Saturday, 25 June 2016
Rais John Magufuli aagiza CCTV camera zifungwe mitaani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa rai ya kufunga CCTV kwenye mitaa, amesema Kinondoni ndio inasifika kuwa na uhalifu mwingi katika nchi hii. Amesema wilaya ya Kinondoni ilikuwa na vitendo vya uhalifu 8,094 na mwaka 2015 vikafika 8,804 huku akitoa agizo kwa TCRA ambao ndio wana wajibu wa ku-monitor simu zote washirikiane na jeshi la polisi. Asietaka kushirikiana na jeshi la polisi aondoke.
Rais Magufuli ameyasemahayo leo wakati akihutubia kwenye hafla ya Uzinduzi wa Kuboresha Usalama wa Raia, iliyofanyika kwenye Viwanja vya BIAFRA, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo Rais Magufuli alikuwa Mgeni Rasmi.
Mbali na hayo, rais Magufuli ameviagiza vyombo vya usalama nchini kuwachukulia hatua za kisheria mara moja makandarasi wote na injia ambao jana waliosimamishwa kazi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kujenga barabara chini ya kiwango jijini Dar es Salaam.
Jana, June 24, 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alizisimamisha kazi na kusitisha mikataba ya Kampuni ya Inshinomya Co. LTD na kuyasimamisha Makampuni mengine ya kujenga barabara ya Germinex construction LTD, Del Monte (T) Ltd na Skol Building Contraction.
Kutokana na kujenga barabara chini ya kiwango na kuagiza makampuni hayo kutopewa tenda yeyote kwenye Mkoa wa Dar es Salaam mpaka Mkuu wa Mkoa atakapojiridhisha na utendaji wa kazi kwa makampuni hayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, akisalimiana na wageni na viongozi walifika kwenye hafla hiyo.
Miongoni mwa waliofika kwenye hafla ya Uzinduzi wa Kuboresha Usalama wa Raia Viwanja vya BIAFRA ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Magufuli, Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mridho Kikwete, Katibu Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi John W.H. Kijazi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Lameck Nchemba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu, mwenyekiti wa mkoa Dar es Salaam, Madabida na wengine wengi.
Mzungumzaji aliyepita ni mkurugenzi wa CRDB, Dr. Charles Kimei na miongoni mwa mambo aliyogusia ni utumbuaji majipu.
IGP Mangu: Mangu amemshukuru Rais Kikwete kwani mpango wa kuliboresha jeshi la polisi ulibuniwa wakati wake.
Tutakaa na wataalam ili kubuni vyanzo fedha ili kutimiza tuliyoyapanga na ni mkakati ili kuboresha huduma tunazozitoa kwa wananchi na kero zote kwa jamii. Mangu anasema wakati Magufuli anafungua bunge alisema ‘Serikali nitakayoiunda nataka ihudumie jamii kwa haraka’ hivyo mpango wao unajibu hilo tatizo.
Amesema mkuu wa mkoa asaidie pia wananchi watakuwa wamejisaidia wenyewe kwa kuweka taa kwenye nyumba zao mbele na nyuma kwani jiji la Dar es Salaam liko kwenye giza. Mangu anasema Bilioni 27 zinahitajika ili jiji la Dar es Salaam liwe kwenye kiwango cha juu cha usalama pengine kuliko majiji yote Afrika.
Mwigulu Nchemba: Mwigulu amewataka wananchi wawe wanatoa taarifa ili kuzuia uhalifu, amemuomba Rais Magufuli kupata fedha za kuweza kutekeleza mpango wa jeshi la polisi ili kuundoa uhalifu kwenye jiji la Dar es Salaam ambayo pia itavutia wawekezaji. Amesema hadhara sio ya kwake na alikuwa anachomeka, anamkaribisha Rais Magufuli.
“Hamna demokrasia ambayo haina mipaka, mpango wa jeshi la polisi unatarajia kuanza utekelezaji wake Julai 1, 2016.” Alisema Mwigulu.
Rais Magufuli: Kwa niaba ya watanzania, niwashukuru wananchi wa Dar kwa kuweza kuacha shughuli zenu na kuja kuhudhuria, wateni wenzangu wakwere wanasema shughuli ni watu. Nawashukuru CRDB, NMB pamoja na Super doll ambao wakurugenzi wao wako hapa, pia nashukuru nchi ya Malaysia ambao ndio wamesaidia uanzishwaji wa big results now (BRN) na mimi nakushukuru kwa kuona matokeo ya big results now.
Nashukuru watu wa Biafra kwa kunipa kura nyingi.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Dar es Salaam, Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment