Waendesha mashtaka nchini Ubelgiji waliwashtaki wanaume wawili kwa makosa ya ugaidi hapo jana, baada ya operesheni kadhaa za msako wa usiku.
Maafisa wamesema hakuna silaha, miripuko au vifaa vyovyote vilivyogunduliwa, lakini wanaume hao wanatuhumiwa kwa kushirikiana na kundi la kigaidi.
Wiki iliyopita maafisa wa Ubelgiji waliwashtaki wanaume watatu kwa makosa ya jaribio la mauaji ya kigaidi. Operesheni kubwa za kupambana na ugaidi zilihusishwa na kuripotiwa kwa kitisho dhidi ya mashabiki wakati wa mechi za michuano ya Euro 2016.
Ubelgiji inaendelea kuwa katika tahadhari ya hali ya juu baada ya mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Kiislamu mwezi Machi.
Waripuaji wa kujitoa mhanga waliwauwa watu 32 katika mashambulizi yaliyoratibiwa dhidi ya uwanja mkuu wa ndege wa Brussels na njia za treni za chini ya ardhi.
No comments:
Post a Comment