Tuesday, 21 June 2016

Ashtakiwa kwa kosa la kutaka kumuua Donald Trump

Mwanaume mmoja wa Uingereza,19, ameshtakiwa kwa kujaribu kumpokonya polisi bastola katika mkutano wa hadhara wa Donald Trump mjini Las Vegas katika jaribio la kumuua mgombea huyo mtarajiwa wa Republican katika uchaguzi wa rais.

Kwa mujibu wa kesi iliyowasilishwa katika mahakama moja ya mjini Nevada, Michael Sandford alijaribu kumpokonya bastola polisi katika mkutano wa hadhara wa Jumamosi ulioandaliwa katika ukumbi wa Mystere Theatre kabla ya kuzidiwa nguvu.

Kijana huyo alimwambia afisa wa ulinzi baada ya kukamatwa kuwa aliendesha gari kutoka California hadi Las Vegas ili “kumuua Trump” na alikuwa katika kituo cha mafunzo ya bunduki siku moja kabla, kujifunza namna ya kulenga shabaha kwa sababu hakuwahi kufyatua risasi hapo kabla. Anakabiliwa na kifungo cha zaidi ya miaka 10 jela na faini ya dola za Kimarekani 250,000 iwapo atapatikana na hatia.

No comments:

Post a Comment