Saturday, 2 July 2016
Ujerumani yakunwa na Serikali ya JPM
Ujerumani imesema utendaji kazi wa Serikali mpya ya Awamu ya Tano ikiwemo kupambana na rushwa, imeweka nchi katika nafasi nzuri ya uwekezaji katika nchi za Afrika Mashariki.
Hatua hiyo imefanya Ujerumani kurejea katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere, baada ya kutoshiriki kwa zaidi ya miaka 20.
Akizungumza katika maonesho hayo, Mkurugenzi wa Biashara na Uwekezaji wa Ujerumani na Tanzania, Dirk Smelty, alisema pia nchi kuwa katika amani ni moja ya sifa za kuwafanya kuwekeza nchini. Alisema kuna fursa nyingi za uwekezaji nchini, ikiwa ni pamoja na viwanda na miundombinu.
Naibu Balozi wa Ujerumani nchini, John Reyels alisema katika maonesho hayo kampuni nane za Ujerumani zitaonesha bidhaa zenye ubora kuanzia za vifaa vya afya, teknolojia za gesi na mafuta, ujenzi wa nyumba na umemejua. Alisema biashara baina ya nchi hizo mbili zina thamani ya zaidi ya Sh bilioni 700.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment