Zaidi ya watu milioni moja wamesaini waraka wakitaka kuitishwa mara ya pili kwa kura ya maoni baada ya upande wa kundi linalounga mkono kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya kushinda kufuatia kura za maoni zilizopigwa Alhamisi wiki hii.
Duru kutoka nchini Uingereza zinaonesha kuwa Tovuti ya bunge la nchi hiyo kwa wakati fulani ilionekana kuelemewa kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa wakitia saini waraka huo wakitaka kuitishwa upya kwa kura ya maoni.
Waliosaini waraka huo wanaitaka serikali ya nchi hiyo kuitisha upya kura hiyo ya maoni kwa kuzingatia kanuni ya kuwa iwapo idadi ya wanaounga mkono kubakia au kuondoka itakuwa chini ya asilimia 60 kutokana na idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura kuwa chini ya asilimia 75 basi lazima kuitishwe kura nyingine ya maoni.
Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura hiyo ya maoni Alhamisi iliyopita ilikuwa asilimia 72.2. Hadi hapo jana watu milioni moja na elfu arobaini walikuwa tayari wamesaini waraka huo katika tovuti maalumu ya serikali na bunge ikiwa ni mara kumi zaidi ya saini laki moja zinazohitajika kwa ajili ya pendekezo linalowasalishwa kupata nafasi ya kujadiliwa na bunge la nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment