Showing posts with label Kiuchumi. Show all posts
Showing posts with label Kiuchumi. Show all posts

Sunday, 26 June 2016

Mhandisi Kakoko ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Bandari Tanzania


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, leo amemteua Mhandisi Deusdedit Kakoko kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Mhandisi Kakoko anachukua nafasi iliyoachwa na Ephraim Mgawe ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Kabla ya uteuzi, Mhandisi Kakoko alikuwa Meneja wa Miradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads).

Saturday, 25 June 2016

Neema ya Ajira kushuka Jijini Mwanza


Mkoa wa Mwanza unatarajia kutengeneza fursa za ajira milioni 1.5 ndani ya kipindi cha miaka 20 ijayo baada ya kukamilisha utekelezaji wa mpango wa jiji la Mwanza.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Mwanza inakadiriwa kuwa na watu zaidi ya 800,000.

Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia watu 2.4 milioni ifikapo mwaka 2035.

Akiwasilisha rasimu ya mwisho ya mpango huo katika kikao cha wadau wa maendeleo jijini Mwanza, mtaalamu na mratibu wa mradi huo, Ketan Kulkarni amesema mpango huo utatoa dira na mwongozo wa matumizi endelevu ya ardhi na maendeleo ya jiji hilo.

Kenya na Ethiopia zakubaliana ujenzi wa bomba la mafuta


Kenya na Ethiopia zimekubaliana kujenga bomba la mafuta litakaloanzia katika pwani ya Kenya na kuelekea hadi mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.

Kuna mpango wa kujenga bandari kubwa mjini Lamu lakini ujenzi huo umekuwa ukifanywa polepole.

Ethiopia ambayo haina bahari iko tayari kupunguza utegemeaji wake wa bandari ya Djibout ambayo ni mojawapo ya bandari ghali duniani.

Uganda hivi majuzi ilijiondoa katika makubaliano na Kenya mafuta yake yapitie nchini humo.

Kampuni iliyopewa kanadarasi ya ujenzi wa bomba hilo la Uganda iliamua lipitie nchini Tanzania kutokana na ukosefu wa usalama nchini Kenya ambako kuna mashambulizi ya mara kwa mara yanayotekelezwa na wapiganaji wa al-Shabab.

Thursday, 23 June 2016

KCB yafuturisha wateja wake mkoani Arusha


Benki ya KCB Tanzania imekuwa mwenyeji wa hafla ya futari kwa wateja na wadau wake wa jiji la Arusha. Shughuli hiyo ilifanyika katika hoteli ya kitalii ya Kibo Palace ambapo wageni zaidi ya mia moja walialikwa ili kushiriki pamoja futari katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Moezz Mir alipokuwa akikaribisha wageni wake alisema kuwa mwezi wa Ramadhani ni wakati muhimu wa kushiriki pamoja na kuendeleza umoja na amani nchini.

“Nawashukuru wote kwa kuwa washirika wa muhimu sana kwa benki yetu ya KCB Tanzania.Tunathamini sana uhusiano wetu na nyie na kila mara tunaendelea kutafuta nafasi ya kuweza kuwapa huduma bora zaidi,” alisema Moezz.

Mkurugenzi Mkuu wa benki KCB Tanzania, Moezz Mir akizungumza wakati wa futuru iliyoandaliwa kwa wateja na wadau wa benki hiyo, jijini Arusha.

KCB Tanzania ni benki ya kwanza nchini kwa kutoa huduma ya kibenki kwa kufuata masharti ya dini ya Kiislamu. Huduma hii ya kibenki inafuata maadili ya Sharia hutolewa katika matawi yote ya KCB nchini hata hivyo benki ya KCB pia ina tawi maalum kwa huduma hii ambalo liko Lumumba jijini Dar es Salaam.

Katika bidhaa na huduma zinazotolewa chini ya Sharia ni pamoja na mikopo, uwekaji fedha na uwekezaji.

Bandari ya Dar es Salaam yalipuliwa tena, kunani?


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameapa kusambaratisha mtandao wa kifisadi uliopo Bandari ay Dar es Salaam.

Ameiagiza pia bodi mpya ya Bandari kushughulikia tatizo hilo alilodai kuwa ni kubwa na linahatarisha utendaji kazi wa bandari.

Akizungumza katika uzinduzi wa bodi hiyo jijini Dar es Salaam jana, Profesa Mbarawa alisema kuna baadhi ya kampuni za kupakua mizigo bandari zenye wafanyakazi walioajiriwa na bandari, huku baadhi yao wakiwa wameajiriwa kwa upendeleo.

