Wednesday, 22 June 2016

Kenya kuuza mafuta nje ya nchi ifikapo 2017


Siku ya Ijumaa Kenya ilitangaza kuwa ina mipango ya kuanza kuuza mapipa 2,000 ya mafuta kwa nchi zingine za nje kwanzia Julai mwaka 2017.

Hayo yalibainishwa na naibu mkuu wa wafanyakazi katika ofisi ya rais Nzioka Waita alipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Nairobi.

Mafuta hayo yanatoka katika bonde la Lokichar kaskazini mwa Kenya .

Aidha Waita aliongezea kwa kusema kuwa mafuta hayo ghafi mwanzo ni yatasafirishwa kwa barabara na reli huku ujenzi wa bomba la mafuta ukitarajiwa kukamilika mnamo mwaka 2022.

Kenya ilifanya ugunduzi wa mafuta kwa mara ya kwanza mwezi Mchi mwaka 2012 na pia kugundua mapipa milioni 750 ya hifadhi za mafuta.

Hata hivyo Waita alifahamisha kuwa Kenya kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya uhaba ya wafanyakazi wenye Ujuzi wa kiufundi katika sekta ya utafutaji wa mafuta.

No comments:

Post a Comment