Saturday, 25 June 2016

Hezbollah kutuma wapiganaji wake Syria


Kiongozi wa kundi la Hezbollah la Lebanon amesema jana kuwa kundi hilo litatuma wapiganaji zaidi katika jimbo la Aleppo nchini Syria, ambapo vikosi vinavyounga mkono upande wa serikali vinapambana na makundi ya waasi wa Syria katika maeneo mbalimbali.

Hassan Nasrallah ametoa ahadi hiyo licha ya kwamba kundi hilo la madhehebu ya Kishia linalomuunga mkono Rais wa Syria Bashar Al-Asaad limeshindwa vibaya mwezi huu katika mapigano yanayoendelea katika jimbo hilo la Aleppo.

Nasrallah amekiri kupoteza wapiganaji 26 katika mapigano hayo mwezi huu pekee lakini pia amedai kuwa zaidi ya wapiganaji 600 wameuawa upande wa adui wao.

Katika hotuba yake ya kumkumbuka Mustafa Badreddine aliyekuwa kamanda wa kundi hilo la Hezbollah ikiwa zimetimia siku 40 tokea alipouawa nchini Syria Nasrallah ameyataja mapigano yanayoendelea mjini Aleppo na jimbo zima kwa jumla kuwa ni mapambano makubwa ya vita nchini Syria.
 

No comments:

Post a Comment