Showing posts with label Madini na Nishati. Show all posts
Showing posts with label Madini na Nishati. Show all posts
Tuesday, 28 June 2016
Vituo vya mafuta Nchini Kenya vyanyang'wa leseni
Tume ya kudhibiti nishati nchini Kenya (ERC), imevipokonya leseni vituo vya mafuta kwa kuuza mafuta machafu.
Uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa mafuta ya diesel na petroli, yalikuwa yamechanyanywa na mafuta taa pamoja na bidhaa zingine.
Hata hivyo ni vituo vichache viliathiriwa kwa sababu asilimia 96.1 ya vituo vyote vilivyofanyiwa uchunguzi viligunduliwa kuwa na mafuta safi.
Tume hiyo ilianzisha mpango wa kuchunguza mafuta mwaka 2015 ili kuwawezesha wauza mafuta, kuhakikisha kuwa mafuta yao ni safi kabla ya kuyauza.
Labels:
Madini na Nishati
Location:
Nairobi, Kenya
Helium yagunduliwa Tanzania
Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
Baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalum wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.
Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.
Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia.
Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.
Mnamo mwaka wa 2010 Mwanafizikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.
Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalam kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen.
''Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI'' alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford.
Labels:
Madini na Nishati
Location:
Tanzania
Subscribe to:
Posts (Atom)