Tuesday, 21 June 2016
Nyumba zateketea kwa moto wilayani Sengerema
Nyumba kadhaa katika Kisiwa cha Kivuvi cha Mchangini wilayani Sengerema Mkoani Mwanza ziliteketea kwa moto usiku wa kuamkia Jana.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Buhama, Bw. Mussa Mwilomba, aliliambia "The Citizens" kwa njia ya simu kuwa chanzo cha moto huo kilianzia kwenye nyumba ya Bw. Frank Wilson aliyekuwa akichoma kunguni na viroboto katika Banda la mbwa.
Mwilomba alisema, "Moto ulianza kwenye nyumba ya Bwana Frank na ulianza kusambaa taratibu kwenye nyumba za jirani na ghafla ulikuwa mkali."
Taarifa kutoka kwa Afisa Mtendaji huyo zinasema wakazi wa kisiwa hicho walikusanyika pamoja huku wakishuhudia nyumba na mali zao zikiteketea bila msaada wowote.
Kamishna wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab Track hakuweza kufika eneo la tukio katika jitihada serikali za kukabiliana na baa hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment