Friday, 24 June 2016
Uingereza yajing'oa EU, Kenya wataathirika vipi?
Gavana wa benki kuu ya Kenya amejiunga na gavana wa benki kuu ya Uingereza na mataifa mengine kujiandaa kwa mdororo wa sarafu za mataifa yao kufuatia kauli ya Uingereza kujiondoa kwenye muungano wa Ulaya.
Gavana Patrick Njoroge kupitia kwa taarifa kwa vyombo vya habari amesema kuwa wakotayari kusaidia soko la ubadilishani wa fedha iwapo kauli hiyo ya waingereza itaathiri pakubwa sarafu ya Kenya. Kenya ambayo ilitawaliwa na Uingereza wakati wa ukoloni inauhusiano wa karibu sana na taifa hilo.
Asili mia 52% ya waingereza walipiga kura wakitaka nchi hiyo ijiondoe kwenye muungano wa Ulaya.
Aidha biashara nyingi na haswa zile za uuzaji wa bidhaa nje ya nchi hiyo huelekea Uingereza.
Kauli hiyo inafuatia tangazo la gavana wa benki kuu ya Uingereza Mark Carney,muda mchache uliopita kuwa hawatasita kamwe kuingilia kati endapo thamani ya sarafu ya Uingereza itaporomoka zaidi kufuatia kauli ya waingereza kujiondoa.
Bwana Carney anasema kuwa benki hiyo imejiandaa na mpango mbadala wa kuepuka mdororo wa kiuchumi unaotarajiwa katika siku za hivi punde.
Uamuzi huo wa Uingereza umesababisha kudorora pakubwa kwa sarafu ya Uingereza.
Huko Afrika Kusini, soko la hisa la Johannesburg limeporomoka kwa asilimia 4%, huku kukiwa na shauku kutoka kwa wadadisi kuwa huo ndio mwanzo tu wa msukosuko katika uchumi wa ulimwengu kuhusiana na kura hiyo ya kujiondoa ya Uingereza.
Uamuzi huo wa Uingereza umesababisha kudorora pakubwa kwa sarafu ya Uingereza ya Sterling Pound mbali na kuyumbisha soko la biashara duniani.
Katika soko la hisa jijini London, mdororo wa asilimia 8 ulishuhudiwa na kuweka historia chini kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa kipindi cha miaka 30.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment