Monday, 4 July 2016
Mchungaji agoma kumzungumzia Gwajima
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, Adriano Edward amesema hawezi kuzungumza chochote juu ya suala la kiongozi wao huyo.
Hata hivyo, wakizungumza suala hilo baadhi ya waumini wamesema hawajatangaziwa kwamba askofu wao anaumwa bali wamesoma kupitia vyombo vya habari.
“Ni kweli hatumuoni hapa kanisani kwa muda wa wiki tatu sasa, tulidhani yuko nje kwa shughuli za kanisa letu lakini taarifa za kuumwa kwake zimetushtua,” amesema John Maliwa.
Paschal Eliud amesema ingawa ibada zinaendelea kama kawaida, lakini vizuri wakaelezwa aliko askofu wao na lini anarudi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment