Showing posts with label Habari mix. Show all posts
Showing posts with label Habari mix. Show all posts

Saturday, 25 June 2016

Watumishi hewa mkoani Mwanza wazidi kubainika


Serikali imeingia hasara ya Sh2.1 bilioni baada ya kubainika kwa watumishi hewa 1,057 mkoani Mwanza.

Miongoni mwa watumishi hao wamo  watoro, wastaafu, waliofukuzwa, waliofariki dunia, wasiojulikana kwa mwajiri na walioacha kazi na kujiingiza kwenye siasa lakini wanaendelea kulipwa mishahara.

Idadi hiyo ya watumishi hewa imebainika katika uhakiki uliofanyika kati ya Aprili 18 hadi Juni 3, baada ya ule wa awali kuwanasa 334.

Akitoa taarifa ya uchunguzi ulioshirikisha vyombo vya dola na mamlaka nyingine za Serikali, Mkuu Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema, “Niliagiza uhakiki ufanyike upya na watumishi wote waliokuwa masomoni, likizo au safari kurejea kwenye vituo vyao vya kazi kuhakikiwa kwa picha na nakala za miezi mitatu iliyopita ya malipo ya mishahara.”

Monday, 20 June 2016

Raia nane wa Syria wauawa mpakani mwa Uturuki


Makundi ya wanaharakati yanasema kuwa wakimbizi wanane raia wa Syria waliuawa kwa kupigwa risasi na walinzi wa mpaka wa Uturuki walipojaribu kuvuka mpaka kwenda nchini Uturuki siku ya Jumamosi usiku.

Wengi wa waathiriwa wanaripotiwa kutoka familia moja wakiwemo wanawake na watoto.

Jeshi la Uturuki limekana kuwaua wakimbizi na kusema kuwa walinzi walifyatua tu risasi za kutoa onyo.

Shirika moja la uchunguzi lenye makao yake nchini Syria, linasema kuwa hadi raia 60 wa Syria wameuawa mwaka huu wanapojaribu kuvuka kuingia Uturuki.