Tuesday, 21 June 2016

Waandishi wa Habari wazuiliwa Uturuki

Uturuki imemkamata mwakilishi wa shirika la Waandishi wa habari Wasio na Mipaka, wakimshitaki kwa kueneza kile ilichokiita kuwa ni "propaganda ya kigaidi". Mwanahabari huyo, Erol Onderoglu, alilifanyia kampeni gazeti linalowaunga mkono Wakurdi la "Ozgur Gundem". Maafisa wanashuku kuwapo na mahusiano baina ya gazeti hilo na makundi ya wapiganaji wa Kikurdi.

Maafisa wa Uturuki pia wanamzuilia mwandishi wa habari Ahemr Nesin na msomi Sebnem Korur Fincanci. Watu hao wawili pia walifanya kampeni za kupinga juhudi za kulidhibiti gazeti hilo la Kituruki. Shirika la Waandishi wa habari Wasio na Mipaka limelaani matukio ya kukamatwa wanaharakati hao wa uhuru wa habari likisema ni "ukandamizaji mkubwa wa uhuru wa vyombo vya habari nchini Uturuki".

No comments:

Post a Comment