoka  Uingereza  pia itajadiliwa.

Amedokeza  kwamba  kinachomuongoza  katika  suala  hilo ni  kulinda  maslahi  ya  Scotland na  hasisitizi  kuhusu uhuru, lakini  iwapo uhuru  unakuwa  ndio  njia  pekee  ya kulinda maslahi  ya  Scotland  basi  itakuwa chaguo litakalojadiliwa.

No comments:

Post a Comment