Si jambo la kawaida kukataa tuzo hususan kwa Waafrika lakini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameikataa tuzo hiyo kwa madai kuwa jiji lake halijastaili kwani bado ni chafu.
Makalla ameungana na wananchi wa jiji hilo kupinga kutajwa kushinda nafasi ya kwanza kwa usafi nchini, na kudai bado limejaa takataka.
Makalla amesema hajatambua vigezo vilivyotumika kwani jiji halina hata bustani za kupumzika wananchi, limejaa takataka karibu na bustani za maua hususan eneo la Kabwe na mitaa mbalimbali.
Awali Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alilitaja Jiji la Mbeya kwamba limeongoza kwa makundi ya majiji kwa usafi, wakati Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ikiongoza nchini na Kinondoni ikiongoza kwa kundi la manispaa za majiji.
Mkazi wa Uwanja wa Ndege, Daudi Mahenge amesema ipo haja kwa Serikali kutoa taarifa sahihi kwani Mbeya haijawahi kuwa safi.
No comments:
Post a Comment