Thursday, 16 June 2016
Bulgaria yajitoa NATO dhidi ya Urusi
Waziri mkuu wa Bulgaria amesema nchi yake haitojiunga na mpango maalum wa kijeshi uliopendekezwa na Jumuiya ya kujihami ya NATO wenye lengo la kuvikabili vikosi vya Urusi katika bahari nyeusi kwasababu nchi yake haiko tayari kuona vita katika eneo hilo. Tamko la Bulgaria limekuja siku moja baada ya Urusi kuonya dhidi ya hatua yoyote ya kuongeza uwepo wa kijeshi kwenye eneo hilo. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na rais Rosen Plevneliev, waziri mkuu Boiko Borisov amesema hataki kuona meli za kijeshi zikielea katika maeneo ya kitalii.Rais Plevneliev kwa upande wake ameitaja Bulgaria kuwa nchi ya amani. Mvutano kati ya Urusi na Jumuiya ya kujihami ya NATO umeongezeka na hasa tangu ulipozuka mgogoro wa Ukraine pamoja na kudunguliwa ndege ya Uturuki mwezi Novemba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment