Thursday, 16 June 2016

Marekani yatoa onyo kwa China kuhusu thamani ya Yuan

Waziri wa Fedha wa Marekani Jack Lew ameionya China kwamba hatua ya kurudi tena katika sera yake ya kuishusha thamani sarafu yake ya Yuan katika soko la ubadilishanaji fedha dhidi ya sarafu ya dola inaweza kuchochea duru mpya ya mvutano kati nchi hizo mbili. Akizungumza katika taasisi ya biashara ya Marekani waziri huyo wa fedha wa nchi hiyo amesema uhusiano wa kibiashara kati ya China na Marekani umetoka mbali kuhusiana na suala hilo la kiwango cha ubadilishanaji wa sarafu. Sambamba na hayo Lew amebaini kwamba China bado inabidi kuchukua hatua zaidi katika kuleta mageuzi kwenye soko hilo la ubadilishanaji wa sarafu na kuongeza kwamba maafisa wa China wamejitolea katika mikutano iliyofanyika wiki iliyopita mjini Beijing kuendelea kufanya mageuzi ambayo yanaruhusu sarafu ya Yuan ya China kupanda thamani na kushuka kuambatana na nguvu za soko hilo itakavyokuwa.

No comments:

Post a Comment