Thursday, 16 June 2016
Mafundi simu waipongeza TCRA ila ............
Chama cha mafundi simu Tanzania – PTT kimeipongeza mamlaka ya mawasiliano Tanzania – TCRA kufikia hatua ya kuzima simu bandia hapa nchini ingawa kinapata hofu ya kupungua kwa wateja kutokana na ukweli kwamba simu zilizokuwa zikiharibika zilikuwa ni bandia ukilinganisha na simu halali.
Kauli hiyo imetolewa jijini dar es salaam na katibu PTT Mrasa Mtoro kwenye semina ya mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani kwa wadau mbalimbali wa mawasiliano ambaye amesema utekelezwaji wa zoezi hilo utaondoa matatizo yaliyokuwa yakiwakabili katika kazi zao ikiwemo namna ya kutengeneza simu bandia ambazo wakati mwingine mfumo mzima unakuwa umeharibiwa hivyo kuwapa wakati mgumu wa kuitengeza na kusababisha ugomvi na wateja wao ambao hawatambui ama wanatambua kuwa simu zao ni bandia.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo kwa niaba ya kaimu mkurugenzi mkuu TCRA, mkurugenzi wa watumiaji na watoa huduma za mawasiliano TCRA Dk Raymond Mfungahema amesema zoezi hili limeonyesha mafanikio kabla ya kutekelezwa kwani uingizwaji wa simu bandia umepungua tangu mamlaka hiyo ilipoanza kutoa elimu ya simu bandia huku watumuiaji wa simu wakiongezeka kwa kasi kutoka laini milioni 3 mwaka 2005 hadi kufikia laini milioni 40 mwaka huu ambazo zimesajiliwa kupitia mitandao mbalimbali ya simu.
Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Paul Makonda amesema ni vema wananchi wakajikita zaidi katika matumizi ya simu halali kuliko kujali thamani ya fedha ya kununulia simu lakini pia ameipongeza TCRA kwa kusimamia sheria zinazolenga kusaidia wananchi na taifa kwa ujumla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment