Thursday, 30 June 2016

Amerika Kaskazini watetea Utandawazi


Viongozi wa Marekani, Canada na Mexico wamekataa kwa kiasi kikubwa mpango wa kulinda biashara na kutokuunga mkono utandawazi katika mkutano wa viongozi wa Amerika kaskazini uliofanyika siku ya Jumatano mapema wiki hi.

Rais wa Marekani Barack Obama, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau na rais wa Mexico Enrique Penya Nieto walisifu faida za mkataba wa biashara huru wa Amerika kaskazini (NAFTA) uliodumu kwa miaka 22 katika wakati ambapo biashara za kimataifa zinashambuliwa Marekani na Ulaya . Kwa pamoja nchi hizo tatu zinajumuisha asilimia zipatazo 27 ya uchumi duniani.

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau alisema mkutano huo ulikuwa wa huzuni kidogo kwasababu ya kile alichokiita matarajio ya kustaafu rais Obama. Watatu hao walieleza urafiki wao wa karibu na jinsi wanavyoheshimiana na kusisitiza neno la “3 amigos” –ikimaanisaha marafiki watatu jina la utani ambalo vyombo vya habari vimewapa.

Obama, Trudeau na Pena Nieto walikubaliana kuunga mkono uzalishaji wa nishati safi kwa Amerika kaskazini katika miaka 10 ijayo wakilenga kuzalisha nusu ya umeme wa Amerika Kaskazini kutoka kwenye vyanzo visivyokuwa Carbon ifikapo 2025.

No comments:

Post a Comment