Showing posts with label Matukio. Show all posts
Showing posts with label Matukio. Show all posts

Wednesday, 13 July 2016

Mtoto anusurika kuliwa na ndege tai Australia


Tai mmoja mkubwa nusura afanye kitendo cha kustaajabisha ,,, tai huyo alijaribu kumtwaa mvulana mmoja na kupaa naye nchini Australia.

Umati wa watu uliokuwa katika hifadhi ya Alice Springs Desert Park ulipigwa na butwaa tai huyo alipojaribu kumbeba mtoto wakati wa kurekodi kwa onyesho moja la wanyama pori.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa ''ilikuwa ni kama tai huyo aliona mnyama mdogo ambaye alitaka kumfanya mlo wake''

Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa ''ilikuwa ni kama tai huyo aliona mnyama mdogo ambaye alitaka kumfanya mlo wake''.

Mvulana huyo anayekisiwa kuwa kati ya miaka 6-8 aliepuka kwa kupiga kamsa na mwishowe ndege huyo mkubwa akapaa na kutoweka.

Mvulana huyo alitibiwa baada ya makucha ya ndege huyo kumgwara usoni.

Hata hivyo wahudumu wa hifadhi hiyo waliingilia kati na kumfukuza tai huyo.

Bi Christine O'Connell kutoka Horsham katika jimbo la Victoria aliyenasa tukio hilo kwa kamera anasema tai huyo alimvamia mtoto huyo akijaribu kumuinua.

Hata hivyo wahudumu wa hifadhi hiyo waliingilia kati na kumfukuza tai huyo.

Wasimamizi wa hifadhi hiyo wamemuondoa tai huyo kwenye onyesho hilo.

Waandalizi wa onyesho hilo walifungasha virago vyao kwa haraka baada ya tukio hilo maarufu.

Wasimamizi wa hifadhi hiyo wamemuondoa tai huyo kwenye onyesho hilo.

Saturday, 9 July 2016

Jerry Muro anusurika ajalini


Muda mchache baada ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kumfungia mwaka mmoja Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro, bahati mbaya kapata balaa jingine.

Kwa mujibu wa salehjembe. blogspot, Muro amekumbana na ajali ya gari akiwa njiani kutoka Machame kijijini kwenda Machame mjini ambako yuko mapumzikoni.

Gari alilokuwa akiendesha liliteleza na kwenda kugonga kwenye karavati na tairi kupasuka.

“Hakika nimenusurika, unajua huku Machame ni milima. Halafu sasa kuna utelezi kutokana na mvua ingawa si kubwa, sasa wakati nateremka, gari likateleza na kwenda kugonga lile karavati,” alisema Muro.

“Lakini namshukuru Mungu, nimepona. Nilipata shida kupiga jeki kwenye tope mwisho nimefanikiwa na baada ya hapo nitaanza safari ya kwenda Dar es Salaam.”

Muro amefungiwa bila ya kupata nafasi ya kujitetea kwa kuwa wakati barua ya mwito kwenda TFF kwa ajili ya kusikilizwa inapelekwa, yeye alikuwa Machame mapumzikoni kwa ajili ya sikukuu.

Monday, 27 June 2016

Mtoto ashambuliwa na fisi Afrika Kusini


Maafisa wa mbuga ya wanyamapori nchini Afrika Kusini wamewashauri wageni kuwa makini, baada ya fisi kumshambulia mtoto wa umri wa miaka 15 alipokuwa amelala ndani ya hema katika mbuga ya Kruger.

Msemaji wa mbuga za wanyamapori William Mabasa, aliwashauri wageni kuchukua tahadhari kila wakati, kwa kuwa kuna wanyamapori wanaowazunguka, na kuwataka wahakikishe kuwa hema zao zimefungwa vizuri.

Mtoto huo alifanyiwa upasuaji ili kupata matibu kwenye mdomo, kutokana na majeraha aliyoyapata kufuatia shambulizi hilo.

Sunday, 26 June 2016

Thelathini wafa kwa ajali China


Watu 30 wamefariki dunia katikati mwa China katika ajali ya basi moja lililoungua moto kufuatia kuanguka pembeni mwa barabara.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari abiria 56 walikuwamo ndani ya basi hilo ambapo majeruhi 21 walikimbizwa hospital kwa matibabu zaidi.

Katika video iliyoonyeshwa na shirika la utangazaji la CCTV, kulionekana moshi mweusi na mzito kutoka katika basi ambapo mamlaka za mji zinasema ajali hyo huenda imesababishwa na kuvuja kwa mafuta baada ya basi hilo kuanguka pembeni mwa barabara.

China inakabiliwa na kiwango kikubwa cha ajali za barabarani ambapo inakadiriwa kuwa watu 250,000 hufariki kila mwaka kutokana na ajali.

Wednesday, 22 June 2016

Diwani anusurika kichapo kutoka kwa wananchi wake


Diwani wa kata ya Nyankumbu wilaya na Mkoa wa Geita Michael Kapaya kupitia CCM amenusurika kupigwa na wananchi wakimtuhumu kuitisha mkutano wake na kutaka kuwachagulia mabalozi wa mitaa kwa kutumia kofia chama chake.

Tukio hilo lilitokea jana katika mtaa wa Nyantorotoro A kata ya Nyankumbu wilayani Geita ambapo inadaiwa mkutano huo
ulioitishwa na diwani Kapaya bila kuwajulisha viongozi wa mtaa huo uliibua sintofahamu kubwa kwa wananchi wengi wakihoji  nini lengo la diwani huyo.

Mwenyekiti wa mtaa huo Gervas Kayelelo amesema kitendo cha diwani huyo kuitisha mkutano kwenye mtaa  bila kuwajulisha wao kwa kutumia kofia ya chams chake ni kinyume na utaratibu.

Wakizungumza na wahandishi wa Habari mara baada ya vurugu kuzimwa na polisi viongozi wa kata hiyo na mwenyekiti wa mtaa diwani Kapaya wamesema lengo la mkutano lilikuwa kujadili wimbi la mauji yanayoendelea katika mtaa huo  na si vinginevyo .

Ahukumiwa miezi 9 baada ya kutembea toka Ufaransa hadi Uingereza


Mwanaume mmoja raia wa Sudan amehukumiwa kifungo cha miezi tisa jela na mahakama moja nchini Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya kutembea kwa miguu kutoka nchini Ufaransa hadi Uingereza akifuata kwa reli.

Abdul Rahman Haroun, ambaye alikiri mashtaka hayo alikuwa amepewa hifadhi nchini Uingereza mwaka uliopita.

Mwanamme huyo wa umri wa miaka 40 anaaminika kutembea umbali wa kilomita 50 kutoka Calaisin nchini Ufaransa, hadi Folkestone nchini Uingereza kabla ya kupatikana tarehe 4 mwezi Agosti mwaka uliopita.

Hata hivyo hawezi kufungwa jela kutoka na kipindi ambacho tayari amekuwa kizuizini.

Tuesday, 21 June 2016

Nyumba zateketea kwa moto wilayani Sengerema


Nyumba kadhaa katika Kisiwa cha Kivuvi cha Mchangini wilayani Sengerema Mkoani Mwanza ziliteketea kwa moto usiku wa kuamkia Jana.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Buhama, Bw. Mussa Mwilomba, aliliambia "The Citizens" kwa njia ya simu kuwa chanzo cha moto huo kilianzia kwenye nyumba ya Bw. Frank Wilson aliyekuwa akichoma kunguni na viroboto katika Banda la mbwa.

Mwilomba alisema, "Moto ulianza kwenye nyumba ya Bwana Frank na ulianza kusambaa taratibu kwenye nyumba za jirani na ghafla ulikuwa mkali."

Taarifa kutoka kwa Afisa Mtendaji huyo zinasema wakazi wa kisiwa hicho walikusanyika pamoja huku wakishuhudia nyumba na mali zao zikiteketea bila msaada wowote.

Kamishna wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab Track hakuweza kufika eneo la tukio katika jitihada serikali za kukabiliana na baa hilo.

Sunday, 19 June 2016

Ndege ya Jeshi la Syria yaanguka

Ndege ya kivita ya jeshi la Syria imeanguka muda mfupi baada ya kuruka katika uwanja wa ndege wa Hama. Chanzo cha kijeshi kimesema hitilafu za kiunfundi ndio chanzo cha ajali hiyo. Hata hivyo chanzo hicho, ambacho kimenukuliwa na chombo cha habari cha serikali cha Syria hakijaeleza ajali hiyo imetokea wapi au kutoa maelezo zaidi.

Ndege kadhaa za kijeshi zilizotengenezwa Urusi zimekuwa zikiangkua tangu mwanzoni mwa mwaka huu kutokana na hitalifu za kiufundi jambo ambalo wataalamu wanasema linatokana na uchakavu. Duru kwa upande wa uasi zililiambia shirika la habari la Uingereza Reuters kwamba ndege iliyoanguka ni aina ya Mig 21 jambo ambalo halijaweza kuthibitishwa.

Washambuliaji wavamia ukumbi wa Muziki Istanbul

Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti kundi la washambuliaji 20 waliokuwa wamebeba fimbo na chupa, waliwavamia mashabiki waliokuwa wamekusanyika mjini Istanbul kusikiliza nyimbo za albamu mpya ya bendi ya Radiohead.

Shirika la habari la kibinafsi la Dogon lilitangaza jana kwamba mtu mmoja alikuwa amejeruhiwa katika tukio hilo. Eneo hilo lilikuwa limefungwa tangu asubuhi. Mabango ya matangazo yaliyokuwa yamewekwa ukutani kwa ajili ya onyesho hilo yalionekana kuchanwa.

Rayka Simon ameliambia shirika hilo la habari la Dogon  kuwa watu waliokuwa wanakunywa bia na kuzungumza wakati wapovamiwa na kuanza kurushiwa chupa na kundi la watu kiasi ya watu 20. Video iliyorushwa mtandaoni ikionyesha tukio hilo, inaashiria kuwa watu hao walichukizwa na mashabiki hao kunywa bia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Saturday, 18 June 2016

Mtu aliyesadikika kuwa jambazi auwa akiwakimbia Polisi


Mtu anayesadikiwa kuwa jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akifanya jaribio la kuwatoroka polisi waliomkamata akiwa na silaha ya kivita aina ya AK 47 aliyoficha kwenye mfuko wa kuwekea kompyuta mpakato.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo amemtaja aliyekamatwa na silaha hiyo kuwa alitambulika kwa jina la Benjamin Wales (Singano).
Amesema alikamatwa jana saa 11.30 jioni katika kizuizi cha  polisi kilichopo Chekelei, Wilaya ya Korogwe katika barabara kuu ya Segera - Njiapanda ya Himo akisafiri na basi la kampuni ya Lakome likitokea Karatu kwenda Dar es salaam.
Kamanda Paulo alisema baada ya askari kulisimamisha basi hilo na kufanya upekuzi walibaini kwenye mfuko wa Benjamin umewekwa nguo pamoja na silaha aina ya AK 47, magazine mbili na risasi 37 vyote vikiwa vimefungwa na karatasi la nailoni.

Auawa kwa risasi akiwa anaangalia video Facebook


Mtu mmoja nchini Chicago alipigwa risasi akiwa katika video ya moja kwa moja inayojulikana kama Live_stream katika mtandao wa Facebook ,polisi wamesema.
Antonio Perkins mwenye umri wa miaka 28 alipigwa risasi katika kichwa na shingo magharibi mwa mji huo.
Kanda hiyo ya video bado iko katika facebook na imeangaliwa mara 700,000.
Ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu mjini Chicago ambapo mauaji yamefanyika moja kwa moja katika mtandao wa facebook.
Mnamo mwezi Machi mtu asiyejulikana alipigwa risasi mara 16 wakati akipeperusha matangazo hewani.
Hakuna mtu aliyekamatwa kufika sasa.Programu ya live-streaming ya facebook inawaruhusu watu kutangaza moja kwa moja mtandaoni .

Watano wa familia moja wateketekezwa kwa moto Burundi


Watu wasiopungua watano kutoka familia moja wameuawa kwa kuchomwa moto wakiwa hai katika kijiji cha Bucana, Wilayani Gitobe, mkoani Kirundo, kaskazini mwa Burundi.

Kwa mujibu wa Mshauri wa Mkuu wa wilaya Gitobe, wahanga kabla ya kuchomwa moto na kuteketea ndani ya nyumba yao, walichomwa visu.

