Monday, 4 July 2016

Viongozi wa Dini wapewa jukumu la kukemea maovu


Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo ametaka viongozi wa dini kukemea maovu yanayotendeka katika jamii ikiwemo vitendo vya ufisadi, uhalifu wa kutumia silaha, dawa za kulevya, mauaji ya albino na tabia zingine mbaya zilizopo kwa sababu baadhi ya wanaofanya mambo hayo ni waumini wao.

Akizungumza na viongozi mbalimbali baada ya kufuturisha nyumbani kwake juzi jioni, Ndikilo alisema ana amini viongozi wa dini zote wakisisitiza amani ni rahisi jamii kuelewa wanachoeleza na kufanya, kwa kuwa hakuna dini inayohubiri uhalifu au mauaji.

Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi kukumbuka baadhi ya matukio yaliyowahi kutokea mkoani humo ikiwelo lile na uvamizi wa vituo vya polisi Rufiji, Mkuranga na Kongowe kuwa hivyo ni viashiria vya kupotea amani ambavyo vinaweza vikajirudia, hivyo waisaidie Serikali kuwafichua wahusikia.

Kadhi wa Mkoa huo, Sheikh Abass Mtupa amesema tunahitaji mahusiano mazuri ndani ya jamii bila kuangalia dini, makabila na matabaka ili kuimarisha upendo, amani na mshikamano kwa jamii.

No comments:

Post a Comment