Thursday, 16 June 2016

Nyumbani ni nyumbani tu, wafanya Harambee ya madawati 70

Katika hatua nyingine, Umoja wa wanafunzi waliohitimu shule ya msingi Bunge mwaka 1991 umetoa madawati 70 kwa Shule hiyo ya jijini dsm ikiwa ni jitihada za kuunga Mkono kampeni ya kuondoa upungufu wa madawati katika shule za mkoa wa dsm pamoja na Harambee inayofanywa na kituo cha Chanel ten kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa DSM ya kuhamasisha jamii kuchangia madawati katika Shule za msingi na Sekondari jijini DSM.
Mkuu wa Mkoa wa dsm Paul Makonda akizungumza kabla ya kupokea Madawati hayo kwa niaba ya Shule, amesema moyo ulioonyeshwa na Umoja huo katika kuchangia madawati unapaswa kuigwa na jamii, ambapo pia ametoa wito kwa wananchi wazalendo kuchangia mpango huo kwa kuwa tatizo la madawati bado kubwa katika shule za jiji la Dsm.
M/kiti wa kamati ya kukusanya madawati mkoa dsm Hamid Abdurahman akizungumza kwenye tukio hilo amesema baadhi ya taasisi, mabenki, mashirika na watu binafsi wameendelea kujitokeza kuchangia madawati kupitia kampeni ya Chanel ten kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa DSM kufanya harambee.

No comments:

Post a Comment