Monday, 4 July 2016

Ajali: Mabasi ya City Boy yaua mkoani Singida


Watu 29 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa leo baada ya mabasi mawili kugongana huko Maweni wilayani Manyoni Mkoa Singida.

Mabasi hayo yanayomilikiwa na Kampuni ya City Boy, moja lilikuwa linasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kahama na lingine lilikuwa linatoka Kahama kwenda Dar es Salaam.

Akizungumzia ajali hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Thobias Sedoyeka amesema idadi ya majeruhi bado haijajulikana japo kuwa amesema ni wengi.

"Nikweli ajali imetokea Maweni na tupo eneo la tukio tunaendelea na utaratibu wa kuondoa majeruhi na maiti," amesema Kamanda Sedoyeka.

 Kamanda Sedoyeka amesema kuwa wanaendelea na juhudi za kuyaondoa mabasi hayo barabarani.

Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia za watu 29 waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment