Wednesday, 22 June 2016

Majeshi ya serikali ya Libya yasonga mbele

Vikosi vinavyoshirikiana na serikali ya muungano nchini Libya vinasema vinasonga mbele katika mapigano yao dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali wa Dola la Kiislam, IS, katika ngome yao ya Sirte.

Msemaji wa vikosi vinavyoiunga mkono serikali ya muungano, Rida Issa amesema wamevikomboa vijiji 700 kusini mwa eneo la kati la Sirte na wamefanikiwa kupata njia ya kuingia magharibi ya mji wa Sirte, akiongeza kuwa wanajeshi 16 wameuwawa na wengine 60 kujeruhiwa kufuatia mapigano hayo ya jana dhidi ya IS. Vikosi vya serikali vimefanikiwa pia kuiteka ghala ya pili ya silaha iliyokuwa ikimilikiwa na IS.

No comments:

Post a Comment