“Kuna wafanyakazi wengi wa bandari wanaofanya kazi katika kampuni binafsi bandarini. Kuna kampuni (anaitaja) ambayo mume wa mmiliki wake aliyeajiriwa bandari ana hisa asilimia 50, tumefanya uchunguzi lakini Mwanasheria wa Bandari anasema hakuna  conflict of interest (mgongano wa kimaslahi). Mwanasheria gani huyu?” alihoji Profesa Mbarawa na kuongeza:

“Watu wameajiri ndugu zao bandarini, kuna mtu ameajiri ndugu zake saba.

Wednesday, 22 June 2016

Tani 5 za kahawa zakamatwa wilaya ya Kyerwa


Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kupitia kamati yake ya mapato na kudhibiti biashara ya magendo imekamata zaidi ya tani tano za kahawa zenye thamani ya  shilingi milioni 6  zikivushwa kimagendo nje ya nchi.

Biashara ya kahawa na maharage iliyokuwa ikifanyika katika njia zisizo rasmi na kuacha nchi ikikosa mapato yake, sasa huenda ikaanza kufuata utaratibu mara baada ya serikali katika wilaya ya Kyerwa, kuunda timu ili kudhibiti hali hiyo iliyokuwa imeota mizizi, ambapo wafanyabiashara walio wengi ukwepa kupita katika mipaka rasmi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Innocent Maduhu ambaye pia ni Kaimu Afisa Mipango wa wilaya hiyo, amesema wananchi walioko mpakani wana mazoea ya kuuza kahawa na mazao mengine kwa wanunuzi wasio rasmi, ambao hutorosha bidhaa hizo nje ya nchi kupitia mto Kagera, unaotenganisha nchini ya Tanzania na Uganda.

Katika zoezi hilo mbali na kukamatwa kwa zaidi ya tani tano za kahawa, pia vitu mbalimbali ikiwemo pikipiki kumi, baiskeli na mitumbwi iliyokuwa ikisafirisha bidhaa hizo, pia vilikamatwa.

Uingereza kuathiri Uchumi wa Kenya endapo itajiondoa EU


Kenya inasema itakuwa miongoni mwa nchi mbalimbali duniani zitakazotikisika kiuchumi ikiwa Uingereza itajiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Gavana wa Benki Kuu nchini humo Patrick Njoroge, ambaye pia aliwahi kuwa mmoja wa wachumi wa Shirika la fedha duniani IMF, amesema ni muhimu sana kwa Uingereza kusalia katika Umoja huo ili uchumi wa nchi yake uendelee kuwa imara pamoja na kuendelea kwa biashara.

Watalaam wa uchumi nchini Kenya nao wanasema, makampuni kadhaa yanayosafirisha bidhaa nchini Uingereza, biashara zitayumba ikiwa Uingereza itajitoa.

Aidha, wanaongeza kuwa matokeo ya kujitoa yanaweza kusababisha mzozo wa kiuchumi duniani, uliowahi kushuhudiwa mwaka 2008.

Kenya imekuwa ikituma bidhaa kama maua katika soko la Uingereza chini ya mwafaka wa Umoja wa Ulaya, na kufanya bei ya ufanyaji biashara kuwa rahisi.

Mbali na Kenya, mataifa makubwa kiuchumi duniani kama Marekani, Ufaransa na Ujerumani yamewataka raia wa Uingereza kupiga kura ya kusalia katika umoja huo.

Raia wa Uingereza kesho Alhamisi watafanya uamuzi huo wa kihistoria wa kusalia au kuondoka kwenye umoja huo.

Kenya kuuza mafuta nje ya nchi ifikapo 2017


Siku ya Ijumaa Kenya ilitangaza kuwa ina mipango ya kuanza kuuza mapipa 2,000 ya mafuta kwa nchi zingine za nje kwanzia Julai mwaka 2017.

Hayo yalibainishwa na naibu mkuu wa wafanyakazi katika ofisi ya rais Nzioka Waita alipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Nairobi.

Mafuta hayo yanatoka katika bonde la Lokichar kaskazini mwa Kenya .

Aidha Waita aliongezea kwa kusema kuwa mafuta hayo ghafi mwanzo ni yatasafirishwa kwa barabara na reli huku ujenzi wa bomba la mafuta ukitarajiwa kukamilika mnamo mwaka 2022.

Kenya ilifanya ugunduzi wa mafuta kwa mara ya kwanza mwezi Mchi mwaka 2012 na pia kugundua mapipa milioni 750 ya hifadhi za mafuta.

Hata hivyo Waita alifahamisha kuwa Kenya kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya uhaba ya wafanyakazi wenye Ujuzi wa kiufundi katika sekta ya utafutaji wa mafuta.

Marekani na kura ya Uingereza


Mkuu wa kitengo cha shirikisho la uhifadhi nchini Marekani ,Janet Yellen, ametupilia mbali hoja ya Marekani kuingia kwenye kipindi cha mpito na kuyumba kwa uchumi wake endapo Uingereza itajiondoa katika umoja wa ulaya.

