Monday, 4 July 2016
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ziarani Barani Afrika
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anatazamiwa kuanza ziara yake ya kwanza Afrika – kusini mwa jangwa la Sahara leo Jumatatu, akiwa anatafuta washirika wapya wa kibiashara barani Afrika.
Ingawa ratiba maalum haijatolewa Netanyahu anatazamiwa kuanza ziara yake nchini Kenya na baadaye kutembelea Uganda, Kenya, Ethiopia na Rwanda.
Ziara hiyo pia inaambatana na siku ya kuadhimisha miaka 40 tangu tukio la kuokolewa mateka wa kiyahudi katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda ambapo kaka yake Netanyahu aliuawa,Julai 4, 1976.
Ziara hiyo ya Netanyahu pia inafuatia ziara ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya nchini Israel, Februari 2016
Baraza la mawaziri la Israel liliidhinisha Juni 25 kufunguliwa kwa ofisi za idara ya misaada ya kimataifa ya Israel katika nchi hizo nne. Netanyahu aliliambia baraza lake la mawaziri kuwa ziara hiyo ni “sehemu ya juhudi za kurudi barani Afrika kwa kiwango kikubwa.”
Ziara hiyo inakuja huku Israel ikiwa inazindua mpango wa msaada wa mamillioni ya dolla kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na nchi za afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment