Jeshi la polisi nchini limeendelea kusisitiza msimamo wake wa kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa mpaka hapo hali ya usalama itakapotengemaa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kamishina wa polisi operesheni na mafunzo makao makuu ya jeshi la polisi nchini Nsato Mssanzya amesema jeshi la polisi halitakubaliana na kauli za uchochezi zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa ambazo zinaweza kuchochea uvunjifu wa amani kwa jamii.
Kamishna Mssanzya amesema jeshi la polisi litaendelea kuimarisha hali ya usalama kwa wananchi wake ikiwemo kulinda usalama wa raia na mali zao huku likiwataka baadhi ya wanasiasa kufuata sheria na taratibu ambazo zimewekwa.
Mssanzya amesema jeshi la polisi limepiga marufuku maandamano pamoja na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa huku likifafanua kuwa jeshi hilo halitaingilia mikutano ya ndani inayofanywa na vyama hivyo.
No comments:
Post a Comment