Sunday, 26 June 2016

Mripuko wa Bomu waua wanne mjini Benghazi, Libya

Maafisa wa usalama na Afya nchini Libya wamesema bomu lililokuwa limetegwa katika gari limeripuka nje ya hospitali katika mji wa Benghazi nchini humo na kuwaua watu wanne na kuwajeruhi wengine 14.

Afisa mwandamizi wa jeshi nchini Libya Brigedia Jenerali Abdul-Salam al-Hassi amewashutumu wanamgambo wa kundi la itikadi kali kwa kuhusika na shambulizi hilo lililotokea hapo jana.

Shambulizi hilo lililitokea nje ya hospitali ya Jalal nchini humo. Polisi wa kijeshi walilazimika kuweka kizuizi katika  eneo hilo la hospitali baada ya kutokea kwa mripuko ambao ulisababisha moshi mweusi kutanda hadi katika eneo la kuegesha magari.

No comments:

Post a Comment