Saturday, 25 June 2016

Watumishi hewa mkoani Mwanza wazidi kubainika


Serikali imeingia hasara ya Sh2.1 bilioni baada ya kubainika kwa watumishi hewa 1,057 mkoani Mwanza.

Miongoni mwa watumishi hao wamo  watoro, wastaafu, waliofukuzwa, waliofariki dunia, wasiojulikana kwa mwajiri na walioacha kazi na kujiingiza kwenye siasa lakini wanaendelea kulipwa mishahara.

Idadi hiyo ya watumishi hewa imebainika katika uhakiki uliofanyika kati ya Aprili 18 hadi Juni 3, baada ya ule wa awali kuwanasa 334.

Akitoa taarifa ya uchunguzi ulioshirikisha vyombo vya dola na mamlaka nyingine za Serikali, Mkuu Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema, “Niliagiza uhakiki ufanyike upya na watumishi wote waliokuwa masomoni, likizo au safari kurejea kwenye vituo vyao vya kazi kuhakikiwa kwa picha na nakala za miezi mitatu iliyopita ya malipo ya mishahara.”

No comments:

Post a Comment