Saturday, 25 June 2016

UKAWA wamjibu Rais Magufuli, wasema Katiba inawaruhusu kufanya siasa


Mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni amepinga vikali kitendo cha Magufuli kuzuia watu kusema. Ali, "Unapozuia watu kusema unasababisha watu kusema kwa vitendo na wakisema kwa vitendo vitendo hivyo vinakuwa vya uvunjifu wa amani."

Alisema nchi ziizojaa vurugu ni nchi ambazo marais wake walikuwa wanajifanya wababe na watawala kujifanya wana mamlaka zote

Alishangaa pia kiongozi huyo wa Nchi aliposema kuwa atawalinda marais wastaafu kwani marais wastaafu wanalindwa na katiba wala sio kauli zake, aliwataka wasaidizi wake wamsaide aache "kuropoka" kwani kauli zake zinalifarakanisha taifa.

Naye mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia alisema Magufuli amewekwa na katiba ya Tanzania hivyo anashangaa yeye mwenyewe anapoipinga katiba na marais wengine wasingefuata katiba kama yeye anavyofanya leo hii asingekuwa rais wa Tanzania na kwamba hawezi kukataza siasa kwa kuwa ipo kikatiba na vyama vipo kisheria.

Aliongezea bila mgongano wa mawazo na demokrasia hakuna maendeleo hivyo.

Naye Peter Msigwa alisema Magufuli anaonekana anapata ushauri wa kijeshi kuliko wa kisiasa, alimtaka kutumia ushauri wa kisiasa kwani vyama vya upinzani vina wafuasi wengi na haitakiwi kutumia nguvu kama anajua maana ya siasa.

Alisema ni kweli nchi ilikuwa na ufisadi na ukosefu wa nidhamu nchini kutokana na utawala wa Kikwete kuwa dhaifu lakini pamoja na kuwa na nia nzuri ya kuondoa vitu hivyo vyote havimpi uhalali wa kufanya mambo bila kutumia sheria na taratibu zilizowekwa na wanamtaka avifanye kwa kutumia sheria.

No comments:

Post a Comment