Saturday, 25 June 2016
Mbunge CCM amtetea Rais John Magufuli
Kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa siku kadhaa zilizopita kuwa ‘siasa sasa basi isubiri mpaka 2020’ imeendelea kuzua gumzo miongoni mwa wabunge wa upinzani.
Hata hivyo, wakati wabunge hao wakiilalamikia, Mbunge wa Karagwe (CCM), Innocent Bashungwa amesema haoni kwa nini watu wameitafsiri vibaya kauli hiyo, wakati ilikuwa na nia njema.
“Rais Magufuli alikuwa anamaanisha kuwa uchaguzi umeisha, tushirikiane kwa pamoja bila itikadi ili tuijenge nchi yetu jambo ambalo ni zuri kabisa,” alisema Bashungwa.
Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe jana alipozungumza na vyombo vya habari, alisema hawatakubaliana na kauli ya Rais Magufuli ya kukataza mikutano ya shughuli za siasa hadi mwaka 2020 na kama hivyo ndivyo, Serikali iandae magereza ya kutosha.
Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alisema kutokana na kauli hiyo kuwa nzito, vyama vinavyounda umoja huo vitakutana na kujadiliana kabla ya kutoa msimamo wa pamoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment