Tuesday, 28 June 2016

Merkel aionya Uingereza kufuatia kujitenga kwake EU


Kiongozi Mkuu wa Ujerumani bi Angela Merkel ameionya Uingereza isitarajie kuendelea kupata faida ilizokuwa ikizipata katika Umoja wa Ulaya, hata baada ya kuamua kujitenga na Umoja huo.

Akizungumza katika mkutano maalum mjini Berlin kabla ya kwenda Brussels kushiriki katika mkutano wa wakuu wa Umoja wa Ulaya, Bi Merkel amesema ukijiondoa katika familia, huwezi kuendelea kunufaika bila kuwajibika.

Merkel amesisitiza kuwa hayatakuwepo mazungumzo yoyote na Uingereza, yawe rasmi au vinginevyo, kabla ya nchi hiyo kuwasilisha ombi la kujiondoa katika Umoja huo.

Bi Merkel amesema kujiondoa kwa Uingereza, maarufu kama Brexit, hakuwezi kuipotosha Ulaya katika kushughulikia changamoto kubwa zilizopo. Mkutano wa Brussels unajadili hatua ya Uingereza kuondoa uanachama wake katika Umoja wa Ulaya.

No comments:

Post a Comment