Afisa huyo ameongeza kwamba idadi ya watu walioteketea kwa moto inaweza kuwa kubwa zaidi: "inasadikiwa kuwa kuna watoto ambao walikua ndani ya nyumba hiyo, ambao hawakupatikana, kutokana na moto mkali ambao ulikua ukiwaka, " amesema Mshauri wa Mkuu wa Wilaya ya Gitobe.

Visa vya mauaji vimekithiri katika nchi hiyo ndogo ya Afrika ya Kati. Burundi ni nchi ya Ukanda wa Maziwa Makuu ambayo imeathirika na mauaji, hasa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe viliyodumu zaidi ya mwongo mmoja, baada ya kuuawa kwa rais wa kwanza kutoka kabila la Wahutu, Melchior Ndadaye aliyechaguliwa mwaka 1993 kuliongoza taifa hilo, ambalo kwa miaka zaidi ya 60 lilikua likiongozwa na kabila moja tu ya Watutsi.

Mashirika yanayotetea haki za binadamu yanabaini kwamba watu zaidi ya 270,000 wamelazimika kuyahama makazi yao na kukimbilia katika nchi jirani na Ulaya kwa kuhofia maisha yao, na wengine waliosalia nchini humo wameendelea kushuhudia visa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mauaji, uporaji, unyanyasaji, ... Mashrika hayo yameendelea kuishtumu serikali kuhusika na visa vyote hivyo vinavyoendelea kushuhudiwa nchini humo.

Hata hivyo Serikali imetupilia mbali tuhuma hizo, ikisema kwamba mashirika hayo ndio yamekua yakichochea chuki na mauaji ili yaweze kufikia madaraka.

Thursday, 16 June 2016

Mbunge wa Chama cha Labour auawa


Mbunge wa chama cha Leba nchini Ungereza Jo Cox ameaga dunia baada ya kupigwa risasi na kuchomwa kisu akiwa kwenye mkutano katika eneo lake la ubunge kaskazini mwa uingereza.
Cox Ndiye mbunge wa kwanza kuuawa nchini Uingereza tangu Ian Gow auawe mwaka 1990.
Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 52 aliyetajwa na majirani kama mtu asiye na marafiki amekamatwa na silaha kupatikana.
Walioshuhudia wanasema kuwa mbunge huyo aliingilia kati mzozo kati ya wanaume wawili eneo ambapo alikuwa akikutana na watu eneo lake la ubunge.
Mtu mmoja aliyeshuhudia alisema risasi ilifyatuliwa wakati Bi Cox aliingilia kati.
Kisha muuaji akaanza kumchoma kisu alipokuwa amelala chini.

Nyumbani ni nyumbani tu, wafanya Harambee ya madawati 70

Katika hatua nyingine, Umoja wa wanafunzi waliohitimu shule ya msingi Bunge mwaka 1991 umetoa madawati 70 kwa Shule hiyo ya jijini dsm ikiwa ni jitihada za kuunga Mkono kampeni ya kuondoa upungufu wa madawati katika shule za mkoa wa dsm pamoja na Harambee inayofanywa na kituo cha Chanel ten kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa DSM ya kuhamasisha jamii kuchangia madawati katika Shule za msingi na Sekondari jijini DSM.
Mkuu wa Mkoa wa dsm Paul Makonda akizungumza kabla ya kupokea Madawati hayo kwa niaba ya Shule, amesema moyo ulioonyeshwa na Umoja huo katika kuchangia madawati unapaswa kuigwa na jamii, ambapo pia ametoa wito kwa wananchi wazalendo kuchangia mpango huo kwa kuwa tatizo la madawati bado kubwa katika shule za jiji la Dsm.
M/kiti wa kamati ya kukusanya madawati mkoa dsm Hamid Abdurahman akizungumza kwenye tukio hilo amesema baadhi ya taasisi, mabenki, mashirika na watu binafsi wameendelea kujitokeza kuchangia madawati kupitia kampeni ya Chanel ten kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa DSM kufanya harambee.

Zaidi maiti 30 zaokotwa Jangwani Niger


Miili ya watu 34, 20 kati yao wakiwa watoto imeokotwa ikisadikiwa walikuwa wakijaribu kuvuka jangwa nchini Niger. Maafisa wa serikali wamesema wanaamini kwamba waathirika walikuwa wahamiaji wanaosafiri kaskazini kwa matumaini ya kufika Algeria au Ulaya.