Wakati akijibu maswali kutoka katika kamati ya Senate, Yellen amesema kipindi cha mpito na kuyumba kwa uchumi wa nchi yake hakutokani ama haitakuwa chanzo cha kura hiyo, hakuna ajuaye nini kitatokea.

Ameeleza imani yake kwa wawekezaji kwamba watafanya maamuzi sahihi na kuamua kwa busara katika masoko ya fedha, ambako italeta taswira bei shirikishi na viwango vya juu vya riba kwa wakopaji walio wengi.

Tuesday, 21 June 2016

Uhaba wa chakula kuikumba Yemen


Raia wengi wa Yemen wanakabiliana na uhaba wa chakula kwa mujibu wa tathimini mpya ya pamoja iliyofanywa na Umoja wa Mataifa na washirika.

Tathmini ya sasa ya pamoja ya hali ya chakula “Intergrated Food Security Phase Classification" (IPC) inaonyesha kwamba kata 19 ama 22 za Yemen zinakabiliana na uhaba mkubwa wa chakula.

Taarifa zinaeleza kwamba zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini humo wanakabiliana na kiwango cha hatari, ikiwa ni kundi la nne katika mfumo uliogawanyishwa mara tano katika utambuzi wa hali ya uhaba wa chakula.

Uhaba wa mafuta na vikwazo vya uingizwaji ndani ya nchi vimechangia kusababisha uhaba wa chakula katika nchi iliyovitani ya Yemen.

Nchi hiyo inatumia asilimia 90 ya chakula chake kutoka nje ya nchi, na mafuta yaliyoingizwa nchini mwezi March yalitosheleza asilimia 12 tu ya mahitaji.

Obama: Marekani ni bora kwa Uwekezaji


Rais wa Marekani Barack Obama amesema hakuna sehemu nzuri zaidi au muda wa kuwekeza kuliko Marekani wakati huu.

Rais Obama alitoa maelezo hayo mjini Washington Jumatatu katika mkutano wa uwekezaji unaojulikana kama SelectUSA unaojumuisha maafisa waandamizi wa Marekani, wakurugenzi katika sekta ya biashara, na viongozi wengine ukiwa na lengo la kuchochea uwekezaji wa moja kwa moja wa nje ndani ya Marekani.

Katika maelezo yake Obama alisema mkutano huo unatoa fursa kwa kila upande Marekani kwa ajili ya uwekezaji wa dunia. Amesema jumuiya za ndani zinazokaribisha uwekezaji wa nje zinakuwa kwa haraka kiuchumi kuliko zile zinazogomea fursa hiyo.

Anasema kwa sababu mkutano kama huu ulifanyika miaka mitatu iliyopita makampuni yaliyoshiriki yaliwekeza zaidi ya dola bilioni 10 katika majimbo 35 ya Marekani na vitongoji vyake.

Obama amesema mkutano huo hauna lengo tu la kufikia makubaliano ya mikataba na kutengeneza pesa, ajira na biashara lakini pia una lengo la kuweka ushirikiano bora kote katika mipaka. Anasema makampuni yanapokuja pamoja inapelekewa uwelewa mzuri wa watu kutoka katika mipaka na kote duniani.

SelectUSA ni programu ya Serikali inayohusisha biashara kimataifa ndani ya idara ya biashara ya Marekani. Programu hiyo imeripoti kuwa tangu ilipoanzishwa imeweza kuwekeza zaidi ya dola bilioni 19 na kutengeneza maelfu ya ajira Marekani.

Sarafu ya Nigeria yashuka thamani

Kwa miezi kadhaa, rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amekua akipinga wazo la kushusha dhamani ya sarafu ya nchi yake - naira. Msimamo huo ulibadilika jumatatu baada ya Benki kuu kuchukua hatua ya kuweka sarafu hiyo kwenye soko huru na kusababisha mara moja thamani ya Naira kushuka kwa asilimia 30 dhidi ya dola ya marekani.

Lakini huwenda hatua hiyo imeokoa kudorora kwa uchumi wa Nigeria unaotegemea mafuta. Wachumi wamesema kuiweka Naira kuwa imara kulimaliza akiba ya fedha za kigeni ya Nigeria na kuwatia hofu wawekezaji.

Mashambulizi ya wanamgambo dhidi ya miundo mbinu nyeti ya mafuta pamoja na kushuka kwa bei za mafuta na upungufu wa sarafu za kigeni kumehujumu uchumi mkubwa wa barani Afrika na hivyo kushushwa thamani ya sarafu ya Nigeria ni jambo lisiloweza kuepushwa.

Monday, 20 June 2016

UDART kuanza kutumua kadi za kulipia


Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (UDART) imeanzisha huduma kwa wateja wao za kutumia kadi maalumu wakati wa kupanda mabasi hayo itakayoanza rasmi kesho.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwasa alisema wameanza kutoa huduma hiyo ya kadi ili kuwarahisishia wateja wao na kuondoa changamoto ya kusubiri tiketi kwa muda mrefu kabla ya kuondoka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu alisema kwamba kwa kuanzia wametoa kadi 200,000 ambapo kila kadi itauzwa kwa shilingi 5000 ingawa bei halisi kwa kadi moja ni shilingi 500 na sh.4500 inayobaki itakuwa ni malipo ya mteja wao.

“Shilingi 4500 zitatumika kama malipo ya nauli kwa siku saba hadi nane kwa kwenda eneo lolote na kuwa kadi hizo zitapatikana katika vituo vya Kimara, Mbezi, Morocco, Gerezani, Posta na kuwa zitakuwa ni endelevu,” alisema Rajabu.

Aliongeza kuwa katika nchi nyingi zimekuwa zikitumia kadi hizo katika kusafirisha abiria na kuwa kwa hapa nchini ni huduma mpya ambayo itakuwa na changamoto zake kabla ya kuzoeleka.

Alisema licha ya kuanzisha huduma ya kadi bado ile ya risiti itaendelea kama kawaida ambapo alisema namna ya kujiunga na huduma hiyo unatakiwa.

Friday, 17 June 2016

Poland kuinua kilimo cha Tanzania kwa kuipa matrekta


Tanzania kupata matrekita ya kilimo kutoka Poland
Kampuni moja inayohusika na utengenezaji wa matireketa ya kilimo ya Ursus ya nchini Poland  imetiliana saini na Shirika moja la kujenga Taifa la nchini Tanzania kwa ajili ya kusambaza jumla ya matrekita 2,400, pamoja na zana nyingine za kilimo na vipuri nchini humo. Kampuni hiyo ambayo pia imekuwa ikifanya biashara na Ethiopia inaendelea na mazungumzo kwa ajili ya usambazaji wa zana hizo za kilimo katika mataifa ya Angola na Nigeria. Mauzo ya nje ya Poland kwa mataifa ya bara la Afrika yanakadiriwa kufikia thamani ya dola bilioni 4.5, likiwa ni ongezeko la karibu kiwango cha asilimia 20 kwa mwaka.

Thursday, 16 June 2016

Marekani yatoa onyo kwa China kuhusu thamani ya Yuan

Waziri wa Fedha wa Marekani Jack Lew ameionya China kwamba hatua ya kurudi tena katika sera yake ya kuishusha thamani sarafu yake ya Yuan katika soko la ubadilishanaji fedha dhidi ya sarafu ya dola inaweza kuchochea duru mpya ya mvutano kati nchi hizo mbili. Akizungumza katika taasisi ya biashara ya Marekani waziri huyo wa fedha wa nchi hiyo amesema uhusiano wa kibiashara kati ya China na Marekani umetoka mbali kuhusiana na suala hilo la kiwango cha ubadilishanaji wa sarafu. Sambamba na hayo Lew amebaini kwamba China bado inabidi kuchukua hatua zaidi katika kuleta mageuzi kwenye soko hilo la ubadilishanaji wa sarafu na kuongeza kwamba maafisa wa China wamejitolea katika mikutano iliyofanyika wiki iliyopita mjini Beijing kuendelea kufanya mageuzi ambayo yanaruhusu sarafu ya Yuan ya China kupanda thamani na kushuka kuambatana na nguvu za soko hilo itakavyokuwa.

Wakurugenzi kubanwa mbavu kuhusu mikopo ya wanawake na vijana


Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema itaanza kuwashughulikia wakurugenzi wa halmashauri ambao hawatoi asilimia 10 ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanawake na vijana.

 Hii si mara ya kwanza kwa ofisi hiyo kutoa maagizo hayo licha ya utekelezaji wake kuwa mdogo.

 Mwaka 2013, aliyekuwa Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri alitoa tamko kama hilo.

 Jana, Naibu Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Sikudhani Chikambo (CCM), amesema ni marufuku kwa halmashauri yoyote kutumia asilimia 10 iliyotengwa kwa ajili ya wanawake na vijana.

Wafanyabiashara wapunguza ujazo wa Sukari


Mbeya. Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA), Mkoa wa Mbeya, Deogratius Hussein amesema wafanyabiashara wa sukari wamekuwa wakipunguza ujazo kutoka kilo moja hadi gramu 700.

 Amesema msako unaendelea kupambana nao na kwamba watatu wamekamatwa huku mmoja akifikishwa kortini na wawili kutozwa faini ya Sh300,000 kila mmoja.

 Tayari kilo 1,150 za sukari zimeingia mkoani humo kutoka nchini Malawi kwa lengo la kupunguza upungufu wa bidhaa hiyo.

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amesema anaamini tatizo la ukosefu wa sukari litakwisha, kwani hadi sasa tani 130 zimeingia.