Tuesday, 21 June 2016

Jumla ya Madaktari 700 waliuawa nchini Syria tangu mzozo ulipoanza


Mashambulio dhidi  ya  hospitali  tangu  vita  nchini  Syria vianze  miaka  mitano  iliyopita  yameuwa madaktari pamoja na  wafanyakazi  wa  kutoa  huduma  za  afya 700, wengi wao  kwa  mashambulizi  ya  anga.

Tume  ya  Umoja  wa  Mataifa  ya  uchunguzi  kuhusu Syria  pia  imeshutumu ukiukaji   mkubwa  unaofanywa  na wapiganaji  wa  Jihad  na  kueleza  wasi  wasi  wake kwamba  wanamgambo  wenye  mafungamano  na  Al-Qaeda  huenda  wanawaandikisha  mamia  ya watoto  katika vikosi  vyao.

Kamishna  Paulo Pinheiro  ameliambia  baraza  la  haki  za binadamu  la  Umoja  wa  mataifa  kwamba  mashambulio yenye  malengo  maalum ya  anga  dhidi  ya  hospitali  na kliniki  nchini  Syria, yamesababisha  vifo  vya  raia  kadhaa, ikiwa  ni  pamoja  na  wafanyakazi  muhimu  wa  huduma za  afya.

No comments:

Post a Comment