Wizara ya mambo ya ndani ya Algeria ilitangaza ugunduzi huo Jumatano.Taarifa kwenye televisheni ya taifa imeeleza kwamba wanawake tisa, wanaume watano na watoto 20 walifariki dunia baada ya kutekelezwa kwenye jangwa na wasafirishaji haramu wa binadamu.

Utaifa wa waathirika hao bado haujatambulika .Taasisi ya kimataifa ya Uhamiaji inasema uhamiaji kutoka Afrika kusini mwa jangwa la Sahara kuelekea Ulaya umeongezeka kwa kiasi kikubwa katika maeneo ya Afrika magharibi na kati katika siku za karibuni.

Mwili wa aliyekamatwa na Mamba wapatikana


Maafisa wa polisi waliokuwa wakiutafuta mwili wa mvulana wa miaka 2 aliyenyakuliwa na mamba katika bustani ya shirika la Walt Disney World mjini Florida wameupata mwili wake.
Waogeleaji waliupata mwili huo ambao ulikuwa hauna majeraha yoyote na wanaamini ni ule wa mvulana huyo wa miaka miwili ambaye alinyakulwia na mamba na kuingizwa ndani ya maji siku ya Jumanne jioni mbele ya familia yake.
Mkuu wa kaunty ya Orange Jerry Demings amesema kuwa jina la mvulana aliyetoweka na mamba huyo ni Lane Graves kutoka Nebraska.
Tangu shambulio hilo mamba watano walikamatwa na kuuawa kwa lengo la kutafuta mabaki ya mwili wa kijana huyo.
Mwili uliopatikana majini bado haujatambuliwa rasmi lakini maafisa wa polisi wana imani ni ule wa Lane.
Mapema siku ya Jumatano maafisa wa polisi walisema kuwa hakuna tashwishi kwamba mvulana huyo alifariki.

Habari kutoka Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LEO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

• WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI WILAYANI ILEMELA NA NYAMAGANA.

KWAMBA MNAMO TAREHE 14.06.2016 MAJIRA YA SAA 10:30HRS KATIKA ENEO LA IGOMBE KATA YA BUGOGWA WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA JONATHAN GABRIEL MIAKA [31] MKAZI WA BUGOGWA AKIWA NA MISOKOTO MIA NNE [400] YA BHANGI KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA ZA NCHI.

INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ANAFANYA BIASHARA YA KUUZA MADAWA HAYO YA KULEVYA KATIKA MITAA MBALIMBALI YA IGOMBE NA ILEMELA PIA, NA PINDI MTUHUMIWA ANAKAMATWA ALIKUWA AKIFANYA MAWASILIANO NA WATEJA WAKE JINSI YA KUWAPATIA BHANGI HIYO.

KATIKA TUKIO LINGINE LA TAREHE TAJWA HAPO JUU MAJIRA YA SAA 13:30HRS KATIKA ENEO LA MWANANCHI WILAYANI NYAMAGANA, ASKARI WAKIWA DORIA WALIFANIKIWA KUMKAMATA RAMADHANI HAMAD MIAKA [24] MKAZI WA NYAKATO AKIWA NA BHANGI KILO TATU [03] KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.

AIDHA INASEMEKANA KUWA MTUHUMIWA AKISHIRIKIANA NA WENZAKE HUFANYA BIASHARA YA KUUZA BHANGI KATIKA MITAA HIYO WANAYOISHI, NDIPO RAIA WEMA WALITOA TAARIFA POLISI NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA AKIWA NA KILO HIZO ZA BHANGI.

WATUHUMIWA WOTE WAWILI WAPO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI, HUKU MAHOJIANO DHIDI YA UHALIFU WANAOUFANYA WA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA BHANGI UKIENDELEA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU MASHITAKA YANAYO WAKABILI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI HASWA VIJANA AKIWATAKA KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA ZA MADAWA YA KULEVYA AMBAYO NI HARAMU NA BATILI KATIKA USTAWI WA NCHI YETU, KWANI JESHI LA POLISI LIMEJIPANGA VIZURI KUHAKIKISHA LINAWATAFUTA WALE WOTE WANAOJIHUSISHA KATIKA BIASHARA HIYO NA KUWAKAMATA KISHA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA KWA AJILI YA KUPEWA ADHABU KALI ILI IWE FUNDISHO KWA WATU WENGINE.

IMESAINIWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.