Monday, 27 June 2016
Benki ya NMB yatoa Mil. 143 Polisi kuimarisha Ulinzi
Benki ya NMB Tanzania imetoa TSh. Mil. 143 katika kuhakikisha usalama wa raia na Mali zaoi unaimarika. Benki hiyo imeunga mkono jitihada za serikali za kuboresha huduma za ulinzi na usalama zinazofanywa na Polisi.
Hivi karibuni, Rais John Magufuli alizindua mpango wa kuboresha Usalama wa Jamii katika viwanja vya Biafra, Dar es Salaam, ambapo pia alizindua moja ya vituo vipya vya Polisi vinavyohamishika vilivyotolewa na Benki ya NMB.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Waziri Barnabas alisema Polisi ipo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa raia na mali zao, hivyo kama benki wameona ipo haja kuunga mkono jitihada hizo za kuboresha ulinzi.
“Ushirikiano tunaojivunia leo unatokana na NMB kuunga mkono ujenzi wa vituo viwili vya polisi vinavyohamishika na kugharamia shughuli hii ya uzinduzi kwa kiasi cha Sh milioni 143 ikiwa ni sehemu ya maboresho makubwa na mabadiliko katika Jeshi la Polisi,” alisema Barnabas.
Aidha, katika hatua nyingine Barnabas alisema Sh bil 28 zimetolewa na kwamba, zaidi ya maofisa wa Polisi 10,000 wanaendelea kunufaika na mikopo ya benki hiyo kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao ya kifedha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment