Thursday, 23 June 2016

Rais Putin ailaumu NATO kwa uchokozi

Rais Vladimir Putin wa Urusi ameilaumu Jumuiya ya Kujihami ya NATO kwa kile alichokiita "matamshi makali" na "harakati zake za uchokozi" karibu na mpaka wa Urusi.

Rais Putin ameonya visa kama hivyo vitailazimisha Moscow kuimarisha nguvu zake za kijeshi. "NATO inazidisha maneno na harakati za uchokozi karibu na mipaka yetu," amesema Rais Putin mbele ya wabunge wa nchi hiyo waliokusanyika katika kumbukumbu za miaka 75 tangu Ujerumani ya zamani ya Wanazi ilipoivamia Usovieti.

Rais Putin amezikosoa nchi za Magharibi kwa kukataa mchango wa Urusi kusaidia kukabiliana na adui wa pamoja ambae ni ugaidi wa kimataifa, kama walivyolipuuza onyo la Soviet Union kuhusu Hitler na kama wanavyojaribu kuitenga Moscow katika mzozo wa Ukraine.

Uhusiano kati ya Urusi na nchi za Magharibi umepooza na kufikia kiwango cha vita baridi tangu Moscow ilipolikalia eneo la Crimea mwaka 2014 na kuunga mkono vuguvugu la wanaotaka kujitenga mashariki ya Ukraine.

No comments:

Post a Comment