Wednesday, 22 June 2016

Diwani anusurika kichapo kutoka kwa wananchi wake


Diwani wa kata ya Nyankumbu wilaya na Mkoa wa Geita Michael Kapaya kupitia CCM amenusurika kupigwa na wananchi wakimtuhumu kuitisha mkutano wake na kutaka kuwachagulia mabalozi wa mitaa kwa kutumia kofia chama chake.

Tukio hilo lilitokea jana katika mtaa wa Nyantorotoro A kata ya Nyankumbu wilayani Geita ambapo inadaiwa mkutano huo
ulioitishwa na diwani Kapaya bila kuwajulisha viongozi wa mtaa huo uliibua sintofahamu kubwa kwa wananchi wengi wakihoji  nini lengo la diwani huyo.

Mwenyekiti wa mtaa huo Gervas Kayelelo amesema kitendo cha diwani huyo kuitisha mkutano kwenye mtaa  bila kuwajulisha wao kwa kutumia kofia ya chams chake ni kinyume na utaratibu.

Wakizungumza na wahandishi wa Habari mara baada ya vurugu kuzimwa na polisi viongozi wa kata hiyo na mwenyekiti wa mtaa diwani Kapaya wamesema lengo la mkutano lilikuwa kujadili wimbi la mauji yanayoendelea katika mtaa huo  na si vinginevyo .

No comments:

Post a Comment