Thursday, 23 June 2016

KCB yafuturisha wateja wake mkoani Arusha


Benki ya KCB Tanzania imekuwa mwenyeji wa hafla ya futari kwa wateja na wadau wake wa jiji la Arusha. Shughuli hiyo ilifanyika katika hoteli ya kitalii ya Kibo Palace ambapo wageni zaidi ya mia moja walialikwa ili kushiriki pamoja futari katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Moezz Mir alipokuwa akikaribisha wageni wake alisema kuwa mwezi wa Ramadhani ni wakati muhimu wa kushiriki pamoja na kuendeleza umoja na amani nchini.

“Nawashukuru wote kwa kuwa washirika wa muhimu sana kwa benki yetu ya KCB Tanzania.Tunathamini sana uhusiano wetu na nyie na kila mara tunaendelea kutafuta nafasi ya kuweza kuwapa huduma bora zaidi,” alisema Moezz.

Mkurugenzi Mkuu wa benki KCB Tanzania, Moezz Mir akizungumza wakati wa futuru iliyoandaliwa kwa wateja na wadau wa benki hiyo, jijini Arusha.

KCB Tanzania ni benki ya kwanza nchini kwa kutoa huduma ya kibenki kwa kufuata masharti ya dini ya Kiislamu. Huduma hii ya kibenki inafuata maadili ya Sharia hutolewa katika matawi yote ya KCB nchini hata hivyo benki ya KCB pia ina tawi maalum kwa huduma hii ambalo liko Lumumba jijini Dar es Salaam.

Katika bidhaa na huduma zinazotolewa chini ya Sharia ni pamoja na mikopo, uwekaji fedha na uwekezaji.

No comments:

Post a Comment