Friday, 1 July 2016

Uganda na Urusi zavunja mkataba wa ujenzi wa kiwanda cha mafuta


Serikali ya Uganda imevunja mkataba wake na kampuni ya Urusi kuhusu mpango wa kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta.

Serikali ilikuwa imekamilisha mazungumzo na kampuni hiyo ya Rostec Global Resources Consortium.

Lakini inasema baadaye kampuni hiyo ilianza kuongeza masharti mengine hata baada ya makubaliano ya mwisho kufikiwa.

Uganda kukata uhusiano na Korea Kaskazini

Mkataba huo sasa umekabidhiwa kampuni ya SK Engineering kutoka Korea Kusini.
Kampuni hiyo iliibuka ya pili katika shughuli ya kutoa zabuni.

Hatua hiyo imejiri wiki chache baada ya Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye kuzuru Uganda.

No comments:

Post a Comment