Monday, 27 June 2016

Uturuki yakasirika kufuatia matamshi ya Papa Francis

Vatican imetoa majibu ya madai ya Uturuki kwamba kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameonyesha "mawazo ya vita vya msalaba" baada ya kutamka mauaji ya waarmenia yaliyofanywa Ottoman kama "mauaji ya kimbari."

Papa Francis amezidisha hasira za waturuki katika ziara yake ya siku tatu katika jimbo la zamani la muungano wa kisovieti la Armenia na kutumia neno hilo kwa mauaji ya siku nyingi ambayo Uturuki inayakanusha kuwa yalikuwa ya kimbari.

Naibu waziri mkuu wa Uturuki Nurettin Canlikli ameyaita matamshi ya Papa kama "bahati mbaya" na kwamba yanaonyesha ishara ya "mawazo ya vita vya msalaba ."

Vatican imekataa madai hayo ikisema kiongozi huyo alikuwa akijaribu kuweka "daraja na sio ukuta" na kwamba hana nia mbaya na Uturuki.

Uturuki ambayo ni nchi ya Kiislamu inakubali kwamba Wakristo wengi wa Armenia waliuwawa katika mapigano yaliyoanza mwaka 1915 lakini inakanusha kwamba mamia kwa maelfu ya watu waliuwawa katika mapigano hayo kustahiki kuitwa mauaji ya kimbari.

No comments:

Post a Comment