Thursday, 23 June 2016

Jeshi la Ujerumani lapanuliwa Mediterrania

Jeshi la Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Bundeswehr, litakuwa siku za mbele linalinda sio tu mwambao wa Libya, bali pia kuwaandama wafanyabiashara haramu wa silaha. Baraza la mawaziri limekubaliana operesheni ya ukaguzi wa manuari za Umoja wa Ulaya katika Bahari ya Mediterenia, inayojulikana kwa jina la Sophia, ipanuliwe.

Juhudi za kusimamia utekelezaji wa vikwazo vya silaha vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa zimelengwa kuwazuwia wanamgambo wa itikadi kali wa Dola la Kiislam wasipatiwe silaha katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.

Zaidi ya hayo, kwa kupanuliwa shughuli za ukaguzi za manuari za Umoja wa Ulaya, itapatikana njia pia ya kupatiwa mafunzo walinzi wa fukwe za Libya. Uamuzi wa baraza la mawaziri unabidi uidhinishwe na bunge la shirikisho, Bundestag. Hata hivyo, serikali kuu ya muungano inadhibiti wingi wa viti bungeni.

No comments:

Post a Comment