Tuesday, 21 June 2016
Mtu aliyevaa mkanda bandia ametishia kujiripua leo mjini Brussels
Mtu aliyesema amevaa mkanda wa mabomu ambao ungeripuka kwa kufyatuliwa kwa mbali amesababisha kitisho kikubwa katika eneo la kibiashara mjini Brussels leo kabla ya polisi kugundua kwamba mkanda huo ulikuwa na chumvi na biskuti ndani yake.
Jiji la Brussels limeendelea kuwa katika tahadhari chini ya ulinzi mkali miezi mitatu baada ya washambuliaji watatu wa kujitoa mhanga wa kundi la Dola la Kiislamu walipojiripua katika uwanja wa ndege wa mjini Brussels na katika kituo cha treni na kusababisha watu 32 kuuwawa.
Leo asubuhi polisi wa mjini Brussels walimkamata mtu mmoja karibu na eneo la maduka baada ya kusema kuwa alikuwa amevaa mkanda wa miripuko. Eneo hilo lilifungwa wakati wataalamu wa mabomu wakimpekua mtu huyo.
Mtu huyo aliyezaliwa mwaka 1990 na kutambulika kwa jina la J.B aliwapigia simu polisi binafsi na kusema ametekwa nyara na kulazimishwa kuvaa mkanda wenye miripuko. Imethibitika kwamba si kweli.
Labels:
Ulinzi na Usalama
Location:
Brussels, Belgium
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment