Wednesday, 22 June 2016
Jiji la Mwanza kuwa la kisasa
Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, inatarajiwa kuwahamisha wakazi wote waliovamia kwenye maeneo yasiyopimwa katika kata za Kisesa, Idetemya, Fera pamoja na Usagara, ili kupisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Jiji la Mwanza la kisasa.
Maeneo mengine husika yatakayoguswa na mpango huo uliotangazwa leo ni kata za Bugogwa, Sangabuye, Buhongwa na Igoma.
Naibu mkurugenzi wa mpango kabambe kutoka Wizara hiyo Amonike Mahenge, ameeleza dhamira ya Serikali Jijini Mwanza, wakati wa kujadili rasimu ya mpango huo, ili iweze kupitishwa na wadau wa ardhi kuwa sheria kamili.
Kupitia mpango huo utakaohusisha ulipaji wa fidia na ugawaji wa viwanja vilivyopimwa kwa Wananchi watakaoguswa na mpango huo, mkuu wa mkoa wa Mwanza John mongela, amesema Serikali haitakuwa tayari kuona maeneo hayo yakivamiwa baada ya rasimu hiyo kupitishwa.
Katika kikao hicho kilichowashirikisha wawakilishi wa Serikali za Mitaa, Madiwani, Wabunge na viongozi wa dini, mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza Adam Mgoyi na John Wanga wa Manispaa ya Ilemela, wakashauri zoezi hilo lisiingiliwe na itikadi za kisiasa.
Mradi wa mpango wa ujenzi wa Jiji la Mwanza la kisasa unatarajiwa kutekelezwa na Kampuni ya washauri ya (Subana), ambayo makao yake makuu yapo nchini Singapore, mji unaotajwa kupangika kimakazi, licha ya kukabiliwa na changaoto za maeneo ya miinuko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment