Saturday, 25 June 2016

Obama kuendeleza Uhusiano wake kwa Uingereza na EU

Rais wa Marekani Barack Obama amewahakikishia Waingereza kwamba matokea ya kura ya maoni hayatoharibu uhusiano mzuri uliopo baina nchi hizo mbili.

Obama ambaye aliwahi kuisihi Uingereza isijiondoa katika Umoja wa Ulaya wakati wa ziara yake nchini humo mwezi Aprili, hapo jana alizungumza kwa njia ya simu katika wakati tofauti na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na kuwaahidi kwamba uhusiano wao wa karibu utaendelea kuwepo.

Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya inatishia hatua za kuufufua uchumi wa Marekani pamoja na kuwatia wasiwasi washirika wa Marekani katika masuala ya usalama wa kimataifa.

No comments:

Post a Comment