Monday, 4 July 2016

Ofisi ya kijiji yageuka kuwa kituo cha Afya


Wakazi wa kijiji cha Sakalilo, Tarafa ya Kipeta wilayani Sumbawanga wanalazimika kutumia ofisi za kijiji hicho kupata huduma za afya ikiwa pamoja na wajawazito kujifungulia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wanawake wa kijiji hicho, walisema wamekuwa wakipata taabu nyakati za kujifungua katika jengo hilo la ofisi ya kijiji, huku shughuli nyingine za kiofisi zikiendelea.

“Inafika mahali uchungu umekubana na ukifikishwa katika ofisi hiyo ya serikali ya kijiji unakuta kuna watu wanaendelea na mashtaka mbalimbali, kunakuwa hakuna usiri wala staha wakati wa kujifungua,” alisema Lucy Mabula.

Mkazi mwingine, Pupe Mwampupe alisema ili kuondoka na kero hiyo na udhalilishaji kwa wanawake, ni vema sasa Serikali ikaharakisha ujenzi wa jengo la zahanati ya kijiji ambalo lilibomoka kutokana na uchakavu.

No comments:

Post a Comment