Tuesday, 5 July 2016

Unamfahamu Rais masikini kuliko wote duniani?


Imezoeleka kuwaona wanasiasa wakiishi maisha ya kifahari kwa kukaa katika majumba makubwa na mahekalu huku wakitembelea magari ya thamani kubwa, pia wapo wanaofanya kila aina ya anasa iliyokuwa katika dunia hii lakini kwa Bw. José Alberto "Pepe" Mujica Cordano ipo tofauti mno.

Bw. Jose Mujica kama wengi wanavyomfahamu alizaliwa kunako mnamo mwaka 1935, mwezi wa 5, tarehe 20, ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe nchini Uruguay.

Mujica, alikuwa mtoto wa mkulima mzee Demetrio Mujica na Lucy Cordano, baba yake alifariki dunia akiwa ana miaka 5.

Alikuwa kuwa Rais wa 40 wa nchi hiyo kati ya mwaka 2010 - 2015. Pia aliwahi kuwa mpiganaji wa msituni na aliwahi kufungwa jela miaka 13 wakati wa utawala wa kimabavu wa kijeshi kati ya mwaka 1970 - 1980.

Mujica, aliwahi kushika wadhifa wa kuwa Waziri wa Mifugo , Kilimo, Uvuvi kati ya mwaka 2005-2008 na baadae kuwa Senator, kabla ya kushinda kiti cha uraisi mwaka 2009 na hatimaye tarehe 1, mwezi machi kuapishwa rasmi.

Asilimia 90 ya mshahara wake wa kila mwezi ambao ulikuwa ni Euro 12,000, alikuwa anawapa watu masikini na wajasiriaamali wadogo katika kipindi cha utawala wake.

Alipoapishwa kuwa raisi alikataa kukakaa katika jumba la kifahari ambalo alipewa na serikali badala yake alikwenda kuishi shambani akiwa na mkewe pamoja na mbwa wao.

Akitokea nyumbani kuelekea Ikulu au katika mizunguko yake binafsi alitumia usafiri wa garii yake 'Mgongo wa Chura" yaani Volkswagen Beetle toleo la mwaka 1987 bila kuwa na msafara wowote.

Kwa wakati huo mwaka 2010 gari hilo lilikuwa na thamani ya dola 1,800, ambapo mwaka 2014 gazeti la Búsqueda la nchini humo liliripoti kuwa Mujica, alipata ofa ya gari yenye thamani ya shilingi dola milionii 1, jibu lake lilikuwa "Kama ningepewa hiyo dola milioni 1 kwa ajili ya gari basi ningechangia katika programu ya kusaidia watu wasiokuwa na mahala kwa kuishi."

Huyo ndio Jose Mujica, Rais  masikini zaidi duniani ambaye alipewa jina la 'Shujaa wa Siasa' au kwa lugha ya kimombo Last hero of politics.

Kuna haja ya viongozi wa kiafrika hususani Tanzania waige mfano kutoka kwa rais huyu wa zamani wa Taifa la Uruguay.

"Mimi nina namna yangu ya kuishi hivyo siwezi kubadilika kwa sababu ya kuupata Urais"
 Jose Mujica.

No comments:

Post a Comment