Saturday, 25 June 2016
Boris Johnson kushika hatamu za Waziri Mkuu Uingereza
Meya wa zamani wa London mji mkuu wa Uingereza Boris Johnson ambaye aliongoza kampeni ya kujiondoa katika Umoja wa Ulaya anatarajiwa kuwa miongoni mwa watakaowania wadhifa wa Waziri Mkuu, pale David Cameron atakapoondoka baada ya kutangaza kujiuzulu ifikapo mwezi Oktoba.
Hatua ya Cameron kutangaza kujiuzulu inatokana na raia wa nchi hiyo kuamua kujitenga na umoja huo katika kura ya maoni iliyofanyika juzi. Johnson amewahakikishia wapiga kura kwamba Uingereza imefanya vyema kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.
Wakati huo huo kiongozi mkuu wa Scotland Nicola Sturgeon amesema kwa vile idadi kubwa ya raia wa Scotland walipiga kura ya kutaka kubakia katika Umoja wa Ulaya hilo linamaanisha sasa kuna uwezekano mkubwa wa nchi hiyo kupiga kura upya ya kutaka kujitenga na Uingereza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment