Thursday, 16 June 2016
Sheria dhidi ya Ugaidi yaidhinishwa Israel
Israel imepitisha sheria mpya ya kupambana na ugaidi ambayo serikali ya nchi hiyo inayoongozwa na mrengo wa kulia ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu imesema inaimarisha mapambano dhidi ya ugaidi ingawa kwa upande mwingine wakosoaji wanasema sheria hiyo inakwenda kinyume na demokrasia.Kwa mujibu wa radio ya Israel miongoni mwa mambo mengine sheria hiyo inasema kwamba mtu atakayehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la ugaidi hukumu yake hiyo haiwezi tena kupunguzwa katika kipindi cha miaka 15 ya mwanzo.Kadhalika kwa mara ya kwanza hatua ya kuchimba mahandaki imetajwa kama kosa la uhalifu chini ya sheria hiyo mpya.Sheria hiyo mpya ya kupambana na ugaidi Israel ilipendekezwa na chama cha kiyahudi cha siasa kali na imepitishwa na wabunge 57 na kupingwa na wabunge 16 katika bunge la Knesset lenye idadi jumla ya wabunge 120.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment