Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti kundi la washambuliaji 20 waliokuwa wamebeba fimbo na chupa, waliwavamia mashabiki waliokuwa wamekusanyika mjini Istanbul kusikiliza nyimbo za albamu mpya ya bendi ya Radiohead.
Shirika la habari la kibinafsi la Dogon lilitangaza jana kwamba mtu mmoja alikuwa amejeruhiwa katika tukio hilo. Eneo hilo lilikuwa limefungwa tangu asubuhi. Mabango ya matangazo yaliyokuwa yamewekwa ukutani kwa ajili ya onyesho hilo yalionekana kuchanwa.
Rayka Simon ameliambia shirika hilo la habari la Dogon kuwa watu waliokuwa wanakunywa bia na kuzungumza wakati wapovamiwa na kuanza kurushiwa chupa na kundi la watu kiasi ya watu 20. Video iliyorushwa mtandaoni ikionyesha tukio hilo, inaashiria kuwa watu hao walichukizwa na mashabiki hao kunywa bia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
No comments:
Post a Comment