Thursday, 30 June 2016
Jambazi sugu Dar mikononi mwa Polisi
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa sugu wa ujambazi aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu Abdallah Bushiri Said ambaye anadaiwa kushiriki matukio mbali mbali ya Uporaji na mauaji ambaye pia anadaiwa kuwa mshirika Mkuu wa Abuu Seif aliyeuawa juzi wakati wa mapambano na Polisi eneo la Buguruni jijini Dar es salaam.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum CP Simon Siro amesema mtuhumiwa huyo ambaye anashikiliwa amekiri kuhusika na matukio makubwa ya unyang’anyi wa kutumia silaha ikiwemo ya mabenki, matukio ya uporaji wa silaha katika vituo vya polisi likiwemo la sitaki shari.
Aidha, jeshi hilo limetangaza kumsaka mtuhumiwa mwingine hatari wa ujambazi Heri Suleiman Mpopezi mwenye asili ya Pemba ambaye alikuwa mwajiri wa kikosi cha JKU Zanzibar na kuacha kazi na kujitumbukiza katika ujambazi wa kutumia silaha.
Labels:
Ulinzi na Usalama
Location:
Dar es Salaam, Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment